Sakata la Kibu Denis na Simba linanifikirisha, kwanini mchezaji anajiamini kiasi hiki?

Sakata la Kibu Denis na Simba linanifikirisha, kwanini mchezaji anajiamini kiasi hiki?

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Ninapata mashaka sana kwenye hiki kinachofanywa na KIBU DENIS, kwanini ANAJIAMINI sana na kufanya mambo ya ajabu namna hii? Mchezaji umesaini mkataba mpya ata mwezi aujaisha alafu unagoma makusudi kujiunga na Kambi ya timu yako na unajua kabisa Sheria zinazoongoza mpira duniani zilivyo unapataje ujasiri huu?
Licha ya meneja wake kusema kibu awadai Simba chochote ninaanza kupata mashaka juu ya mkataba mpya wa Simba na KIBU Kama ni kweli walitimiza matakwa yote ya kimkataba, viongozi wa Simba wamekuwa na uswahili mwingi na propaganda nyingi ndio maana tunaona Wana kesi za wachezaji 3 pale TFF wakilalamikiwa kutozingatia matakwa ya usajili wao!

Inawezekana kabisa hata suala la Kibu Kuna jambo linafichwq nyuma ya pazia, aiwezekani mchezaji awe na ujasiri wa kufanya icho anachokifanya tena kwa kujiamini namna iyo, wanasema ameipata timu Norway je ataendaje kucheza bila baraka za timu inayommiliki? Kibu yeye ajui icho kitu?

Jambo hili la Kibu Lina ukakasi Tena mkubwa!
 
Taarifa zilizopo, wamempa million 50 ambazo alikuwa akizidai kwenye mkataba uliopita. Mkataba mpya wakawa hawajaweka hata senti ndio maana kakaa kimyaa.
 
Aliitwa Timu ya Taifa akiwa huko Marekani, Alikubali? Kiburi kilianzia hapo?
 
Na viongozi wa Simba tunaomba mtulie kimyaaa.
Wala msimtafute
 
Back
Top Bottom