Sakata la Makinikia linatuonesha Watanzania tusivyo wamoja


..chochote tunachohitaji kujua kuhusu wizi wao tunaweza kukipata kupitia taarifa za mapato yao.

..pia angekuwa informant asingekuwa exposed kwa kupewa ubunge, bali angefichwa asijulikane.

..Nia ya ripoti na sakata lililofuatia ilikuwa kutafuta umaarufu wa kisiasa tu, vinginevyo kusingekuwa na ulaghai-laghai na maigizo ikiwemo kudanganyana kwamba Barrick ni wazuri na Acacia wabaya.
 

..siku ripoti inapokelewa kuna wasanii waliitwa Ikulu kuimba.

..toka lini zoezi la kupokea ripoti za kichunguzi za kitaalamu likasindikizwa na nyimbo za " kizalendo" za wasanii?
 
..siku ripoti inapokelewa kuna wasanii waliitwa Ikulu kuimba.

..toka lini zoezi la kupokea ripoti za kichunguzi za kitaalamu likasindikizwa na nyimbo za " kizalendo" za wasanii?

Ahaa😂😂 ahaa, kipindi kile ndio ulitokea uzalendo wa maigizo. Kukazuka na utaratibu wa kualika viongozi wa dini kwenye hizo hafla, ili kuhadaa umma kuwa tuna kiongozi mzalendo na mcha Mungu. Utawala ule rasmi ndio umetuachia haya madhara ya chawa hadi kwenye utawala huu.
 
Hakika, kuna porojo nyingi sana za viongozi Panapo rasilimali za Tanzania
 
Tutakuwaje pamoja wakati wengine wanakula nyama,sie tunapiga mihayo!walioingia mikataba ya kishenzi ni ccm!harafu wanazunguka huku kudangsnya watu kwamba sie tumetoa maisha yetu kupigania wengine,wazungu wanatuibia!!
Ujinga mtupu,kama wale Ma profesa walioandika ile ripoti ya makinikia,walikuwa na huo utaalam,ilikuwaje miaka yote tangu mkspa hawajawahi kusema?
Hawa maprofesa wetu ni njaa tu,mtu kazoea kushika chaki,leo una mpa V8 atasema lolote,Kabudi aliponogewa na utamu,akasema yeye ni nani,Rais kamtoa jararani!akaenda kutuletea dawa ya corona mpaka leo kimya,wengine walilipwa pesa wakasema,samaki mto mara wanakufa kwa kula mbolea ya ngombe!!!
 
Akili yako inakutosha kuvaa na kuvua nguo tu unapiingiliwa na mumeo. Huna ubongo wa kuchakata mada kama hizi. Haya nenda ukavue usubiri shughuli ya usiku
Rudia kusoma uliyoyandika utaona mwenyewe ulivyo mpuuzi na juha
 
..Tundu Lissu mtetezi wa rasilimali kwa miaka 20++ anatangazwa msaliti na kuhukumiwa kifo.

..Bosi wa Acacia, kampuni aliyoiba madini, anateuliwa na Ccm kugombea ubunge.

..Wazungu mabosi wa Acacia toka Canada wanakaribishwa Ikulu na kupewa 90%+ discount ya kulipa walichotuibia.

..Mawaziri, Wanasheria Wakuu, Makatibu Wakuu, Makamishna, wa wizara ya madini hakuna anayeguswa.

..Katika mazingira hayo ni nani anaweza kuamini kuwa tulikuwa tunatetea madini yetu?
 
Kama kweli alikuwa na uwazi huo, yale mazungumzo ya kina Kabudi yangewekwa hadharani.
Mazungumzo hatima yake si ndo yale mafaini ya ma trilioni, au ?

Na baadae Mkanada akaja kuomba poo ? Akasema wamekubaliana waingie joint venture ya TWIGA ?


Ni nini sasa kilifichwa ?
 
Na kwanini tumekwenda kupiga marisasi kwa nia ya kuua mkosoaji wa ripoti za serikali. Hivi mkosoaji wa ripoti anastahili kuuwawa, na muandamizi wa Acacia anastahili ubunge wa Ccm?

..Kwa maoni yangu ripoti zilikuwa na malengo ya KISIASA tu.
Hapo kwenye kumshambulia mkosoaji ndio doa kubwa kabisa kwenye utawala wa Magufuli....sidhani kama wahusika walitathmini athari zake baadae.

Hilo la utata wa ripoti husika bado ni mtanziko namna hayo mabilioni ya $ yalivyosamehewa huku watuhumiwa wakikwepa mkono wa sheria na taifa kupoozwa na kishika uchumba.

.. anyway ile Vita ya kiuchumi iliyokuwa inaimbwa huenda nayo ilikuwa sehemu ya siasa tu za kupata uungwaji mkono wa raia kwenye utawala ule na kuhalalisha katiba kusiginwa .
zitto junior Tindo Nguruvi3 Mag3
Pascal Mayalla
 
Mazungumzo hatima yake si ndo yale mafaini ya ma trilioni, au ?

Na baadae Mkanada akaja kuomba poo ? Akasema wamekubaliana waingie joint venture ya TWIGA ?


Ni nini sasa kilifichwa ?

Ni wapi kuna faini ya matrilioni? Zile zilikuwa ni ndoto za mchana. Barrick walisema watatoa $300m kama Goodwill na sio faini yoyote. Mcanada hakuja kuomba po yoyote, bali alifuatilia biashara yake ambayo iliingiliwa na rais wetu. Lakini hakuna popote tulidhibitisha kuwa tunawadai Barrick.

Hiyo kampuni ya Twiga sisi ndio tuliomba ianzishwe ili kufanya wananchi waone na wao wanafaidika na raslimali zao. Lakini fuatilia vizuri utakuta hiyo 16% ni ya kujifariji tu, lakini hamna lolote. Kama ingekuwa tunapata hiyo 16% kweli, usingeona tunakimbizana na hizi tozo uchwara za miamala ya simu.
 
1. Kama ripoti zilikuwa za kweli kwanini Tanzania haikuwashtaki Acacia ktk mahakama ya kimataifa ya migogoro ya uwekezaji?

2. Kama ripoti zilikuwa za kweli kwanini tumelipwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na madai yetu ya usd 191 billion?

3. Kishika uchumba cha usd 300 million ni 0.16% ya madai yetu dhidi ya Acacia.

4. Serikali haikuchukua hatua zozote dhidi ya waliohusika kuiingiza nchi ktk mikataba mibovu. Hakuna hata mmoja aliyefunguliwa mashtaka.

5. Chama cha mapinduzi CCM kilimpitisha, Deo Mwanyika, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Acacia kuwa mgombea ubunge wa Njombe mjini.

6.Kama Acacia walituibia kiasi kikubwa namna ile inawezekanaje mmoja wa watendaji wake wakuu aaminiwe na Ccm kuwa mbunge?
 
Kila nikitafakari hili jambo naona kama Magufuli alikula mchongo na Barick. Kwa nini Deo ambaye ni mtuhumiwa wetu aliyewekwa ndani muda wote huo, asamehewe kwa kuambiwa alipe fidia na mara akaenda kuwa mgombea ubunge wa ccm?
Baada yakulipa pre bargain alipewa kifuta majanga
 
Hakika, kuna porojo nyingi sana za viongozi Panapo rasilimali za Tanzania
Kwenye siasa za nchi maskini, uongozi ni kitu muhimu sana,ndiko kwenye malipo makubwa zaidi kuzidi hata zile taaluma ngumu. Mtu haoni shida kusema uongo hata kama utaleta madhara kwa watu.
Issue ya makinikia iliharibu maisha ya watu wengi sana, kwani lundo kubwa la wafanyakazi liliondolewa kazini baada ya mgodi kusimama. Kumbuka bulyankulu mine ilikuwa inaajiri watu wengi zaidi pengine kuzidi migodi mingine hapa nchini, lakini unamsikia mtu anasema Mimi sijali hata hao wakikosa kazi ni wachache mno. Ni sawa, basi uwe na uhakika na hayo madai. Sheria zenyewe za kazi ni hovyo tu,.
 
Ina maana huamini zile ripoti? Na yale majadiliano ya kina Kabudi je ?
Magufuli aliwadanganya Watanzania kuhusu Tsh 360 Trillion kutoka ACÀCIA sawa na Kinjekitile alivyowadanganya Wamatumbi mwaka 1905 kuwa risasi za mjerumani zitageuka maji. Maelfu walikufa kwa UJINGA ule. Naye Magufuli kaacha wajinga wengi Tanzania
 
Mlipigwa mkapigika.SEHEMU IKIWA NA WAJINGA WENGI,BASI NI MTAJI NA FAIDA KWA WALIO NA AKILI.
 
Mpinzire maswali yako haya. Majibu tafadhali...
 

..tatizo mkosoaji hakufa kama walivyopanga.

..Na mkosoaji alipotua nchini muuaji alikuwa akienda "gereji" mara kwa mara.

..kama utakumbuka hata kwenye msiba wa mstaafu kule kusini muuaji alichelewa kufika nadhani sababu ya maradhi.
 
Hili jambo inapaswa kama Taifa tuungane na kumdai beberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…