Sakata la Rio Ferdinand lafika kwa Watangazaji wa Kenya "Tatizo la Watanzania wanaandamana kiroho"

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Wakuu

Naona hawa watangazaji wa Kenya wanaendelea kupeleka moto

Mtangazaji wa Radio 47, Mbaruk Mwalimu, amezua mjadala mzito baada ya kutoa kauli za kejeli dhidi ya Watanzania, akidai kuwa nchi hiyo bado iko nyuma kifikra na kisiasa ikilinganishwa na Kenya.

Katika kipindi cha Maskani 47, Mbaruk amechambua ujio wa mchezaji wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand nchini Tanzania, akisema kuwa ni mbinu ya kisiasa inayotumiwa na viongozi kuwazuzua wananchi na kuwasahaulisha matatizo yao ya msingi.

"Nasemaje, umeenda mbali kwa Samia, umeenda mbali kwa Abdul. Hii ni kazi ya Waziri, Paul Makonda... basi. Sasa mbona analeta mchezaji na haleti Arena? Hamna Arena? Wanajua! Mbona wamejitokeza? Tatizo la Watanzania wanaandamana kiroho. Wao wakikosewa wanakasirika kiroho kwamba 'haki yetu, haki yetu' ndani kwa ndani. Waumia, hawana! Watapasuka, watalipuka. Watalipuka! Hawana kidari, hawana kifua Watanzania ya kupigania na kupambania haki zao za kimsingi"

Your browser is not able to display this video.
 
Jamaa mboni yupo sahihi?tuukubali ukweli.

Kipi alichosingizia hapo?nchi ndani ya week tatu mafuta yamepanda mara tatu lakini kimyaa kama hamna kilichotokea.
 
 
And guess what? These Kenyans are 100% right!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…