Ili mtu apatikane na hatia ni lazima kuwe na ushahidi
Ndugu yangu Ipole, ni nani ambaye anatakiwa kupeleka ushahidi? Polisi ndiyo ambao wanaongoza kwa kuficha ushahidi ama kuvuruga ushahidi na hasa kama mhusika wa kesi ni kigogo kama ilivyo kwa vigogo wa EPA ambao mpaka leo hii haijulikani hatima yao ni nini.
Fikiria Waziri Mkuu anasema watuhumiwa wa EPA ni watu wazito sana na hivyo serikali inabidi iende taratibu (hapo ina maana ni kuwabembeleza na ndicho Kamati ya Mwanyika imekuwa ikifanya eti wanaongea nao ili warudishe fedha). Hivi kweli unaweza kukaa kujadiliana na mwizi kwamba arudishe kwanza hela?
IGP Mwema kwa maneno yake alitamka wazi kwamba nchi hii imetekwa na mafisadi. Kauli kama hiyo ilihitaji IGP ahojiwe alikuwa anamaanisha nini wakati yeye ndiyo yuko responsible kuhakikisha kwamba sheria za nchi hazivunjwi? Kauli hiyo ilikuwa na maana nzito sana kwamba kuna vikwazo vingi ambavyo polisi wanakumbana navyo katika kutekeleza wajibu wao, to be specific ni kwamba kila kona wanakutana na kigingi cha fisadi ambalo linalindwa na ofisi kubwa na hivyo mafisadi hayagusiki.
Je, baada ya kauli ya Mwakyembe bungeni umemsikia mbunge yeyote akitetea ama kusafisha waliotuhumiwa na skendo ya Richmond? Hiyo ilikuwa message clear kwamba kuna mengi nyuma ya pazia na kama wangeanza kujadili upya mtu asingeishia kujiuzulu tu may be hata uanachama wake ungetenguliwa.
PCCB walichunguza kesi ya Mahalu ambayo sasa iko mahakamani, kipindi kile kile wakachunguza skendo ya Richmond wakasema hakuna kesi na deal lilikuwa safi kabisa. Bunge lilipokuja kupata matokeo tofauti wakaja kusema kwamba sheria ya PCCB iliyotumika kuchunguza Richmond ilikuwa butu, lakini sheria hiyo hiyo ilikuwa kali kwenye kuchunguza kesi ya Prof. Mahalu. Unapata picha gani ukilinganisha hayo matukio mawili?
Kwa hiyo swala la kudai ushahidi wakati Polisi, UWT na PCCB wamewekwa mikononi mwa mafisadi ni kazi ngumu sana. Polisi, UWT na PCCB ndiyo watu ambao responsible kusaka ushahidi once wanapopewa tuhuma. Sasa kama na wao wamefika mahali wamekubali kwamba nchi imetekwa na mafisadi, unategemea upate wapi ushahidi wa ufisadi? Kwa kifupi ni kwamba serikali yetu ni ya mafisadi na hivyo yanalindana, period!