inaonekana global publisher wamejiunga na harakati za makusudi zinatumika ili kummaliza nape kisiasa. ama kweli mfa maji atashika hata jani akiamini ataelea. hbeu soma hapa chini.
Kigogo wa CCM apata skendo akiwa kaburini
risasi mchanganyiko
Kigogo wa CCM apata skendo akiwa kaburini
Watoto anaodaiwa kuzaa Brigedia Jenerali huyo mstaafu, nje ya ndoa ni mwanasiasa chipukizi ambaye hivi sasa amekuwa gumzo kubwa, Nape Nnauye na Zuhura Nnauye.
Habari za kiuchuguzi zinasema kuwa, huku akijua kuwa alikuwa ndani ya ndoa na mama Mwanaisha Nnauye, waliyekuwa wakipendana kupita maelezo, Mzee Nnauye alijiweka kwa kinadada wengine na kujikuta akipata watoto wawili kidume Nape na dada yake aitwaye Zuhura Nnauye.
Hii ni skendo kwa kigogo huyo wa CCM ambayo ameipata akiwa kaburini, alisema mmoja wa wananchi walioongea na mwandishi wetu mara baada ya sakata la Nape ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM kuibuka na kutawala kurasa za mbele za vyombo vya habari.
Ingawa kuwa au kutokuwa na wanawake na watoto zaidi ya wanaofahamika sio kipimo cha uongozi nchini, watu waliohojiwa na gazeti hili wamedai kuwa, kitendo cha marehemu Nnauye kuzaa na mwanamke mwingine bila kumfahamisha mkewe ni kudhihirisha kuwa naye alikuwa hajambo kwa dogodogo.
Kwa skendo hii iliyoibuka miaka saba baada ya kifo chake, Mzee Nnauye ambaye wakati anakufa alikuwa mshauri wa Rais anayeshughulikia siasa, anakuwa mwanasiasa mkongwe wa kwanza nchini kukumbwa na skendo la aina hiyo wakati akiwa tayari amekufa.
Hata hivyo, kubumbuluka kwa maisha yake ya siri ya kuzaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa bila kumshirikisha mkewe, kunatokana na Nape kushupalia suala la mkataba wa mradi wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM kuwa haukupitishwa na vikao halali, hivyo kuvuta hisia za watu na kujikuta wakitaka kumfahamu vizuri kijana huyo.
Suala la Nape kuwa mtoto au si mtoto wa Nnauye limezua mtafaruku mkubwa baada ya mjane wa marehemu kumkana kuwa si mwana wa mzee Nnauye wakati kaka wa marehemu ambaye ni msimamizi wa mirathi na msemaji wa familia hiyo, Gallus Abeid amethibitisha kuwa, kijana huyo ni familia ya kiongozi huyo aliyefariki dunia.
Pamoja na Nape na dada yake Zuhura, watoto wengine wa marehemu Nnauye ni Mariam, Joseph, Mwate, Samora na Mussa.
Nape amekuwa gumzo hivi karibuni kutokana na kuibua suala la utata wa mkataba wa Jengo la Umoja wa Vijana wa CCM hivi karibuni ambapo alidai kuwa ulipitishwa kienyeji, bila kuridhiwa na vikao halali vya jumuiya hiyo ya Chama cha Mapinduzi.
Kufuatia kauli hiyo ya Nape, Baraza Kuu la Umoja huo liliamua kumvua uanachama ikiwa ni pamoja na kumvua nyadhifa zote alizokuwa nazo kupitia umoja huo kwa madai kuwa alisema uongo nje ya vikao.
Hata hivyo, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Jumatano wiki hii ilitengua uamuzi huo wa Baraza la Umoja wa Vijana wa kumvua Nape uanachama wa umoja huo.
Mzee Moses Nnauye alifariki katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam saa 3.00 asubuhi, Desemba 6, 2001 kufuatia maradhi ya moyo na kuzikwa Desemba 7 katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Hadi kifo chake, mzee Nnauye alikuwa na umri wa miaka 64, baada ya kuzaliwa mwaka 1937 katika Kijiji cha Chiuta, Tarafa ya Nyangamala, Wilaya ya Lindi Vijijini, mkoani Lindi.
Mbali ya kuwa Brigedia Jenerali Mstaafu ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, marehemu aliwahi pia kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Mapinduzi na serikali ikiwemo ya Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
source:
Global Publishers - Tanzania Newspapers