mtambobajeti
Member
- Jun 22, 2008
- 5
- 0
PCCB walichunguza kesi ya Mahalu ambayo sasa iko mahakamani, kipindi kile kile wakachunguza skendo ya Richmond wakasema hakuna kesi na deal lilikuwa safi kabisa. Bunge lilipokuja kupata matokeo tofauti wakaja kusema kwamba sheria ya PCCB iliyotumika kuchunguza Richmond ilikuwa butu, lakini sheria hiyo hiyo ilikuwa kali kwenye kuchunguza kesi ya Prof. Mahalu. Unapata picha gani ukilinganisha hayo matukio mawili?
Umepotoka sana rafiki yangu.wewe ni kati ya wanaofata mkumbo bila kuujua ukweli.nenda kasome mwenyewe kwanza ripoti ya mwakyembe na uonyeshe ni wapi ambapo lowasa ametajwa kuwa amuhusika na ufisadi zaidi ya preamle ambayo haikiuwa na ukweli wowote kwani watu wameongea nje ya viapo...siku moja wanahistoria watasema ukweli na sie sisi ambao tayaritumehalibiwa akili na magazeti na tuna uoande ambao kamwe hatutaki ata kisikia upende wa pili wa shilingiHuu ufisadi sasa unafikia pabaya.
Yaani hao wanaoitwa wa usalama wanafuata nini huko kwa kubenea?Mbona hawajampekua EPA hata mmoja?
Huyu Lowassanae alishalaaniwa tangu zamani hana staha ya kuwa kiongozi.kila mahali anataka kula tu eti anajiandaa kuwa rais.Kweli anaweza kuongoza nchi hii?
Siku inakuja na ukweli huwa always unasimama.
Tutajua makapi ni yapi,pumba ni zipi nk
Hivi kumbe PCCB walipoharibu kwenye uchunguzi wa Richmond walisema tatizo lilikuwa sheria zilikuwa butu. Sasa Tume ya muda tu ya Bunge, ya Mwakyembe, ilitumia sheria gani ambazo Tume maalum ya kushughulikia rushwa nchini haina?
Na baada ya kusema sheria wanazotumia ni butu halafu ikawaje? Waliongezewa nguvu au ndio bado ni butu?
Sasa mahakama imewapaje search warrant ambayo ina neno "criminal" something, kama ambavyo Kubenea alitamka redioni?
Unajua katika sheria sio busara kuseme lolote kabla hujaona, sio tu shitaka, bali hata ushahidi, ambao mwenzio atakuja nao mahakamani. Huwezi kuanza kusema hakuna kesi hapa wakati hujui mwenzio analalamika nini.
Ingekuwa ni nchi yenye viable press tungekuwa tumeshafahamu yule Jaji alitoa search warrant kuhusiana na uvunjaji wa sheria gani. Bahati mbaya press yenyewe ndio hivyo tena.
samahani kaka kidogo,
kisutu hakuna jaji,ni hakimu.Endelea..............
Hahahahaha! Kuhani hapa umepatikana.Yashakuwa hayo!
Hahahahaha! Kuhani hapa umepatikana.
Wewe haya maneno uliambia na Lowassa Jana,naona ndiye anayaekutuma?tuambie Utajiri aliona alutoa wapi?Mie mwalimu aliniambi siku kimuona Lowassa nimuulize hilo swali
Mkuu kwanza kabisa ni kweli mimi siyo yule Mh.Thomas Mwang'onda, mbunge wa kuteuliwa.Hata hivyo, niko njiani kuwa na hadhi kama yake kwani natarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kwa uchaguzi ujao wa 2010 na kunyakua moja ya majimbo muhimu.Bora uzima!Bwn Tom,
..........sitaki kuamini kuwa ndio wewe mbunge wa kuteuliwa, kwani maneno yako hapo juu yametulia na yako deep....anyway..........well said Tom.......kijana Nape anahitaji ushauri.
.....sasa mkuu Tom hebu tueleze....inakuwaje mradi umeanza kabla ya kupata baraka za CC?........kwanini mradi uanze wakati vijana wanaupinga??...........na pengine hapo ndipo kijana Nape anazo inside information zote.........
.
Mkuu kwanza kabisa ni kweli mimi siyo yule Mh.Thomas Mwang'onda, mbunge wa kuteuliwa.Hata hivyo, niko njiani kuwa na hadhi kama yake kwani natarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kwa uchaguzi ujao wa 2010 na kunyakua moja ya majimbo muhimu.Bora uzima!
Mkuu kwa kujibu hoja zako ni kwamba,hili sakata la mradi wa jengo la UVCCM lina utata kidogo kutokana na ukweli kwamba taarifa za pande zote mbili yaani kutoka kwa bwana Nape na kutoka kwa uongozi wa UVCCM haziko wazi sana.
Bwana Nape alitoa shutuma tu,lakini hakuwa na ushahidi wowote ule wa kuuwasilisha mbele ya waandishi wa habari kama hatua muhimu ya kuipa nguvu hoja yake.Ningemuelewa Nape kama angetuletea hata nakala ya mkataba wenyewe, muhtsari wa kikao cha baraza kuu lililokaa kujadili mradi ili tuone kama ni kweli baraza liliupinga mkataba ama lah.
Unajua kama nilivyosema awali kwamba, kutokana na taratibu za vikao, inawezekana kabisa kuna baadhi ya wajumbe hawakuunga mkono. Hilo ni sawa kabisa kwa demokrasia ya vikao. Lakini linapokuja suala la kufikia maamuzi,kinachoangaliwa ni idadi ya wingi wa wajumbe waliounga au kutounga mkono hoja.
Huo ndio utaratibu wa vikao.Sasa hatuwezi kuhitimisha kwa kusema vijana waliupinga mkataba,kumbe walioupinga ni 10, 20 au 50, ambao kwa mujibu wa ikama ya wajumbe wa kikao, hoja zao zilimezwa na idadi kubwa ya wajumbe waliounga mkono.
Sasa ili kuondoa utata katika hili ilipaswa Nape, kwakuwa alishaamua kulipua bomu, basi angekuja kamili kamili. Angepaswa kubeba sehemu ya mkataba anayoipinga pamoja na muhstari wa kikao husika mbele ya mkutano wake na waandishi wa habari. Haya yote Nape hakuyafanya. Ndio maana binafsi inanipa tabu kuamini kama Nape anaelewa kwa undani mchakato mzima wa mkataba kwa ushahidi mahususi,ukiachilia mbali kuujua mchanganuo wa mradi pekee.
Mimi ninashawishika kuamini kwamba, kwa kujua kuwa vikao halali vya awali kama, baraza kuu na baraza la wadhamini la UVCCM vimeubariki mkataba wa mradi,uongozi wa UVCCM ukaona kuwa wanaweza kuanza shughuli za ujenzi wakati wanasubiri baraka za Kamati Kuu.Sasa hili kibiashara sioni kama ni tatizo.Kwa sababu,ukimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Mzee Makamba,anadai kuwa hata sekretarieti ya NEC iliuunga mkono mradi na hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni kufikisha agenda ya mradi huo mbele ya CC.
Sasa, kwa uozefu wangu ndani ya CCM,ni nadra sana sana, CC kupinga maamuzi ya sekretarieti.Na hii ni kwasababu sekretarieti inaundwa na wajumbe takribani saba wa CC pamoja na makatibu wakuu wa jumuiya za chama. Sasa hawa wajumbe walioko kwenye sekretarieti ndio watapaswa kutetea hoja walizozipitisha kwenye sekretareiti mbele ya CC.
Kinachoweza kufanyika ni kuagiza yafanyike baadhi ya marekebisho kwenye vifungu fulani fulani kama ikibidi. Na daima marekebisho hayo mara nyingi huwa yanalenga kuboresha tu.
Kwa hiyo, kimsingi mimi kwangu suala la mradi kuanza kabla ya baraka za CC sio hoja sana kwa kuzingatia ufafanuzi wa itafaki za vikao vya CCM kama nlivyojaribu kuuelezea hapo juu. Maana kuna suala la muda wa kuanza ujenzi kama ulivyokubalika katika mkataba pia lazima lizingatiwe. Mwekezaji yeye hatambui ratiba za vikao vya chama, yeye haingii mkataba wa kupiga propaganda, yeye anaingia mkataba wa kibiashara.Na katika biashara, kujali muda ni moja ya mambo ya msingi ili faida iliyokusudiwa iweze patikana kwa muda muafaka.
Tatizo kwangu lingekuwa kama kweli baraza kuu na baraza la wadhamini halikuidhinisha mradi husika,halafu itokee ghafla uongozi wa UVCCM makao makuu wanaanza ujenzi.Hapa kungekuwa na tatizo la kimaadili na ingepaswa uchunguzi wa kina ufanyike katika kubaini nani amehusika na maamuzi hayo kinyume cha kanuni na taratibu za UVCCM.
Nimewasikia wajumbe kadhaa wa baraza kuu wakiunga mkono hoja ya bwana Nape. Ni sawa. Lakini nasema hiyo haitoshi kama hawakuweza kuwashawishi wajumbe wengi wa baraza kupinga mradi kwa taratibu za vikao, kwa mujibu wa kanuni.
Kimsingi mimi sipo hapa kujadili kama mradi una manufaa kwa UVCCM ama la.Maana sijausoma mradi husika.Nimesikia kutoka upande mmoja tu, wa Nape. Sasa kwa misingi yangu, ni lazima nipate maelezo ya pande zote husika ndipo nifike mahali nitoe maoni ni nani yuko sahihi juu ya umuhimu na manufaa ya mradi.Ninachojadili ni kama tararibu za kufikia maamuzi ya kuwepo kwa mradi zilifuatwa.
Nadhani nimejibu hoja mkuu. Hatahivyo, nakaribisha maswali zaidi kama yapo.
TATIZO NDANI YA UVCCM NI NCHIMBI: elimu ndogo (kazi kununua digrii za Ph.D wakati ana Diploma tu ya Mzumbe), ushamba (kipofu kaona mwezi!), ufisadi (ni errand boy wa Rostam, Lowassa na Karamagi na usanii wa kuact as if ni msomi kumbe hata kuandika jina lake ni taabu.
Mkuu yawe ya dhati au siyo kwanza hatapita hilo la kwanza tulitambue kabisa kwa sababu amegusa mabapo hapagusiki na tena haparuhusiwi kuguswa.wewe unamchokonoa Lowassa unategemea nini?Vile vile hayo siyo maneno ya kuombea kura.CCM waahidi fedha then watakupa kura.
Unajua mtu hasiye na madhara kwenu hamwezi kila siku kumtajataja na kumfanyia wtat the rubbish you call analysis...pamoja na yote ukweli unabakia palepale kuwa yeye ni kiboko yenu..hatingishiki na wala hapotezi mchezo....kwa mara ya pili tuone game kati ya Nape na Nchimbi,nani zaidi.Kwa uhakika ni kuwa Nape atachakazwa kwa aibu kubwa na pengine atahama mpaka ccm na kuja huko ChademaHongera kwa kutupa correct analysis ya huyo jamaa NCHIMBI ongezea na roho mbaya
Ok Ni Yule Mfanyakazi Wa Bakheresa Ambaye Kubenea Alikuwa Akimchukulia Mkewe.
Moja ya kitu cha msingi MwanaHALISI wanahitaji ni uwakilishi mzuri zaidi wa kisheria. Mwanasheria wake anafanya miscues fulani ambazo zinaweza kuboreshwa zaidi.
Kwa mfano, Kubenea alipohojiwa kuhusu uhalali wa utoaji taarifa za akaunti za watu, aliiambia KLH News kwamba wao hawatoi akaunti za "walima Kahawa wa vijijini," na wa wananchi wa "huko Buhemba" na kwingineko. Ila ni viongozi fulani fulani wa nchi. Sasa, huhitaji kuwa mwanasheria kujua kwamba, kama ni makosa kuvujisha akaunti za benki - assuming ndilo kosa - basi ni wazi kwamba kila mteja mwenye hizi akaunti analindwa na sheria ya nchi, na sio mlima Kahawa tu. Wakili wake hatakiwi kumruhusu atoe justification kama hivi za kujifunga kitanzi.
Mfano mwingine, wakili aliyeitwa kuja eneo la tukio, hakutakiwa kuruhusu isainiwe search warrant inayomtafuta "Msaki and others." Msaki hakuna anae mjua hapo MwanaHALISI. Na hao "others" wanaweza kuwa wako kwenye sayari ya Zebaki (kama ambavyo Kishoka huwa anasema.)
Hizi nadhani ni faux pas zinazoweza kuboreshwa zaidi. Humo ndani pia wawe na watu wanapitia vitu wanavyoandika. Vinginevyo wanaweza kuishia kulipa mapesa kama yale ya Sumaye. Tukikosoa press ya Bongo ni katika kujaribu kuijenga vile vile.