Sakata la kufungiwa Pius Buswita, maswali yenye kuhitaji majibu

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Chama cha mpira wa miguu Tanzania TFF kimemfungia Mchezaji Pius Buswita kwa kosa la kusajili timu mbili za Yanga na Simba.

Ambako kwa sheria za TFF mchezaji atakayekutwa na kosa hilo atafungiwa mwaka mmoja.

Kuna maswali yanahitaji majibu.

1- Je mchezaji huyo alisaini fomu za usajili za Klabu ya Yanga na Simba ambazo zimetoka TFF?

2- Katika orodha ya wachezaji wa Yanga iliyopelekwa TFF jina la Pius Buswita lipo, Mbona orodha ya wachezaji wa Simba iliyopelekwa TFF halipo(Kama kweli amesajili simba)?

3- Kwanini Simba hawakuweka jina lake kama mmoja wa wachezaji waliomsajili?

5- Kwa nini TFF wamfungie mchezaji aliyesajili timu moja, kwa kosa la kusajili timu mbili?

6- Je TFF wana ushahidi gani au wametumia upi, kwamba mchezaji huyo amesajili timu mbili ili hali timu ya Simba hayupo kwenye orodha yao iliyopelekwa TFF?

Ukweli kinachoonekana Pius Buswita amechukua pesa za Simba kwa ajili ya makubaliano ya kusajili timu hiyo. Ila ukweli hakusajili. Kinachotakiwa Mchezaji huyo alipe alichochukua kwa timu ya simba na si kufungiwa kucheza mpira.

Ni sawa na mchezaji kufanya kosa nje ya uwanja (Mfano kupigana Disco au kumtukana mkewe) basi iwe sababu ya kufungiwa kucheza mpira kwa muda wa mwaka mmoja.

Kwa mwanzo huu wa TFF mpya ya kuanza kutoa adhabu kiuonevu na baada ya raundi ya kwanza ya ligi tayari ratiba ishaanza kusogezwa mbele, muda si mrefu tutaona uongozi wa Malinzi (ambao ni mbovu) ulikuwa na afadhali.
 
Yeye mchezaji mwenyewe anasemaje?, nyakati hizi mchezaji anasajiri klabu mbili ni dalili za kutojitambua..
 
Yeye mchezaji mwenyewe anasemaje?, nyakati hizi mchezaji anasajiri klabu mbili ni dalili za kutojitambua..
Hajajisajili timu mbili, alichukua kishika uchumba Simba lakini akasaini Yanga. Sijui umeelewa?
 
Hajajisajili timu mbili, alichukua kishika uchumba Simba lakini akasaini Yanga. Sijui umeelewa?
Hayo ni makubariano kabla hajasaini contract!... ukienda kinyume chake ni utaperi...kwanini uingie huko kwenye utata?
 
Haya ni maelezo ya upande mmoja hatujawasikia tff ushahidi wao
Haya wasubiri. Simba wao hawakupeleka jina la Buswita huko TFF, hilo liko wazi. Sasa inawezekana Karia ndiye aliyehusika kumsainisha
 
Hayo ni makubariano kabla hajasaini contract!... ukienda kinyume chake ni utaperi...kwanini uingie huko kwenye utata?
Asante. Haya hayaihusu TFF, iweje wamwadhibu kwa kumfungia wakati wao wanasimamia mikataba tu? Hilo ni suala LA kuchunguzwa na polisi kisha likapelekwa mahakamani.
 
Hivi haki za vilabu, ni nani anaesimamia pale inapotokea wachezaji wenye tamaa, kuitapeli klabu, kwa kulamba pesa zao, alafu anaenda kusaini kwingine.
 
Hivi haki za vilabu, ni nani anaesimamia pale inapotokea wachezaji wenye tamaa, kuitapeli klabu, kwa kulamba pesa zao, alafu anaenda kusaini kwingine.
Ni kweli,
Buswita kama alipenda kujiunga na Yanga fc huku ameshachukua pesa za Simba sc, angerudisha kwanza Pesa ya Simba na kuyafuta makubaliano yake ya awali na timu hiyo.
Hapo angekuwa huru kusaini timu anayoipenda yeye.
Kusaini Timu nyingine huku akiwa amechukua pesa za makubaliano ya awali timu nyingine na kukaa kimya ni utapeli kama utapeli mwingine wowote ule.
Pesa ya Simba sc, nani atailipa ?
Je ni halali kwake kufanya huo utapeli kwasababu tu amebadili mawazo na kuamua kujiunga na Yanga fc ?
Nidhamu ya mchezaji bora inaanzia nje ya Uwanja.
 
 
Alichukua pesa simba na akasaini simba, angalia post #11
 
Asante. Haya hayaihusu TFF, iweje wamwadhibu kwa kumfungia wakati wao wanasimamia mikataba tu? Hilo ni suala LA kuchunguzwa na polisi kisha likapelekwa mahakamani.
 

Attachments

  • IMG-20170901-WA0001.jpg
    53.1 KB · Views: 32
nyie ndio mnawajaza ujinga wachezaji mwache afungiwe kuwa mchezaji mzuri ni pamoja na kuwa na nidhamu huyu hana nidhamu
 
Je akirudisha pesa alizochukua simba ataondolewa kifungo
cha kutokucheza kwa mwaka mmoja?
Kosa la utapeli ni la kupelekwa mahakamani ikiwa
Simba wana ushahidi wa kufanya hivyo.
 
mbona yule dogo aliechukua pesa za yanga za kishika uchumba alizirudisha kwanza then akawaambia amebadili mawazo anaenda AZAM na mambo yakaisha.. huyu ilikuaje ashindwe kuwaambia simba kuwa amebadili mawazo anakwenda yanga pesa zao awarudishie... au alijiona mjanja kwa kuwa ahajasini basi atawadhulumu hajui kuwa anaweza fungwa kwa utapeli... halafu eti anadai alilazimishwa kusign simba kwa kutishiwa maisha. hivi kweli karne hii mtu atishiwe kuuwa asiposign kuchezea club.. dah huyu dogo kachemsha
 
na hata kama alitishiwa ni kwanini hakupeleka suala lake kwenye vyombo husika?
 
Yeye mchezaji mwenyewe anasemaje?, nyakati hizi mchezaji anasajiri klabu mbili ni dalili za kutojitambua..
Hiyo ni sababu tosha ya kubatilisha adhabu ya TFF. Hakupewa hiyo nafasi na TFF ilhali kanuni ya msingi ya utoaji haki popote pale, kwa yeyote yule, ni kupewa nafasi ya kujieleza na kusikilizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…