Elections 2010 Sakata la Mama Kikwete lajibiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MAJIBU dhidi ya mke wa Rais Jakaya Kikwete anayokabiliwa na tuhuma za kutumia fedha za serikali katika kampeni limekanushwa na kutolewa ufafanuzi na chama hicho. UFafanuzi huo ulitolewa jana, na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi, Abralrahman Kinana mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Kinana alisema kuwa, Mama Salma Kikwete anatumia fedha za CCM katika kampeni na si fedha za serikali kama inavyodaiwa na Dk. Slaa

Alisema huku akijibu tuhuma hizo alifafanua kuwa, ni kweli Mama Salma alitumia ndege ya serikali katika kampeni zake za kanda ya ziwa ila CCM ilikodi ndege hiyo kwa wakala wa ndege za serikali na hawakuitumia kama kiongozi wa serikali na alionyesha stakabadhi ya malipo walipokodi ndege hiyo.

Alisema ndege hizo za wakala wa ndege za serikali zinakodishwa na mtu yoyote na wao walifanya hivyo kama wateja na si vinginevyo

Pia CCM kilimtaka mgombea huyo kuwajibika na suala zima la kampeni na si kuwema malumbano kila kukicha na kuacha shughuli muhimu ya kampeni ambayo inawakabili mbele yao.

Awali mgombea wa urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Dk. Wilbrod Slaa ilitakra chama hicho kujibu tuhuma kwa kukiri wanachama wa CCM hutumia fedha za serikali katika kampeni zake.

Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Nafkiri wameisoma hii hata kama hawajibu...:becky:
 
Stakabadhi zenyewe alizotoa Kinana ni fake. Huu si mwisho wa suala hili.
 
Hizo sio stakabadhi bali ni hati za madai. CCM bado hawajathibitisha kuwa wamelipa hizo fedha kwa kuonyesha risiti ya pesa kupokelewa.
 
Stakabadhi zenyewe alizotoa Kinana ni fake. Huu si mwisho wa suala hili.

CCM inaongozwa na watu waliopinda akili kama kinana, anaita waandishi wa habari kuwaonyesha hati ya madai (invoice) kwa kuvimbisha mashavu kuwa ccm wamelipa pesa kwa huduma ya kukodisha ndege. Kuna haja ya vongozi vilaza kama hawa wapewe darasa la kutofautisha stababathi na hati ya madai.

Kinana hakikisha pesa za serikali zinalipwa mapema, mtalinyonga hili shirika dogo kama mlivyofanya ATC
 
Dah, kumbe mtu yeyote anaweza kuikodi ndege ya rais? Incredible, basi si waipeleke tours? Haya maelezo kwa mwenye kufikiri vizuri hayaingii akilini!
 
Hizo sio stakabadhi bali ni hati za madai. CCM bado hawajathibitisha kuwa wamelipa hizo fedha kwa kuonyesha risiti ya pesa kupokelewa.

Pia TFGA nao wathibitishe kuwa wamelipa VAT na TRA nao wathibitishe kuwa kodi yetu imelipwa!!!
 
Dah, kumbe mtu yeyote anaweza kuikodi ndege ya rais? Incredible, basi si waipeleke tours? Haya maelezo kwa mwenye kufikiri vizuri hayaingii akilini!

Ndege ya Rais haimo katika ndege za wakala wa serikali!!
 
Wee September, acha kudandia TGV kwa mbele. Utapata mimba bureee.

Hizi mbona ziliwekwa hapa JF na kwa Michuzi? Kama hujui wee uliza kuliko kuanza kuonyesha ushamba wako hapa.

Wewe uliziona?
 
Stakabadhi zenyewe alizotoa Kinana ni fake. Huu si mwisho wa suala hili.

Nakubaliana nawe 100% huu siyo mwisho wa sakata hilo. Subirini tu CCM na huyo Salma wataumbuka vibaya sana muda si mrefu. Hizo stakabadhi zina utata mkubwa saaaaanaaaa!!!
 
Nazani issue sio endapo ni stakabadhi au hati ya madai; but issue ni nani yupo responsible na stakabadhi au hati ya madai husika; CCM au serikali!!!!???
 
Wee September, acha kudandia TGV kwa mbele. Utapata mimba bureee.

Hizi mbona ziliwekwa hapa JF na kwa Michuzi? Kama hujui wee uliza kuliko kuanza kuonyesha ushamba wako hapa.

Ukiniwekea picha ya mama yako utasema nimemuona mama yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…