Sakata la Bernard Morrison, Mtendaji Mkuu Senzo Batha abwaga manyanga Simba SC.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nakumbuka nilisema juzi humu kuwa kuna pahala Simba SC wanakosea. Huwezi kuifanya klabu iendeshwe kwa weledi na wakati huo huo unaiendesha kwa Uhuni wa kizamani.

Nilikuwepo na Social Media Content Manager pande fulani usiku wa Jana. Jamaa akanimwagia mchele chini ya kwamba sakata la BM kusaini Simba SC litaondoka na mtu, Sikumuelewa.

Mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya yalioachwa na kocha Kishingo alikuwa nayo mtendaji mkuu wa klabu ambaye ni msouth afrika bwana Senzo Mbatha. Kwa utaratibu wa kiuweledi yeye ndiye anayehusika na masuala ya usajili wa aina ya mchezaji kutokana na ripoti ya mwalimu aliyo iacha.

Baada ya BM kusajiliwa Jana, jamaa akashtuka. Maana ulikuwa usajili ambao wala haukuwa kwenye mapendekezo ya mwalimu. Senzo ikabidi amvutie waya Bwana Mo, Boss akamwambia yeye alitaarifiwa na baadhji ya viongozi kuhusu kuhitajika kwa pesa kwa ajili ya mchezaji fulani na yeye akaidhinisha.

Senzo akaamua kuthibitisha kwa Mwalimu mkuu ikiwa kama yeye pia alichangia usajili huo ambao yeye mhusika hakihusishwa hata kwa asilimia 1. Mwalimu akasema ahusiki kwakuwa yeye alikwisha acha repoti ya wachezaji wanao hitajika.

Mtendaji Mkuu huyo akaamua kuachia ngazi klabuni hapo kwa madai ya kuwa anaingiliwa kwenye majukumu yake kwa kulazimishwa kuenenda na tamaduni ya usajili wa klabu hiyo. Pia hofu ya kutiwa doa kwa CV yake na sifa yake kiujumla kumempelekea kuachia ngazi.

Ca.PNG
SENZO.jpg
 
Senzo is a professional, hawezi kuvumilia uswahili uliofanywa jana na wakina Manara, Safi sana. [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] Mashabiki tumechukizwa na CEO alichukizwa

Kama Morisson hakuwa kwenye mipango ya kocha
, sitashangaa naye kocha akisepa
 
Nakumbuka nilisema juzi humu kuwa kuna pahala Simba SC wanakosea. Huwezi kuifanya klabu iendeshwe kwa weledi na wakati huo huo unaiendesha kwa Uhuni wa kizamani.

Nilikuwepo na Social Media Content Manager pande fulani usiku wa Jana. Jamaa akanimwagia mchele chini ya kwamba sakata la BM kusaini Simba SC litaondoka na mtu, Sikumuelewa.

Mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya yalioachwa na kocha Kishingo alikuwa nayo mtendaji mkuu wa klabu ambaye ni msouth afrika bwana Senzo Mbatha. Kwa utaratibu wa kiuweledi yeye ndiye anayehusika na masuala ya usajili wa aina ya mchezaji kutokana na ripoti ya mwalimu aliyo iacha.

Baada ya BM kusajiliwa Jana, jamaa akashtuka. Maana ulikuwa usajili ambao wala haukuwa kwenye mapendekezo ya mwalimu. Senzo ikabidi amvutie waya Bwana Mo, Boss akamwambia yeye alitaarifiwa na baadhji ya viongozi kuhusu kuhitajika kwa pesa kwa ajili ya mchezaji fulani na yeye akaidhinisha.

Senzo akaamua kuthibitisha kwa Mwalimu mkuu ikiwa kama yeye pia alichangia usajili huo ambao yeye mhusika hakihusishwa hata kwa asilimia 1. Mwalimu akasema ahusiki kwakuwa yeye alikwisha acha repoti ya wachezaji wanao hitajika.

Mtendaji Mkuu huyo akaamua kuachia ngazi klabuni hapo kwa madai ya kuwa anaingiliwa kwenye majukumu yake kwa kulazimishwa kuenenda na tamaduni ya usajili wa klabu hiyo. Pia hofu ya kutiwa doa kwa CV yake na sifa yake kiujumla kumempelekea kuachia ngazi.

View attachment 1532173View attachment 1532199
Daaaaaah we jamaa unajua kutengeneza nadharia ambazo hazina uhalisia? Ulivyoripoti utafikiri ndo alivyosema Senzo kwenye tweet yake,
Kuna siku hizi nadharia mtakuja kuzikataa muda ukifika
 
Hizo ndiyo Fitina za kiswahili. Unajiuliza Huyu Senzo anatula pesa mingi lakini mkataba unagomba huwezi kumwacha kienyeji kwahiyo unamtafutia zengwe ili ajitoe mwenyewe. Picha limeisha
 
Wewe Jamaa unatatizo la mtindio wa Ubongo.

Yaani MO ashindwe kumlipa jamaa 12,930 USD monthly salary huyu jamaa?
 
Simba wamechemka sana. Kweli mswahili haachi asili, pamoja na kumsajili BM wapenzi wengi wa Simba hawajafurahishwa nao.

Manara kaingilia jukumu la Senzo.

Jamaa wako na uweledi wa hali ya juu. akaona isiwe tabu ngoja aachie ngazi.

Si unajua kuwa MO hana sauti kivile inapokuja ku-inforce proffesionalism klabuni.
 
Kama ndivyo basi walipoteza fedha kumwakiri Senzo. Waendelee kuendesha timu kienyeji.
 
Kiukweli Kuondoka kwa Senzo ni pigo kubwa jamaa angeweza kutusaidia kupata wachezaji wazuri na mipango mizuri benard Morison hakuwa anahitajika msimbazi ni kama tulivyomsajili Ajibu tukamwacha Okwi kwa madai anataka pesa nyingi ukiangalia mchango wa Ajibu ni sifuri ulikuwa usajili wa kukomoa zaidi wachezaji aina ya Morison simba wako wengi tunahitaji beki wa maana kati , beki wa kumsaidia Kapombe na mshambuliaji wa kati ila ujuaji mwingi haya ndio matokeo yake
 
Mimi nilishtuka baada ya Kuona bernard Morrison anasaini mkataba lakini haonekani yupo na viongozi gani aliombatana nao.lakini mchana nilimuona akipiga misele na hajji nikasema hapa kuna kitu. Washamzunguka MO hela imepigwa hapa TAKUKURU fuatilieni.
 
Huyu Manara anaposajili, lengo lake si kuisaidia Simba ila kuidhoofisha Yanga.
Simba wanafanya makosa mengi katika Usajili kwa kurundika wachezaji wengi wazuri ambao hawatumiki.
Viwango vya wachezaji hawa ambao hawatumiki vinashuka na hata kama walikuwa wanaitwa Timu ya Taifa, hawaitwi tena.
Gadiel Maiko, Ajibu, na wengine wengi wako wapi sasa?
Manara anasumbuliwa na mihemko ya kitoto.
 
Alafu mtu anakwambia Tanzania hakuna fursa, hii nchi ni shamba la bibi wageni wanakuja kujichumia rasilimali wanasepa zao
 
Mimi nilishtuka baada ya Kuona bernard Morrison anasaini mkataba lakini haonekani yupo na viongozi gani aliombatana nao.lakini mchana nilimuona akipiga misele na hajji nikasema hapa kuna kitu. Washamzunguka MO hela imepigwa hapa TAKUKURU fuatilieni.
Jamaa anataka kuzinduka ila Manara anampiga kipapai
2.jpg
 
Back
Top Bottom