Sakata la Morrison Kinachoendelea

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Uongozi wa klabu ya Yanga umetoa taarifa kuhusu maendeleo ya kesi waliyofungua dhidi ya winga wao wa zamani Bernard Morrison.

Akizungumza mapema leo kutoka jijini Mbeya, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kesi hiyo itasikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) na tayari imepangiwa Jaji

Mwakalebela amesema baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko yao CAS, Morrison alitakiwa kujibu malalamiko hayo na juzi Yanga imepokea barua kutoka CAS ikiwataarifu kuwa majibu aliyotoa Morrison hayana mashiko na hivyo wanapaswa kulipia pesa za Kifaransa franc 12,000 ili kesi hiyo inze kusikilizwa

Malipo hayo yanapaswa kufanyika kabla ya Januari 12 2021 ambapo pande zote zimetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha

"Yanga tulipeleka malalamiko Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) kupinga maamuzi ya kubatilisha mkataba wa Bernard Morisson na Yanga yaliyotolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF"

"Morrison alitakiwa kujibu malalamiko yetu na juzi tumepokea barua kutoka CAS iliyotutaarifu kuwa majibu yaliyotolewa na Morrison hayana mashiko na kwamba shauri letu litapangiwa Jaji wa kuendelea kulisikiliza"

"Hadi kufikia Leo hii, Jaji ameshapatikana, Morrison na Yanga sote kila mmoja tunapaswa kulipa Franc 12,000 tayari shauri hilo kuanza kusikilizwa"

"Tarehe ya mwisho ya fedha hizo kulipwa ni Januari 12 2021, sisi kama walalamikaji tutalipa fedha hizo ili shauri lisikilizwe", alisema Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga.
 
Mwakalebela amelikomalia sana hili swala,na watu wanamchukulia poa na kumkebehi kwa umbo la mwili wake ,labda atapata majibu sahihi ya kile anachokiamini soon,pamoja na hayo Simba nao walijichanganya kwa huyu mchezaji ata mienendo yako si mizuri.
 
yangu macho!! yanga hili shauri hamshindi na hamtashinda! viongozi wenu walipeleka hili shauri huko CAS kama kuwaridhisha mashabiki lakini imekuwa kama zali tu CAS wamewaita kulisikiliza. ngoja tusubiri mtanambia.
 
yangu macho!! yanga hili shauri hamshindi na hamtashinda! viongozi wenu walipeleka hili shauri huko CAS kama kuwaridhisha mashabiki lakini imekuwa kama zali tu CAS wamewaita kulisikiliza. ngoja tusubiri mtanambia.
Mpaka kasimamishwa yule Morrison kucheza na kuambiwa utetezi wake hauna mashiko anakesi ya kujibu,unadhani anaenda kwenye kamati ya msomali?
 
Mwakalebela amelikomalia sana hili swala,na watu wanamchukulia poa na kumkebehi kwa umbo la mwili wake ,labda atapata majibu sahihi ya kile anachokiamini soon,pamoja na hayo Simba nao walijichanganya kwa huyu mchezaji ata mienendo yako si mizuri.
Kaka yake MO niliwahi msikia akishauri huyo mchezaji kuwa hafai kabisa kusajiliwa na timu yake,ila kwasababu ya mambumbumbu wengi msimbazi (Rage),walidhani wanaikomoa Yanga,saizi hawasaidii maana hachezi na makesi hayaishi,mastress kibao.......mara vidole.....walidhani atawasaidia saizi anawapanda vichwani kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…