Sakata la mahindi litaondoka na serikali?

Hili tatizo limesababishwa na serikali wenyewe kila siku wanakuja na sheria mpya wanawanyima wafanya biashara kuuza soko wanalotaka wao kwa manufaa ya wakulima. Kuna wakati hakuna kuuza mahindi nje mara uzeni mara tutanunua hata hujui kesho watakuja na sheria zipi bila kujali watu wame invest wewe huchangii katika gharama zao ikifika siku wanataka kufanya biashara wanaingiza pua zao utasema walitoa ruzuku kusaidia kilimo. acha soko huru wauze wanakotaka ili uhitaji uwe mkubwa na bei itapanda wateja wakiwa ni wengi bei itajihukumu yenyewe kama soko huru tuache kuingilia biashara za watu. Ni kama ndege wakiona booking watu wengi bei zinapanda mnaweza kuwa mko wote ndani ya ndege lakini kila mtu kalipa bei tofauti. Usifanye regulation katika bei acha soko lihukumu iwe usafirishaji, wakulima hata real estate. Mwezi wa 6 nilikuwa Dar hotel zote bei juu sababu high season ni sawa lakini sasa ije mfano mwaka mpya wenye magari hakuna kupandisha bei askari wameshajaa mbona hawafanyi kwa biashara zingine. Kama Mahindi waacheni wauze wanakotaka kwenye maslahi kwao serikali kusanya kodo stahiki tu biashara sio jukumu lako.
 
Mkuu Nawatania, huwatani unasema kweli tu. Matatizo ya kilimo chetu hayapewi ufumbuzi sahihi wa kuyatatua, ndio maana leo vijana wengi wapo mjini na kufanyabiashara ya umachinga baada ya kuona kwamba kilimo hakilipi inavyotakiwa kwa sababu ya gharama za kilimo. Wakulima wengi sasa ni wazee ambao hawana uwezo na pilikapilika za kutafuta masoko mbali. Aidha kwenye kilimo kuna matatizo mengi sana, ila kwa sababu kilimo ni nature basi twende hivyo hivyo.
 
Watu Hawali milo mitatu siku hizi..umasikini umezidi...ndio maana mahindi hayatoki. Walishaharibu masoko...it is hard to get masoko tuliyokuwa nayo wakati wa kikwete...
 
Serikali ya wajinga labda, serikali ndio inapanga bei ya mahindi sokoni? Kuna mtu aliambiwa alime? Alafu hizi bei ziko hivi mwaka wa 3 huu sasa sijui kiwewe kinatoka wapi kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…