Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Vijana wa CCM ambao wana uchungu wa dhati na wanalitakia mema taifa lao na Chama chao wanapaswa kusimama imara na kuunga mkono mwenzao anayeonyesha ujasiri wa kupambana na uovu uliopo. Hata kama Nape anafanya kampeni za kuutaka uenyekiti wa UVCCM, ameonyesha ujasiri mkubwa. Nape ni jasiri. Anastahili pongezi maana ni wachache wanaoweza kujitokeza na kuwanyooshea vidole watu 'wanaoogopwa' kwa mengi
Nape kama unasoma hapa kaza uzi wa kupambana na mafisadi ndani ya CCM usiogope lakini uwe mwangalifu maana hawatasita hata kidogo kukutoa roho ili watimize ufisadi wao.
Sijapata kumuongelea mama yenu mpendwa ana kilango,kwa kuwa siongeleagi watu wajinga....Wewe ni kati ya wanaomdanganya Nape kuwa alipuke nao watamsaidia.nilipata kusema hapo nyuma kuwa ata kwa muujiza Nape hawezi jina lake kurudi kwa uenyekiti wa uvccm...leo narudia tena kwa faida yako na wengine wote wasio na jazba kama wewe....jina la nape haliwezi kurudi ata iweje...why?kwanza amekosea sana kutukana wenzie kuwa ni mafisadi ata kama ana hoja,kila kitu kina wakati wake wa kusema,kuwahi kwake kutamzuia kufika popote....pili ni wazi kuwa kanuni inasema mgombea uenyekiti ni lazima awe chini ya miaka 35 anapomaliza muhula wake.Nape kazaliwa mwaka wa 1977.leo ni 2008.ata mtoto wangu nikimpa hesabu hio nyepesi ni wazi kuwa Nape kavuka umri.....mimi nasema jina la Nape likipitishwa na kamati kuu ya m naenda mahakamani kuusimimisha.maana watakuwa wamevunja kanuni iliotuzuia wengi kuchukua form.na nitawashinda na atazuiwa kugombea.Unajua kila ninapsoma post zako ninasikia kutapika, mtu mzima unapokuwa kama mtoto mdogo, hivi unachohangaikia ni nini hasa? Hivi huoni aibu?
Exactly unachoweza kufanya ni nini? Nape ni mjumbe wa NEC, hivi kweli wewe una ndoto hata siku moja kufikia huko? Yaani wewe unayehangaika kutoka majuu lkumfuata Malecela Dodoma, wakati hata kwenu hujaenda kuona ndugu zako leo una ubavu wa kusema haya?
Mijitu mingine bwana yaani hovyo! Nape anaondoka huyo, hakuna cha nani wala nani, kuna watu wengi tu tunaomuunga mkono, sasa tumesubiri aguswe tu na mafisadi uone mtoto utakaowaka, unafikiri amemka tu na kusema?
Subiri uone, ila next time usiniingize kwenye maneno yako ya choooni, nilishakuambia siku nyingi sana kuwa nilishakudharau siku nyingi sana, sasa nashangaa kwamba bado tu jina langu, la Malecela, na mama kilango hayakutoki mdomoni vipi mkuu?
Mkuu Kitila,
tunahitaji vijana imara kama huyu bwana mdogo, it is about time ukampa nafasi na yeye aonyeshe vitu vyake kwa taifa letu.
Ahsante mkuu!
Nashauri jina lako umalizie na herufi "o" mwishoni ndio litatoa maana yako halisi.....tumuongelee Nhimbi kama Nchimbi maana tukianza kuongelea kuwa ana Diploma tu au la sio issue hapa kwa kuwa tuna wachangiaje wengi hapa watajiona wamekuwa offended kwa kuwa wao pia hawana....Nchimbi siyo mshamba,vigezo gani umetumia wewe wa mjini,ni mwanasisa mjanja ambaye hajapata kukosea karata zake,ameutawala uvcmm kwa miaka kumi sasa.nani aliweza?walishindwa wengi sana.Anaweza kampeni za wananhi na za ndani ya chama pia na ndio maana alishinda kwa kishindo ubunge wa songea mjini.na wala msiombe afanye maamuzi ya kumpinga Nape kwa kuwa kitakuwa ni kimbunga ambacho Nape kamwe hatokimudu.TATIZO NDANI YA UVCCM NI NCHIMBI: elimu ndogo (kazi kununua digrii za Ph.D wakati ana Diploma tu ya Mzumbe), ushamba (kipofu kaona mwezi!), ufisadi (ni errand boy wa Rostam, Lowassa na Karamagi na usanii wa kuact as if ni msomi kumbe hata kuandika jina lake ni taabu.
Ni wazi lazima apelekwe mahakamani...jamaa ni muongo sana.anasma kuwa mkataba ulisainiwa usiku,wakati hakuna mkataba uliosainiwa kwa kweli.na hata makala yenyewe hakuna mahali walipofafanua zaidi kuwa kusaini usiku maana yake ni nini...pia si kweli mkataba umesainiwa bali ni ujinga wa kulewa wa Kubena.kwani kilichosainiwa ni memorundum of understanding.Kesi zote zinaendelea vema na muda si mrefu Kubenea atajua hayuko above the law.
Ni wazi lazima apelekwe mahakamani...jamaa ni muongo sana.anasma kuwa mkataba ulisainiwa usiku,wakati hakuna mkataba uliosainiwa kwa kweli.na hata makala yenyewe hakuna mahali walipofafanua zaidi kuwa kusaini usiku maana yake ni nini...pia si kweli mkataba umesainiwa bali ni ujinga wa kulewa wa Kubena.kwani kilichosainiwa ni memorundum of understanding.Kesi zote zinaendelea vema na muda si mrefu Kubenea atajua hayuko above the law.