jrharakati
Member
- Jul 13, 2015
- 37
- 1
wasanii na watangazaji waiingilia kati kuhimiza serikali iweze kuwasaidia wanafunzi hao matatizo yao yatatuliwe ijiwepo lile la kuhamishwa kupelekwa vyuo vingine
Nimeipata hii kwa mdau ambaye hakupenda jina lake litajwe. Wanafunzi, kuweni makini!
Salamu brother hop ur gud!
Kaka nakuandikia nikiwa na imani kubwa kwako wewe kama mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa wanafunzi wa Kitanzania.
Mimi ni kijana ninae soma Kampala Int University iliopo Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Kitengo cha Afya ya Binanadamu (am a medical student).
Kaka naomba uwasihi wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wachaguapo vyuo waangalie the following facts such as, je chuo kimesajiliwa na bodi husika mfano kinatambulika na bodi ya maabara kama unataka kusomea maabara je chuo kimesajiliwa na baraza la wafamasia kama unataka kusomea ufamasia na je chuo kimesajiliwa na body ya madaktari kama unataka kusomea udaktar!
Nina andika nikiwa na uchungu mkubwa sana n ninaumia kwan future yangu haieleweki. 2013 Tanzania Government kupitia TCU imetupeleka kuchukua DEGREE za afya chuo cha KAMPALA INT UNIV sasa tupo mwaka wa pili na sisi ndo wa kwanza kupelekwa na serikali pale.
Baada ya wanafunzi wa certificate kumaliza na kwenda kuomba lessen yakufanyia kazi kwenye mabaraza yanayosimamia afya Tanzania, mabaraza yakawakataa wakisema chuo hakijasajiliwa.
Ndipo wakaja chuo na kutuambia kuwa wamenyimwa vibali vya kufanyia kazi kwa hiyo fuatilien swala hili kabla ya hamajahitimu. Kufiatilia ni kwel chuo hakijasajiliwa na mabaraza husika, tumeenda office zote za serikali, Bungeni, Wizara zote mbili Afya na Elimu na hawajatoa majibu, sasa twende wapi?
Mgomo chuoni umedumu kwa miezi mitano sasa bila mafanikio.
Naomba uwasihi wanafunzi wanapochagua vyuo waangalie endapo chuo kimesajiliwa na mamlaka husika, wasije kurudia kosa tulilofanya wenzao.
Chanzo: Allan Lucky || Facebook
![]()