Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Nafikiri sasa tubadilishe jina, BADALA YA KUITA WALA RUSHWA TUITE WAFAKAMIAJI RUSHWA. EL hajatajwa anashtuka then anasema issue ya zamani, zamani? hata kama ni miaka 10 ataijibu

Wamezoea kupitishia mambo yao PCCB ili itudanganye waTZ, sasa ukweli umejulikana b'se PPRA are professional people.

Wafakamiaji Rushwa wataitumbukiza nchi kwenye Vita.
 
tutafute basi hii ripoti iliwatu wajue kulikoni,au itahatarisha amani na utulivu wa nchi
 
tutafute basi hii ripoti iliwatu wajue kulikoni,au itahatarisha amani na utulivu wa nchi

wewe katibu tarafa.... huiogopi serikali... utashikwa na usalama wa Taifa (just kiddin -- natania tu)..

Hii report iko hapa ndani tayari na watu wanajichukulia. Kumbuka kuwa una masaa chini ya sitini kabla haijatoweka kwa hiyo ichukue haraka sana uwezavyo!

angalia kitu ina neno ASAP hapa kwenye forum ya siasa..
 
na kweli now tuna wafakamiaji wa rushwa na ni walafi haoo hawashibi..jamani mie mbona niliwahi sikia kuwa hiyo richmond kwa upande wa Tz..ni ya mtoto wa EL????au ndo yale yale ya "Mali hizi siyo zangu bali za mke wangu au za mtoto wangu wa kwanza??"
 
Ukitaka kujua kuwa huyu EL yumo ama anajua kwa uhakika ni nani mhusika msikilize hapa alipodai kuwashushua gazeti la Thisday!
The PMO statement also censured THISDAY for 'reviving' the issue of corruption allegations related to the Richmond deal even after the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has already declared it to have been clean and devoid of corruption, after conducting its own investigation in the face of a public outcry.

Jibu lake:-
The PCCB declaration was made last May - three months before the PPRA report was prepared (August 2007).

Kwa nini hawa viongozi wetu hutafuta majibu ya kupingana badala ya kutafuta Ukweli wa madai!
 
kama anasema hakuhusika then hakuhusika, basi semeni nyie mliohusika !
 
KadaMpinzani,
EL ni kiongozi wetu mwenye madaraka makubwa sana. Akisema yeye hahusiki inatakiwa awaeleze wananchi akina nani wamehusika ama ni hatua gani atazichukua kuhakikisha anawapata wahusika...
Ebu soma vizuri maelezo yake utagundua tunachosema hapa. EL anachofanya hapa ni kufunika kombe kawa mwanaharamu apite!
Ikiwa yeye anadai hahusiki na mkataba wa Richmond it means mabaya yote yaliyotokea ktk mkataba huo hahusiki!. na ndio maana kajifuta vumbi yeye wakati ni kazi yake yeye kama waziri mkuu kutufahamisha sisi kipi ktaendelea baada ya uchunguzi wa PPRA kudhihirisha kwamba kulikuwepo mkono na kiongozi toka ngazi za juu.
Ni jibu gani wewe umelipata toka kwa waziri mkuu?... Je, unapodai tuseme sisi tuliohusika una maana gani haswa?.. nashindwa kukuelewa ama ndio ktk kulinda maslahi binafsi.
 
did anybody check in na waziri husika wa hiyo wizara responsible kwa ajili ya umeme, akibanwa huyo nadhani atawataja wenzake wote !
 
Hivi anaposema hakuhusika ana maana gani, wakati sote tunajua kuwa ni alihusika, let me refresh his memory:

Source:: Daily News
Story by: CHARLES KIZIGHA
Date: 20.10.2006


THE Prime Minister, Mr Edward Lowassa, held a meeting with the power sector top brass led by the Minister for Energy and Minerals, Mr Nizar Karamagi, in Dar es Salaam yesterday to critically review the power crisis and chart out strategies to alleviate the problem at the earliest time possible.

The country is facing a serious power shortage caused by lack of rainfall which has reduced electricity generation at the hydro plants from their installed capacity of 650 mw to an average of about 200 mw and intermittent breakdown of Songas gas turbines with a total capacity of 181 mw.

A senior government official told the 'Daily News' yesterday that the meeting was necessary as the situation was expected to worsen following the shut down of Mtera Dam and possibly Kidatu power station any time from today.

The meeting reviewed all strategies drawn by the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) to counter the power crisis, which included the leasing of gas turbines from Aggreko International Power Projects of the United Arab Emirates (UAE), the US-based Richmond Development Corporation (RDC) and the one to be bought from Warstila.

Tanesco presented at the meeting names of some foreign companies that submitted proposals to import gas and diesel engines and evaluated them, he said.

The official, who declined further comment, said that the recommendations from yesterday's meeting would be submitted to higher authorities for a decision likely to be made at the earliest possible time in view of the prevailing power crisis.

Sources within Tanesco explained that hydro plants production dropped from 647 mw to almost 200 mw. The following are the capacities of the plants with current generation in brackets: Kidatu 200 mw (average of 24 mw), Mtera 80 (zero), Kihansi 180 mw (closed during the day and switched on at night giving between 100 and 150 mw).

The New Pangani Falls 68 mw (50 mw), Hale 21mw (5mw) and Nyumba ya Mungu Dam eight mw (two mw).

A 20-mw gas turbine installed by Aggreko at Ubungo power station is now on line and components of the second 20-mw generator, which were to start arriving yesterday from Sharjah, UAE, are expected in Dar es Salaam today.

Efforts to reach the Country Manager of RDC, Mr Naeem Gire, to comment on latest development on the 20-mw gas turbine that he said was in North Caroline were futile.

Na Mwandishi Wetu, Gazeti la Mwananchi

WAKATI Bunge linaanza mkutano wake wa tano leo, serikali imewaangukia wabunge wa CCM katika harakati za kujaribu kuwafumba midomo ili kufifisha makali ya mjadala wa hali ya umeme unaobashiriwa kwamba utaibuliwa bungeni.

Harakati hizo za serikali zilijibainisha juzi (Jumapili) wakati wa kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Serikali ililazimika kuwaweka sawa wabunge wa CCM kufuatia hisia kuwa suala la hali ya umeme na uhalali wa kampuni ya Richmond Development Corporation (RDC) kupewa zabuni na serikali, linaweza kuibuka ndani ya mkutano unaoanza leo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zimesema, wabunge wa CCM mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kuchuja majina 36 ya wana-CCM wanaogombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, waliihoji serikali juu ya wingu zito linalotanda dhidi ya hali ya umeme nchini hususan uhalali wa kampuni ya RDC kupewa zabuni ya kuleta majenereta ya dharura.

Wabunge hao waliitaka serikali iwaeleze kinagaubaga juu ya mazingira ya Richmond kupewa mkataba huo na kufafanua juu ya tuhuma kuwa kampuni hiyo inayodai kuwa imesajiliwa Marekani, haitambuliki huko.

Akijibu hoja za wabunge, chanzo cha habari kimesema, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alikwepa kuzungumzia hoja ya Richmond moja kwa moja akidai kuwa yeye ndiyo kwanza ameingia wizarani hapo na hakuwapo wakati mikataba ya kampuni hiyo ikisainiwa.

Waziri Karamagi anadaiwa kusema kuwa mara baada ya kuingia wizarani alianza kushughulika hali ya umeme ili kuhakikisha inatengemaa walau ifikapo Desemba upatikanaji wa nishati hiyo urejee katika hali ya kawaida. Hata hivyo, Waziri Karamagi aliwaambia wabunge hao kuwa pamoja na malalamiko yanayoihusu Richmond, kama serikali itavunja mkataba nao, italazimika kubeba hasara kubwa kwa kuwa italazimika kulipa fidia kubwa kwa Richmond.

Alisema kwa sasa Richmond bado haijavunja mkataba na wanaendelea na utekelezaji kwa mujibu wa makubaliano. Hata hivyo, majibu hayo ya Karamagi yanaelezwa kuwa hayakuwaridhisha wabunge hao wa CCM ambao walitaka kuelezwa bayana juu ya uhalali wa kampuni ya Richmond kupewa zabuni hiyo na serikali.

Kufuatia maswali hayo, Waziri Mkuu Lowassa ilibidi aingilie kati na kumsadia Karamagi na kuwaeleza wabunge kuwa Serikali ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mwenyewe, inalifuatilia kwa karibu suala la umeme nchini. "Lowasa alisema suala la umeme linamsononesha sana Rais na analifuatilia kwa karibu na kwamba kuna siku Rais aliwahi kumpigia simu saa saba za usiku kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo na waliongea kwa saa nzima," alisema mbunge mmoja wa CCM aliyehudhuria kikao hicho cha juzi.

Inadaiwa kuwa katika ufafanuzi wake, Lowassa aliwaomba wabunge wa CCM kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kutafuta suluhisho la kudumu la hali ya umeme, kauli ambayo inatafsiriwa kuwa ni kuwanyamazisha wabunge hao kuzungumzia hoja hiyo kwa kishindo ndani ya Bunge.

"Serikali ilisema inajua kuwa wapinzani wataibua hoja hiyo ndani ya kikao cha Bunge, na hivyo ni muhimu kwa wana CCM kuielewa serikali katika jambo hilo na kuiunga mkono," kilisema chanzo kingine cha habari. Tangu serikali iingie mkataba na kampuni IPTL mwaka 1995 kwa ajili ya kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco, kumekuwako na malalamiko mengi juu ya mikataba ya nishati.

Tangu wakati huo, serikali imekuwa ikiahidi kuwa itakuwa makini, lakini tangu kuanza kwa mgawo mkali wa umeme nchini ambao umesababishwa na ukame na hivyo mitambo ya kufua umeme wa maji kushindwa kufanya kazi kutokana na kupungua kwa maji, juhudi kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuingia mkataba wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.

Miongoni mwa kampuni zilizioingia mkataba na serikali katika siku za hivi karibuni kabisa ni ya Aggreko ambayo tayari imekwisha kuanza kuzalisha megawati 20 za umeme takribani wiki mbili zilizopita huku kampuni nyingine iliyoingia mkataba huo ni Richmond na ilitakiwa iwe imekwisha kuanza kuazalisha umeme huo sasa.

Kutokana na sababu mbalimbali Richmond ndiyo kwanza awamu ya pili ya mitambo yake ya kuzalisha umeme huo iliwasili juzi jijini, baada ya kwanza kuwasili wiki moja iliyopita.

Kabla ya kuwasili kwa mitambo ya Richmond, kumekuwapo na taarifa za kutatanisha kuhusu uwezo wa kampuni hiyo, uhalali wake wa kupewa kazi hiyo na kama ni kweli kwamba kampuni hiyo ina makazi yake nchini Marekani.

Kuna habari pia kwamba kuhamishwa kwa mawaziri wote wa Nishati na Madini katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais hivi karibuni, kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na jinsi suala la umeme lilivyoendeshwa katika mchakato mzima wa kupatikana kwa kampuni za kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi.
 
Kama hakuhusika ilikuwaje afanye kazi ya ziada ya kuzima hoja ya kujadiliwa Richmond kwenye vikao vya Bunge? Hilo pekee linamfanya ashukiwe kwamba ni mmoja wa wahusika wakuu kwenye hilo dili. Kwa hiyo wenye akili timamu wanaelewa nini kinachoendelea na wale walio kwenye kundi la kutetea maslahi ya EL wanajua fika kwamba kuna nini huko ndani.

EL sasa hivi anatapatapa kwa kuwa amekosa tawi la kushika na ndiyo maana anaishia kutumia sheria ya PCCB ili kuwanyamazisha ThisDay wasiendelee kumwaga sumu zaidi. Kama yuko clean kwenye hilo dili na kwa kuwa hakutajwa na gazeti husika, alitakiwa akae kimya! Kitendo cha kuanza kusema sema ovyo ovyo ndiyo kinazidi kumpaka matope zaidi na sisi hatuwezi kukaa kimya tu, lazima tutasoma hizo news plus PPRA Audit Report ya Tanesco kwa makini zaidi.
 
did anybody check in na waziri husika wa hiyo wizara responsible kwa ajili ya umeme, akibanwa huyo nadhani atawataja wenzake wote !

Swala siyo kumbana waziri husika, swala ni kwamba je akina EL walikuwa tayari waziri husika aseme kila kitu kuhusu hilo dili? Kumbuka kuna barua ilivujishwa kwenye vyombo vya habari ikitoka kwa EL kwenda kwa Dr. Msabaha (wakati huo akiwa waziri wa Nishati na Madini), barua ile ilileta kadhia kubwa Bungeni ambapo kamati ya Bunge ilihoji uhalali wa barua za siri za serikali kuchapishwa kwenye magazeti wakati Kamati ya Bunge ilikuwa imenyimwa kuona Mkataba wa Richmond, "eti" kwa kuwa ni siri!

Dr. Msabaha aliondoka (aliondolewa) wizara ya Nishati na Madini baada ya kadhia ya Richmond ... ni kwanini 'aliondolewa'? Tutaaminije kwamba kuna mkubwa fulani alikuwa analindwa ili jamaa asije akamwaga sumu? Tuna macho na tunaona, tuna akili na tuna uwezo wa kutambua pia! EL hana ubavu wa kuikwepa Richmond na ndiyo maana swala hilo likianza kuongelewa jamaa huwa anakosa usingizi. Mbona tangu atajwe kwenye orodha ya mafisadi hatujamsikia akijitetea, imekuwaje leo hii aguswe na mzoga wa Richmond ambao yeye anasema ni swala lililozikwa?
 
Je, ni kwanini aliwakataza Wabunge wa CCM kuhoji kuhusu mkataba wa Richmond?

Yeye akiwa kama Kiongozi wa baraza la mawaziri, kama yeye hakuhusika atutajie ni nani alihusika na alipata wapi ruhusa ya kuingia mkataba huo bomu?
 
Government pays out 19.5bn/- to Dowans

-Despite delays in commencement of power supply

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE government has already paid almost 20bn/- to the company that inherited the controversial Richmond power generation project despite actual power supply being delayed by almost a whole year, THISDAY can now reveal.

According to our latest findings, Dowans Holdings S.A of the United Arab Emirates, which took over the project last December after the initial agreement with the US-registered Richmond Development Company went awry, has so far received a total of $15m (approx. 19.5bn/-) from the government.

The ’advance’ pay-out was made even as the UAE firm fell a staggering 243 days behind schedule in its pledge to start supplying the agreed 100 megawatts of thermal plant electricity to the national grid run by the Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO).

This delay has led to Dowans now owing the government an accumulated fine of $2,430,000 (over 3bn/-), calculated from a $10,000 (approx. 13m/-) daily penalty imposed from February 2 this year - when the company was supposed to start delivering - to October 3 which was when they actually did start delivering.

The state-run Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) confirms in its latest report on TANESCO that the government has already forked out $15m to Dowans, but at the same time has raised concern about how it (government) will be able to recover the 3bn/- in accumulated fine arrears from the same company.

According to the PPRA report, the earlier contract between Richmond Development Company and TANESCO, signed on June 23 last year, did not provide for re-assignment of the agreement to Dowans.

’’There is no agreement between the parties (in the original contract) as to how the amount would be claimed from Dowans Holdings,’’ the report notes.

As already reported exclusively by THISDAY, the same report by the government’s procurement watchdog has underscored what it describes as ’political influence’ and ’clear interference’ by unnamed ’higher authorities’ in TANESCO’S tender process for the contract, resulting in Richmond emerging bid winners.

According to the PPRA findings, the TANESCO evaluation process had initially identified two other bidders out of the short-listed eight - Renco SPA of Italy and Real Energy of the UK - more relatively more ’responsive’ to the bid requirements than Richmond Development Company.

However, the process was later taken over by the Ministry of Energy and Minerals, which recalled the bid documents submitted by all eight bidders from TANESCO and processed them itself, eventually coming up with Richmond.

TANESCO was then ’ordered’ to sign the contract despite the power utility company’s initial rejection of Richmond and overall resistance ’’especially after the process that brought the winner was handled outside TANESCO’s procurement process.’’

It is further asserted that the contract was ’’signed in strange circumstances, at night and at the ministry, with some contractual issues protecting the client having been ignored as there was no room for TANESCO to review the draft contract and the company secretary does (did) not know who drafted the contract.’’

As part of its own recommendations after assessing the entire Richmond affair, the PPRA made a note to advise the central government through TANESCO’s parent ministry ’’to understand its limits in involvement in procurement process, to reduce persistent interference in the procurement affairs of TANESCO.’’

The latest serious concerns raised by the PPRA report on irregularities in the Richmond deal have come to light several months after the state-run Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) made a surprise announcement last May that its own investigations had found the deal to be clean.
 
Government pays out 19.5bn/- to Dowans


Pesa za walipa kodi hazina mwenyewe na hapo hapo hawakuweza kutimiza malengo na hakuna mkataba wa wao kulipa pesa za uchelewaji.

1. Hii ilikuwa emergency sasa kwa nini hawa punguani bado wapo na wameshindwa hata kuleta umeme wowote kwa wakati muafaka?

2. Je, serikali inalipa hiyo pesa kwa misingi ipi?

3. Huu mkataba ambao wameshindwa kutekeleza lazima uangaliwe na Kamati ya Bunge na Richimondulian inabidi aambiwe wazi hii sio kazi yake kuwazuia wabunge kufanya kazi yao.
 




Nimeona kwenye habari za magazeti kwamba mkataba wa Richmond nao umevuja. Kama kuna yeyote ambaye anaweza kutuwekea hapa tutashukuru ili tuuchambue kama karanga kipengere kwa kipengere.

Nadhani mwelekeo sasa ni mzuri, kama tutaendelea hivi basi mengi yatajulikana!
 
Inakoelekea ni kwamba mawaziri watakwenda na mikataba majumbani, na wakifika huko wake zao wataiiba na kutuwekea hapa JF.
 
keil.. tulia..mtawekewa wimbo baada ya kukamilisha mambo fulani. Nyumbani tunawaaonjesha tu kwanza.. vinapikwa hapa...
 
kwi kwi kwi ... ina maana upinzani uko mpaka kwenye ngazi ya familia? je, mikataba hiyo ihifadhiwe wapi ili isiendelee kuvuja? kwanini uvujaji wa nyaraka hizo umeongezeka? I think there is something wrong somewhere ingawa bado sijaweza kujua exactly tatizo liko wapi?

Hii ni signal mbaya kwa JK na wana mtandao wenzake, people within the system are not happy with madudu yanayofanywa na wana mtandao na sasa silaha iliyobaki ni kuumbuana na kuanika siri za ndani ili wananchi wajue uozo unaoendelea. Ngoja tuendelee kusubiri skendo nyingine ambazo zitawaangusha wana mtandao.

Dhambi ya wana mtandao itawamaliza wao wenyewe, kama walijua kwamba wame-win basi nadhani bado wana safari ndefu zaidi. Kama walitarajia kwamba wakichukua dola watakula sana basi naona wameingia kipindi kibaya au majeruhi wa mchakato wa kusaka mgombea wa urais wanaendelea kula nao sambamba ili waone mwisho wao ni wapi. Ukijua hili wenzako wanajua lile!!!!!
 
keil.. tulia..mtawekewa wimbo baada ya kukamilisha mambo fulani. Nyumbani tunawaaonjesha tu kwanza.. vinapikwa hapa...

fanya hima kidogo niupate kabla hata Kaimu Rais hajarudi,EL anakutafuta sana coz kuna mtu wa PMO kaniambia anataka kujua unafananaje?
 
msiwe na haraka.. ila kama hamchezi mbali mnawaze kujikuta mnaburudishwa na kibao murua ndani ya siku chache zijazo.. kwa sababu tatizo kubwa ni kuhakikisha vitu hivyo viko salama na haviwi counterfeited... so naomba msipush tuharakishe.. kwani wajanja wao wanaweza wakatoa "mkataba wao".. halafu mkachanganyikiwa.. Naomba hili niliache hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…