Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MAJIBU dhidi ya mke wa Rais Jakaya Kikwete anayokabiliwa na tuhuma za kutumia fedha za serikali katika kampeni limekanushwa na kutolewa ufafanuzi na chama hicho. UFafanuzi huo ulitolewa jana, na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi, Abralrahman Kinana mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Kinana alisema kuwa, Mama Salma Kikwete anatumia fedha za CCM katika kampeni na si fedha za serikali kama inavyodaiwa na Dk. Slaa
Alisema huku akijibu tuhuma hizo alifafanua kuwa, ni kweli Mama Salma alitumia ndege ya serikali katika kampeni zake za kanda ya ziwa ila CCM ilikodi ndege hiyo kwa wakala wa ndege za serikali na hawakuitumia kama kiongozi wa serikali na alionyesha stakabadhi ya malipo walipokodi ndege hiyo.
Alisema ndege hizo za wakala wa ndege za serikali zinakodishwa na mtu yoyote na wao walifanya hivyo kama wateja na si vinginevyo
Pia CCM kilimtaka mgombea huyo kuwajibika na suala zima la kampeni na si kuwema malumbano kila kukicha na kuacha shughuli muhimu ya kampeni ambayo inawakabili mbele yao.
Awali mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Dk. Wilbrod Slaa ilitakra chama hicho kujibu tuhuma kwa kukiri wanachama wa CCM hutumia fedha za serikali katika kampeni zake.
Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.