Hawa CCM kweli wanatisha .Nimeona wameamua kujenga jengo jina na wameanzia kitu kinaitwa Videco .CCM kweli ni mali ya wahindi maana hata pesa za usafiri kwa Vijana wa CCM kwenda Dodoma kwenye kuchambua majina ya wagombea pesa zimetolewa na wahindi na huku JK anasema CCM ni ya watanzania .Ama kweli baba ombaombana mtoto the same .Aibu kubwa hii .
angalieni maslahi ya jumiya na chama chetu,
Simply PR gimmicks...
2.Quote: Fisadi Mtoto
unatuletea mpaka taarifa za msafara wa kuzikwa AC...jina lililukwa wewe ndiwe ulijaza hayo majina????falasi.Vita hiyo Nape kamwe haiwezi atachapwa kama amesimama na kama Nchimbi kwela ameamua kula sahani moja na nape nakwambia Nape hana pa kutokea....hatoki maisha yakenasema.niko tayari kuweka dau la milioni 50...mziki wa nchimbi Nape hauwezi....tarehe sita baraza kuu.sikiliza kama Nape hatopewa alama F
Yesterday 09:13 PM
Quote: Kutoka Bungeni
Mgombea wa kiti cha Uenyekiti, Vijana (UVCCM), Nape Nauye, ambaye anaelekea kutokuwa chaguo la uongozi uliopo madarakani aliyeshangiliwa kwa nderemo katika ukumbi wa Bunge, Dodoma Ijumaa.
Tausi Mbowe, Dodoma
Mwananchi
MGOMBEA wa kiti cha Uenyekiti katika Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Nape Nauye, jana alilitikisa Bunge pale alipotambulishwa na kushangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushangiliwa huko kulimfanya Nape, anyanyuke mara tatu kuwashukuru wabunge waliokuwa wakimshangilia kwa kugonga meza zao kama ishara ya kumkubali huku yeye akiwapungia mikono wabunge hao.
Shangwe hizo ziliwafanya wabunge hao kushindwa kuendelea kumsikiliza Spika Samuel Sitta, aliyekuwa akitoa matangazo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu. Hali hiyo ilimlazimisha Spika Sitta, kusubiri Wabunge hao wamalize kumshangilia Nape, ambaye katika siku za hivi karibuni ameingia katika mzozo mkubwa na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM mara tu baada ya kutangaza kuwania nafasi hiyo na kutoa tuhuma zito kwa baadhi ya viongozi wa umoja huo.
Baada ya kuona hali ya mambo imetulia Spika Sitta, alisema Nape, ni mmoja wa vijana machachari aliyeibuka siku za hivi karibuni katika UVCCM.
Sitta alisema anamtakia kila la heri mgombea huyo, katika mambo yake hasa katika kipindi hiki anachoelekea bila kufafanua ni kipindi gani lakini kwa hali ya mambo ilivyo alikuwa akimaanisha mchakato wa uchaguzi wa UVCCM.
"Huyu ni kijana machachari umoja wa vijana wa CCM na nimtakia kila la heri katika mambo yake yajao," alisema Spika na kushangiliwa na wabunge wengi.
Najua siku zote chuki za Field marshal dhidi ya nchimbi lakini hainizuii kuendelea kumwelimisha......record ya nchimbi kwenye uongozi wa nchi yetu....akiwa DC wa bunda alikuta bunda ikiwa na shule za sekondari zipatazo saba tu...lakini kwa kipindi cha mwaka mmoja wa u dc wake aliweza kusimamia ujenzi wa shuile mpya 17 za sekondari..hakuna mkuu wa wilaya alieweza fanya hivyo kwa kipindi chote cha awamu ya tatu ya Mkapa...
With all respect kwa wakuu wote, naomba kuigusa hii topic kidogo, maaan imenigusa sana:-
1. Wa-Tanzania tumefikia mahali ni lazima tukubali kuwa ufisadi ndio siasa ya sasa kwa taifa letu, kwamba pmaoja na matatizo yote tuliyonayo ukweli wa mbali ni kwamba tukiweza kulikabili tatizo la ufisadi, basi mengine yote yaani matatizo tuliyonayo, yatajinyoosha yenyewe, lakini the name of the game ni ufisadi.
2. Sasa kwenye hili la ufisadi, lets be honest with each other, yaani wananchi at large ni lazima tuamue sasa tunataka kuwa upande gani kwa sababu, hakuna neutrality, wala middle position na ufisadi, either you are for it au you are not, either uko with us tunaoupinga au uko na wanaoufanya na wanaoushangilia.
3. Kwenye hili ninaomba kusema wazi kuwa ninatoa heshima nzito na a strong support kwa kiongozi huyu kijana Nape, ninajua for a fact kwamba record yake ni safi haina mikwaruzo, na heshima yangu kwake ilianzia pale ambapo yeye kama mimi pia, tuliitwa na muungwana kwa wakati tofauti wakati wa uchaguzi wa urais uliopita, katika kutaka our support kwa kambi yake, yeye ninajua kuwa alimkatalia kata kata muungwana, kwa sababu nyingi sana lakini ya msingi ilikuwa ni marafiki wengi wa muungwana, hawakuwa safi kushirki nao kwenye coaliton ya kisiasa kwa maneno mengine ni corrupt, kama wote tunavyojua sasa kutokana na ushahidi mbali mbali uliokwisha jitokeza, wazi.
4. Inanisikitisha sana kwamba somehow tumewaachia viongozi wasiofaa kuushika Umoja Wa Vijana ambao one time ulikuwa umeshikiliwa na Mzee Joseph Nyerere ambaye hakuwa na mchezo kabisa katika kufuata haki, sasa huu umoja umekuwa almost wa mtu mmoja, ambaye kwa kuamini kuwa ana ukaribu na the powers wa sasa basi anaweza kufanya atakalo that is pathetic.
Hapa again ninamlaumu Rais wa sasa, kwa sababu haiwezekani kiongozi mmoja wa CCM apewe alama ya E kiuongozi na uongozi huu suspect wa Vijana halafu aende bungeni na kushangiliwa namna hii na viongozi wengine tena wa CCM, something is not right na uongozi wa sasa!
Kwa kumaliza ninasema kuwa kwa wale wapenda mabadiliko kwa taifa letu, huwezi ukasema serikali ya sasa haifai lakini ukampondea huyu kijana Nape, huwezi ukampenda Obama, anayesimamia change, halafu ukamponda Nape ambaye pia anasiamia hiyo hiyo change, ila kwa njia tofauti kuliko ya Obama, hasa kutokana na tofauti ya mazingara ya kisasa ya grounds wanazozisimamia.
Nape, aendelee ksuimama kidete akielewa kuwa mabadiliko ya kisiasa sio kitu rahisi kukubalika, Umoja Wa Vijana yes ni step kubwa sana katika kutafuta nafasi ya kiongozi kuonyesha uwezo wake wa kulilia na kuleta mabadiliko, kwa hiyo Nape apokee kwa heshima kubwa vietndo kama hivi vya kusimamiwa na wabunge karibu wote bungeni kutoa heshima zao kwa ushujaa wake wa kusimama kidete,
Hakuna tatizo la time kwenye kutafuta mabadiliko, kwa hiyo ni sawa kabisa kwa Nape ksuema maneno mazito now kwa sababu politically huu ndio hasa wakati wa kusema na usikike wakati wa kukaribia uchaguzi, kwa sababu huyu mama Pelin huko kwao Alsaka kula Moose ni sawa, lakini sio sasa wakati yeye na Makeni wakigombea urais, sasa ataulizwa kwamba kwa nini unakula yule mnyama, asingekwua mgombea isingekuwa tatizo, ndio siasa inavyochezwa, maswali serious kuhusu nonesense huulizwa wakati wa uchaguzi sio kabla, kwa hiyo Nape hakukosea kuuliza kuhusu majengo sasa, yaani wakati wa uchaguzi kukaribia.
Mkuu Nape, tunakutakia mafanikio katika hivi vita ambavyo wengine tumevulia nguo siku nyingi sana, na sasa tuko kwenye kuvioga, usimame imara bila kuogopa, you have our attention sasa wewe ni kungalia mbele tu, hata ukikosa huu Umoja wa vijana, bado kuna nafsi nyingi sana tena muhimu kuliko hiii, ninasema bravo Nape, na kuna mabao tuko nyuma yako. na heshima kwa wabunge wote waliotoa heshima kwako.
Mingu Aibariki Tanzania.
Huzo shule zote zilikuwa chini ya serikali kuu na zilipata usajili mwaka wa 2005...wananchi wenyewe wa bunda wanajua hilo vizuri sana.shule utendaji wao ni ngumu kuujua kwa kuwa form four wa kwanza wanatoka mwakani...najua imewauma kuona jamaa kumbe ana record bora na ya mfano ambayo imekuja kutumika kwa nchi nzima.na hapo bado.Hivi ni shule za Serikali au za jumuiya na wananchi? Unaweza kutupatia majina ya shule hizo na utendajiufanisi wao tangu zikamilike?
Kama mimi ningekua Nchimbi, ningekuwa shujaa kwa kumpigia debe na hatimaye kuhakikisha Nape anashinda. Siasa ndio zinataka mtu anayeweza kubadilika. Naamini kwa hili Nchimbi atakua ameelea na kuvuka katika hili dhoruba
....Kwamba ni waarabu wa Pemba yakhe??CCM wamesimama kumshangilia CCM mwenzao, kuna ajabu gani?
Kaka mwenye chuki dhidi ya Nchimbi....ulikuwa unampa ruhusa wewe kutokuwa eneo lake la kazi au unajitungia tu wewe..hujui siasa za tanzania ndio maana mambo menginine ya ndani inabidi tuwaaachie walioko nyumbani tz.ili nchimbi aweze kuooperate sio lazima atembee yeye,tayari ana watu kila sehemu ya tanzania....Mkuu vipi ukwieka majina ya hizo shule 17, alizozijenga in one year huku akiwa hayupo kwenye kituo chake cha kazi kwa karibu mwaka mzima akiwa Dar na Mwanza, kutengenza kampeni za urais wa mtandao!
Ilimchukua almost miezi sita ya u-DC kutayarisha yale maandamano yake bubu, yaliyozimwa na uwt akitaka kwenda Ikulu Chamwino kumtishia Mkapa kuwa lazima mtandao ushinde! Mkuu kuwa mkweli useme wazi hapa katika kipindi cha karibu mwaka na nusu ya u-DC wa Nchimbi, alikuwepo physically kule Bunda kwa muda gani?
Eti alijenga shule 17? ziko wapi mkuu hasa hizo shule? Madaraka wamepata matokeo tumeyaona tena wazi, sasa ungetegemea waanze kujiweka pembeni na uongozi baada ya hii aibu ya kujifanya tunataka viongozi vijana, kumbe ni bure ya ghali! Wakajifanya wana hela sana za kampeni kumbe ni kuchota BOT kwa ujanja ujanja, aibuu kubwa sana kwa taifa,
Bravo Nape, kwa kusimama kidete, Tanzania tunahitaji viongozi angalau wanne tu kama Nape, wanaoweza kusimama na ksuema msimamo wao bila kuogopa mtandao wala wanaojikomba kwa hao matandao!
Hapa ni taifa kwanza, na hizo affiliation na wapambe baadaye.