Sakata la Mizania: Kwanini Magufuli ni mbabaishaji?

Sakata la Mizania: Kwanini Magufuli ni mbabaishaji?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Sakata la mizania limeonyesha Magufuli siyo mkomavu wa kiutawala na anadhani kwa kutumia mabavu na vitisho basi ataogopwa na kuendelea kupesa lakini ukweli ni kama ifuatavyo:-

1) Magari ya aina zote hususani makubwa yamekuwa yakibebeshwa mizigo mikubwa ya marejeo ya kodi kinyume na sheria ya kodi. Utitiri wa aina mbalimbali za kodi zimeelekezwa kwenye vyombo vya usafiri na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa mlaji na kudhoofu kwa ushindani wa wafanya biashara wetu kwenye soko la Afrika mashariki.

2) Tangia JK aingie madarakani hususani kipindi cha Meghji akiwa Waziri wa fedha tumeona vyombo vya usafiri vikibebeshwa mzigo mkubwa wa kodi kupitia mafuta, gharama za usajili wa magari, kodi za umiliki wa magari, n.k kwa visingizio vya kuuwezesha mfuko wa barabara kumudu gharama za matengenezo ya barabara.

3) Hoja za maongezeko makubwa ya gharama za kodi kwa madai potofu ya matengenezo ya barabara yamekuja wakati ushindani wa kandarasi za barabara umepotea na hivyo kuongeza maradufu gharama za matengenezo ya barabara na hivyo kukamuliwa kwa wananchi hakwendani na kasi ya matengenezo ya barabara.

4) Katika mizania utaikuta yote ipo upande mmoja na hakuna hata maeneo ya kupaki na hivyo kuleta usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa barabara wa aina zote hata wale wa magari madogo. Kama kila upande wa barabara ungelikuwa na kituo chake na kiwe na sehemu kubwa ya kupaki na mizania nazo zikawa angalau tatu kila upande wa barabara misongamano ingelipungua sana.

5) Njia rahisi ya kuthibiti uzito wa magari ni namba ya axles na kuhimiza matumizi mazuri ya barabara ukadiriaji kwa wale ambao wangelipendelea ungelipunguza sana misongamano kwenye vituo vya mizania.

6) Mabasi yangeliondolewa udhia wa kupima na hivyo kuwaondolea abiria karaha za kusimama sana njiani. Hili kufanyika ni vigumu kwa sababu wakubwa hawaguswi na karaha tajwa. Nchi nyingi zenye usafiri wa mabasi huwa wenye mabasi hawatakiwi kupima mizigo kwa sababu abiria ni mfalme lakini hapa nchini raia wa ngazi ya chini hathaminiwi na ndiyo maana hakuna kiongozi anayekerwa na maudhi mengi wasafiri wanayoyapata barabarani ambako hata vyoo kwenye mizania hizo hakuna na vilivyopo havifanyi kazi kutokana na pesa zipatikanazo kwenye ushuru huu kutorejeshwa kutoa huduma kwa wateja husika.

7) Hakuna chombo huria ambacho kinahakiki ubora wa mizania zinazotumika na upo ushahidi kuwa watendaji wasio waaminifu wamekuwa wakizichakachua zionyeshe uzito batili na kuwapa ubavu wa kudai hongo.

8) Sehemu kubwa ya mapato haya ya ushuru kutoka kwenye mizania hayafiki serikalini bali huishia mikononi mwa wajanja wachache. Hata wafanyakazi wanaochaguliwa au kuondolewa kwenye maeneo haya huchukulia aidha ni kupandishwa cheo au ni adhabu kwa kuondolewa kwenye nafasi ya ulaji kama hii. Sasa kama mapato haya hayafiki serikalini kufanya shughuli za kujenga barabara kwa nini yasifutwe na ushuru huu ukawekwa kwenye mafuta na kupunguza gharama nyingi za uendeshaji wa kufanikisha mradi huu kwa manufaa ya watu wachache? Magari yawe yanapimwa ili kukusanya takwimu za matumizi ya barabara lakini ushuru uondolewe na kuingizwa kwenye mafuta ambako uzito wa gari unachangia katika matumizi halisi ya mafuta.

9) Kwavile mizania hizi mapato yako ni kiduchu kutokana mianya mingi ya ufisadi hivi Magufuli haoni ana kila sababu ya kuishauri serikali kuachana nayo na kupima faida na hasara ya ajira kubwa iliyopo kwenye mizania hizo ikiwa na pamoja na miundombinu ambayo inaonyesha wizara yake inafurahia kulea mianya ya kifisadi badala ya kuibomoa na kutuaacha na maswali mengi hivi Mheshimiwa Waziri Magufuli mgawo wake kwa mwezi huwa ni ngapi?

10) Kiujumla shughuli zote za ukusanyaji wa mapato ni jukumu la TRA sasa yawaje Wizara ya Ujenzi iwe na kajimradi kake kadogo ambako hakana uthibiti wowote ule?
 
Si katika mizani tu,bali maeneo mengi aliyo pita Magufuli ameonesha he's like robot,asiye na reasoning katika kutekeleza yale anaagizwa kufanya.
nahisi hata JK akimwita:
John,nenda chinja Invisible pale,
Atajibu,"Sawa mzee,panga likwapi?"
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom