Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kutokana na Mvutano uliopo kati ya Serikali, Watoa Huduma na Wananchi kuhusu Bundles na Shutuma za Wizi inabidi sisi wananchi tuelewe tunataka nini na Wizi ni nini?
Issue za Wizi:
Kama kuna issue za Wizi na mtu kaibiwa kuna vyombo vya kisheria na TCRA inabidi mwananchi aweze kupeleka issue zake huko ili asaidiwe, na hapa wizi ni kuuziwa tofauti na makubaliano yaani unanunua mb 10 unapewa mbili na sio gharama ya bei
SULUHISHO
A: Serikali ikae Kando
Mbaya katika haya mambo mara zote ni Serikali kuingilia haya mambo na mara nyingine gharama inatokana na Tozo / Au Sheria za Serikali, Wote tunakumbuka SKYPE ilivyokuja nchi kama Tanzania ilikuwa inazuiliwa eti TTCL itakosa mapato..., Juzi Juzi tunakumbuka Serikali iliipa Mitandao Bei elekezi na kilichotokea mitandao yote ikacheza kwenye zile Bei Elekezi!!! (ALAS!! kumbe Bando zilikuwa bei rahisi kuliko Bei Elekezi hivyo Bei zikapanda na Mitandao yote Bei zikawa sawa zote Juu); Kumbe Ushindani ulipelekea kila kampuni kushusha to the minimum sasa kuwekewa bei elekezi wote wakawa na bei sawa...
Kumbuka pia huyu Mtetezi mwisho wa siku anatetea Mapato yake na sio necessarily bei rahisi kwa mtumiaji (Refer Matamko ya Naibu Spika akimwambia Waziri akaangalie ni vipi wanaweza kupata fedha zaidi kutoka kwenye Data)
Au Kuna waziri alishasikika wacheki ni vipi wanaweza kupata pesa kwenye mitandao kama Whats-app
Kuwepo kwa bei elekezi huenda kweli bei ikashuka lakini vipi kuhusu quality ? Sababu kama wote bei zitakuwa sawa na huwezi kuwavuta wateja kwa bei huenda quality ikawa minimum na uwekezaji ukashuka... AFTER ALL UBINAFSHAJI TULIFANYA ILI ULETE USHINDANI sasa tukipangiana Bei kwa Sheria Ushindani utapotea... Kwahio ushauri wangu Hii Mitandao Binafsi iachwe hata ikitaka kuuza Bundle kwa Laki moja ifanye hivyo Tigo wakipandisha watu watahamia Halotel na Voda..., Ingawa kuna uwezekano wa Cartels hii Mitandao kukaa pamoja na kupanga Bei nadhani Suluhisho la kuzuia hilo ni Hapo Chini B:
B: Ili Kuepusha Cartels na Bei kupanda sana Juu Serikali Iwekeze / Maintain Quality ya Mashirika yake TTCL na Airtel (ambapo wana Share nyingi)
Huwezi kumpangia mtu bei wakati hujui uwekezaji wake upo vipi, ni kweli huenda leo napata faida kubwa ila ninawekeza kwenye Research and Development kwa ajili ya Kesho ya Promotion ili kuwafahamisha wadau kwamba bei zangu ni ndogo kuliko za jirani.
Sababu ni ushindani na ushindani ndio determinant na kuepusha upangaji wa bei Serikali na kama Serikali inaona bei fulani ndio halisi kwa mwananchi kuchajiwa basi ihakikishe hizo bei na hizo Quality zinatolewa na mashirika yake ambayo ni TTCL na AIRTEL, yaani hizi Kampuni mbili ndio pace setters, Bei ndogo na Quality ya Juu hivyo basi hizo nyingine zitakuwa hazina jinsi ili kupata wateja ni either kushusha kama TTCL au zaidi ya TTCL
C: Serikali iangalie manufaa yanayotokana na Outcomes za Cheap Bundles na Sio Kutaka kupata Pesa Directly
Juzi tu hapa tumepata mkopo wa TEHAMA na kila siku tunaimba ngonjera za vijana kujitafutia ajira na kuongeza uvumbuzi..., Kwahio kama kweli tunataka kuleta / kuhimiza ukuaji wa TEHAMA tuanzie kwenye kufanya Bundle kuwa as Cheap as Possible..., na hilo linaweza kufanyika kwa Serikali kupunguza kuchota kwenye Data na sio Kuongeza Uchotaji..., Kuliko kuomba misaada ya sijui kuwekeza kwenye majengo ya TEHAMA tunaweza kuwekeza kwenye kutokuchaji TOZO nyingi kwenye DATA hivyo vijana wanaweza wakajifunza wenyewe kwenye mitandao (Karne hii Information zipo Widely available and for Free)
D: Tuache Siasa na Cheap Politics
Badala ya kuwekeza sijui kwenye TUME / SHERIA na Wadau (tunaowalipa kwa gharama) kukaa vikao vya kila mara ili waonekane kwamba wanawatetea wananchi lakini ukweli ni kwamba tunaongeza gharama za kuwalipa watu na hii mitandao tunaiongezea gharama za kuajiri wanasheria na consultancy firms kuona ni vipi wanaweza wakafanya lobbying ili bei ifike ile wanayotaka - Kwahio kwenye hizi Siasa ni kwamba tunawapatia ulaji wachache...
C: Wananchi tuelewe tunataka Kupata nini na Wizi ni Nini
Wananchi inabidi tuelewe tunataka nini ? Kupangiana Bei au Soko Huria ? Na wizi ni nini ? : Sababu wizi ni kufanya / kwenda tofauti na makubaliano, sasa kama inabidi usome vigezo na masharti na ushaambiwa kwamba hili bundle linakwisha masaa 24 basi ukiona hutaki unataka likae mwaka basi ongea na Kampuni wape proposal ya ma-bundle ya mwaka wakiona kuna wateja watafanya hivyo na huenda ukalipwa kwa mawazo yako mazuri...
Sababu ukinganganiza Bundle la Masaa 24 sijui likae wiki huenda Kampuni limeweka hilo bundle wakijua kwamba Jtatu watumiaji ni wachache hivyo tushushe bei ili watumie wengi zaidi ila likikaa wiki alafu jmosi ambapo watumiaji ni wengi huenda capacity ikajaa na hata wale wanaotulipa 1000/= wasipate the required quality
Hivyo wananchi tutumie Power yetu ya Choice Kampuni A ikizingua tuhamie Kampuni B na Kampuni zote zikipanga zituibie tuna Kampuni yetu ya TTCL tuibane Serikali iweze kuifanya hii Kampuni iwe mfano ili wengine waige..., na hizo suggestions zetu tuzipeleke huko TTCL ambapo atleast sisi ni wamiliki na sio Hizo Kampuni Binafsi ambazo hatukuzisaidie kuwekeza leo tuwapangie vya kufanya....