ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Kitendo cha kinyama kilichofanywa na mwalimu/meneja wa shule ya Green City la kumpiga mwanafunzi hadi kupoteza fahamu kwa masaa karibu 20 eti kisa kachelewa masaa machache kuripoti shule Jumapili ni kitendo kinachopaswa kulaaniwa na serikali inabidi ifanye uchunguzi wa shule nyingine zenye tabia za namna hiyo.
Wazazi tujitokeze na kuzianika shule za namna hii zenye adhabu zinazopitiliza ili wajirekebishe au serikali izimulike.
Korogwe girls inasemekana adhabu zilizopitiliza pale napo zimekithiri, wanafunzi wanalimishwa, wanachimbishwa mashimo makubwa kama adhabu, hali inayopelekea hata ufanisi wa watoto kushuka shule sasa inathamini hizo kazi/adhabu, shule ina maekari ya mashamba yanayotegemewa kulimwa na wanafunzi wenyewe kwa kigezo cha adhabu.
Nimeridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya mkoa wa morogoro kumsimamisha kazi meneja wa shule na kumkabidhi kwa jeshi la polisi.
Jamani shule zenye tabia hizi tuziseme hapa serikali ifuatilie, watoto wetu wanateseka.