Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Inategemea kitakufanye Mkuu, nchi yetu itayumba sana CCM ikifa kifo cha mende cha ghafla.
Mwandishi mahiri Padri Karugendo alibashiri kuanguka kwa Nape Mnauye mwezi August 08. Alisema katika semina ya kutathini uchaguzi wa 2005 Karugendo alifichua ufisadi wa CCM yeye akiwa kama mmoja wa waagalizi wa uchaguzi huo. Nape alipinga na kumtukana Karugendo kwa kuichafua CCM. Wakati wa mapunziko Karugenmdo alimwita Nape na kuongea naye kwa kina bila mafanikio.Kwenye biblia inasimulia jinsi Saulo aliyekuwa muovu aliokoka akiwa njiani kwenda Damascus na kuwa Paulo ambaye alikuwa muhubiri mahili wa injili. Lakini Mt. Paulo aliteswa sana na mafarisayo. Tumfananishe Nape na Saulo amabaye alibadilika kuwa Paulo hivyo ategemee shuluba ndani ya CCM. Na ndivyo imekuwa! Je, Nape atarudi nyuma? Saulo hakurudi nyuma.
Mkuu Yebo yebo,
Ikiwa inakufa bado tutakua na muda wa kutosha kujipanga
Mkuu asante sana, siasa za bongo wazijua nimekuvulia kofia...endelea kutuhabarisha...maisha ya dogo Nape yako hatarini kila anayegombana na Nchimbi mauti humkumba....natamani kutuma rambi rambi kwa familia ya Nape
A what cost?
... hivi ni kweli amavuliwa uanachama au atachukuliwa hatua zingine tu za kinidhamu kwa ajili kutoa siri za chama kwenye vikao ambavyo sio rasmi.
Kama ni kweli basi wamemuonea kijana wa watu. Kwa nini wasimuenzi hata baba yake
Mkuu,walinena,Tukanena na bado tutanena lakini unabii unakaribia.Kwa hali inayoendelea,ipo siku mioyo ya Watanzania iliyojaa visasi na uchungu wataamua kuonyesha kwa vitendo.Nchimbi ana dhamira zake na kwa bahati mbaya sana anadhani amefanikiwa katika dhamira alizojiwekea, na hii yote ni kwa sababu yote anayoyaona yakitokea hayaangilii kwa umakini anaamini ana waungaji mkono wengi katika dhamira zake na kutoutambua ukweli huu inatokana na kuwaangalia watu waliomzunguka kwa macho ya kilevi. Anadhi waungaji mkono wake ni wengi.maskini hafahamu kuwa idadi aipatayo imezindishwa na macho yake ya kilevi kwa "pombe alizokunywa".
Sasa hivi ni Naibu waziri wa ulinzi anaongea maneno ambayo hajui athari zake kwa nafasi na dhamana aliyonayo, anakwenda mbali zaidi na kudiriki kutukana watu wanaoweza kutambua na kulalamikia dhurma katika jamii kuwa ni wendawazimu.
Anaongea kama mtawala mkuu katika nchi itayoendeshwa na utawala wa Ki-dictator.
Nchimbi napenda kutumia fursa hii kukukumbusha kuwa ni afadhali kama ungepewa wizara ya mambo ya ndani ya nchi...ungeweza kuwatumia Polisi utakavyo na wao wangekulinda kwa sababu Polisi ni jeshi la serikali na wapo kwa ajili ya viongozi wa serikali na masuala ya raia kwao ni secondary issue, lakini huko ulipo ni jeshi la wananchi na wapo kwa ajili ya wananchi na si watu wenye ndoto za aina yako hapo ndiyo mwisho wako unajiandika...jaribu kuangali mfumo na utendaji wa taasisi hiyo unayoiongoza utajua nina maanisha nini.
Aliyekuweka hapo ni kwasababu hakupendi usijidanganye na kufikiri kuwa wewe ni the most favored desciple"Peter/Petro", ninafahamu kuwa mwisho wetu sote ni mmoja lakini wako hautakuwa na kificho wala utata na kwa wengi itakuwa ni uhuru kamili, hakuna mtu anaetaka kuandika historia kupitia wewe lah..! isipokuwa historia imeamua kujidhihirisha na yenyewe ndiyo itachagua wa kuiweka...mikono yako imejaa hatia, na kwa jinsi ulivyolewa na kupofuka hutapata nafasi ya kutubu dhambi zako, wachache wakuzungukao, ni walewale wamtumikiao kafiri wapate chao.
Haiwezekani mtu ukosoe chama kwa maslahi ya chama uitwe mwendawazimu, hayao ni matusi ya dhahiri, inaonekana hata elimu uliyoipata(INGAWA NA WASIWASI NA VYETI VYAKO )ilikuharibu akili badala ya kukujenga, ndiyo tunao wasomi wa aina yako wengi tu...hata wewe ni shahidi.
Kwa hiyo kwa kufuata kanuni mpo tayari kumuweka bata na mbuzi watuongoze kuliko watu wenye sifa na mawazo ya kimapinduzi sivyo? Ninyi si ni Chama Cha MAPINDUZI..? Vp muogope mawazo ya kimapinduzi na kuchagua kuishi katika kivuli cha HOFU na UFISADI,
Haya na tuendelee kusubiri na muda si mwingi maoni haya yangu yatakapotafutwa na kusomwa tena na tena na kuchukuliwa na kuhusishwa na tukio kwa namna moja au nyingine
CCM sio wote mafisadi bali wameelemewa na mafisadi.
Kila wakati mimi nasema kwamba kama wapinzani wakichukua ikulu basi yale matunda yaliyooza kwenye CCM yote yataondolewa ili yasiambukize wenzao
Na hapo ndio CCM itabakia na watu wazuri.
Mpaka sasa sina msimamo wowote wa chama lakini bila CCM kuondolewa hatutafika popote.
Nao hawakusita kuchukua maamuzi magumu na mazito
Inaonekana Nape alikua anatoboa siri za chama-teh teh teh.
yawezekana nape alikua anawafitinisha viongozi wa chama teh teh teh.
Ama naye CHIMBI alisimama ktk kikao na kunena.
Hayuko tayari kumwachia uenyikiti NAPE ama yeye avuliwe uanachama ama yeye Nchimbi abwage manyanga teh teh teh teh.
kazi kweli kweli
Nape alikuwa sahihi ila timing ilikuwa mbaya. Angengoja wampitishe kwanza!
Tatizo la viongozi wetu bongo kukosa washauri wa kisiasa.
mkuu,walinena,tukanena na bado tutanena lakini unabii unakaribia.kwa hali inayoendelea,ipo siku mioyo ya watanzania iliyojaa visasi na uchungu wataamua kuonyesha kwa vitendo.hakuna damu imwagikayo ambayo haijahesabiwa kwani hata nywele za kichani ambazo hazi-sense nazo zimehesabiwa.
Matusi hayo si kwa nape pekee,yameelekezwa hata kwa wanapinduzi wote wanaosimamia mageuzi.ni matusi mazito kwa wapambe wa demokrasia ndani ya taifa hili.ipo siku nchimbi atawajibu watanzania kwa kuwaomba msamaha.najua hatasubiria hata tume kama ile ya mandela kule south africa ya maridhiano.kiburi cha leo,kina kikomo kesho
Mkisikia kulikologa ndo hili uongozi wa MAKAMBA,NCHIMBI na BABU KINGU ni wa kukalili.....wamechemka sana eti wao wasiulizwe na vijana kwa vile ni wazee.....duh hii kali JK kama unajua hawa watu ndio wanao kuvulugia mipango yako na kukuzunguka.
Hapo sasa Nape ndo mnampa umaarufu wa hali ya juu sasa atauzika jimbo lolote akitaka kugombea ubunge huyu kijana.
Mzee Kawawa ana mwanae kwenye hicho kinyanganyiro cha Uenyekiti wa UVCCM...hivyo namuona Mzee Kingunge anampa Mzee mwenzie "Support" Makamba ni Katibu Mkuu hana jinsi iwapo Mwenyekiti wa UVCCM akishirikiana na Mzee Kawawa na Ngombale wametaka iwe hivyo.
Mtihani hapo ni wa JK, hawa wazee wamemuweka mtegoni.
Hizi comflict of interest sijui dawa yake ni nini.kuna watu wameshajiamulia kwamba ni wao na wano na wajukuu zao tu wenye hati miliki ya mamlaka katika Taifa hili.
Vijana vyenyewe vijinga. Kwa nini vikubali vibabu, Mwiru, Kawawa, na Makamba, vije kuingilia uchaguzi wao?