Sakata la TFF: Leodgard Tenga yuko sahihi lakini Wambura anajikongoja...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Katika mahujiano ya jana kwenye Radio One kipindi cha michezo usiku khoja za Wambura zilirejewa na kuungwa mkono na baadhi ya watangazaji na wasikilizaji wakati ni hoja zinazokinzana na sheria za FIFA
!

Mgogoro wa uongozi ndani ya TFF unahusu sifa za baadhi ya wagombea akiwemo Wambura ambaye amekuwa akienguliwa kila mara kwa sababu zilezile na hivyo kimsingi kuwa ameonewa. Huwezi kumwadhibu mtu mara mbili kwa kosa lilelile kwa kufanya hivyo ni kuwa hujamsamehe na adhabu yenyewe inaonekana haina mipaka na hivyo kutokubalika. TFF inabidi watafute sababu nyingine mbali ya zile ambazo wamekuwa wakizitumia kumzuia Wambura kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Kuhusu Malinzi kuzuia ni kichekesho kabisa kwa sababu uongozi ndani ya mpira ni madraka tu au hata ushiriki pia? Hivi mchezaji wa mpira hawezi kugombea wadhifa ndani ya TFF mpaka kwanza aliwahi kuwa na wadhifa kwenye kilabu kama siyo uendawazimu hivi ni nini?

Zipo sababu za kimsingi za kuhoji maamuzi ya TFF na hata taratibu zao za kukata rufani kama kweli zimezingatia haki za ubinadamu na hayo ni maeneo ambayo kamati ya FIFA itakapokuja inafaa kuyanyoosha.

Wambura na wenzie wanakosea kudai ya kuwa serikali ina ubavu ndani ya TFFhiyo mitazamo inampunguzia sifa ya kulisimamia kabumbu letu. Sheria za FIFA ziko wazi kwenye hilo na hata hivi sasa FIFA imewaandikia DRC kuwa waache kuingilia utawala wa chama cha mpia cha kwao au hata maombi yao ya kuchezesha soka mwaka 2014 huenda yasifikiriwe kama hawatajirekebisha. Barua hiyo kaandikiwa waziri mkuu wao kujibu maombi tajwa.

Kwenye suala la uhuru wa vyama vya mpira kujiendesha FIFA haina cha ubabaishaji hapo ila kusimamia kabisa sasa huyu Wambura anafikiri sisi hatujui hilo?

Wambura pia anatupotosha sana pale anaposema Tenga muda wake umekwisha na kwa hiyo hana mamlaka ya kisheria ya kusimamia uchaguzi ujao. Hivi haya ameyatoa wapi? Na hili anafikia mahali anajichanganya kwa Wambura kudai Tenga atakeleze maamuzi ya serikali sasa atayatekelezaje kama yeye hana nguvu ya kisheria kuusimamia uchaguzi husika?

Nionavyo Wambura khoja zake ni zenye kukithiri na ubinafsi sana na lolote lile litakafanikisha azma yake ya kutwaa uongozi ndani ya TFF atalikumbatia na anonekana anaichukulia TFF kama sehemu ya ajira hivi wakati ni kujitolea tu.

Tenga yuko sahihi kupinga serikali kujiingiza katika uendeshaji wa TFF na huo ndiyo msimamo wa FIFA na Wambura aache kuwapotosha wadau wa soka.

Jingine ni kuwa baadhi ya waathirika wa maamuzi ya TFF wamekimbilia mahakamani kwa kutumia vikaragosi wao ili kushinikiza kupata ugali wao. Hawa wachunguzwe na ushahidi ukipatikana wazuiwe kugombea nafasi zozote zile ndani ya TFF kwa sababu nilizozitaja awali.

Vilevile, mahakama zetu ni pofu yawaje zikaribishe migogoro ya TFF wakati kanuni zake za uendeshaji zinakataza migogoro yake kutatuliwa na mahakama kulingana na maelekezo ya FIFA?

Kuhusu marekebisho ya katiba ya TFF ya mwaka 2006 ni dhahiri serikali inajikaanga kwneye mafuta yake yenyewe kwa sababu markebisho tajwa yawe mazuri au la serikali iliyasajali na kuwa sheria sasa yawaje leo iyafute kama siyo kuingilia utendaji ndani ya TFF. Mamlaka ya serikali kufuta sheria halali za TFF inayatoa wapi kama siyo kujaribu kuwatungia sheria zake yenyewe?
 
Tatizo ni dogo sana hapo, Serikali haijafuta katiba, katiba haipo maana kama utaratibu haukufuatwa inakuwaje iitwe katiba? TFF waitishe mkutano wapitishe katiba kama utaratibu unavyosema, maana TFF wenyewe wamekiuka katiba yao inayosema marekebisho yatafanyika kwenye MKUTANO MKUU sio kwa njia wa waraka....Tenga hawezi kulikwepa hili apambane nalo mapema iwezekanavyo uitishwe mkutano wa kurebisha katiba
 
Rutashubanyuma, kwanza nikubaliane nawe kwamba kuna baadhi ya maeneo Michael Wambura anajikongoja hana hoja za msingi.
Lakini pili nisikubaliane na wewe kabisa juu ya uendeshaji wa TFF, kwakuwa unatoa hoja potofu nadhani kwa kutojua hata kanuni za FIFA zinasemaje kuhusu uingiliaji wa serikali katika kuendesha/kuongoza chama cha mpira katika nchi husika.

Kadri ninavyofahamu FIFA wanaheshimu katiba za nchi na wanahimiza vyama vya soka vya nchi husika kuheshimu na kufuata sheria na katiba za nchi zao. Pale ambapo serikali inaingilia utendaji/uendeshaji wa chama cha mpira cha nchi ndipo FIFA wanaingilia.

Kwa hili la TFF kwanza utambue kwamba TFF wameivunja katiba yao wenyewe kwa kufanya marekebisho/mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012 kinyume na matakwa ya katiba yao wenyewe. Katiba inatamka kwamba wenye mamlaka ya kufanya marekebisho ya katiba ni "general assembly", kwa lugha nyepesi kabisa assembly inakuwepo pale ambapo watu wanakutana na si kwa njia ya kuandikiana waraka, kama ulimsikia mwanasheria mmoja akihojiwa redio one utakuwa ulipata ufafanuzi wa kina sana juu ya tafsiri sahihi ya general assembly na jinsi TFF chini ya Tenga walivyoibananga katiba yao. Tenga mwenyewe alibanwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akakimbilia kujitetea kuwa kulikuwa na makosa ya uchapaji wa katiba kwamba badala ya kutumia maneno at the general assembly ilitakiwa kuwa by the general assembly. Akasahau kuwa hata kama ilikuwa ni makosa ya uchapaji kwakuwa katiba hiyo imeshasajiliwa basi maana inabakia kuwa at the general assembly hadi hapo yatakapofanyika marekebisho mengine kwa mujibu wa maelekezo ya katiba.

Jambo lingine nataka nikufahamishe ni kwamba mgogoro uliopo si kuhusiana na sifa za wagombea wa uongozi Wambura na Malinzi bali ni namna kamati ya rufaa ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Iddi Mtiginjola ilivyokiuka kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi katika kuwaengua baadhi ya wagombea, mathalani kamati hiyo kumuengua malinzi kwa kisingizio kwamba hana uzoefu wa kuongoza mpira kwa miaka mitano kwa sisi wafuatiliaji wa masuala ya michezo hapa nchini kilichofanyika ni uamuzi wa kiuwendawazimu kabisa, Jamal Malinzi amekuwa kiongozi wa mpira katika nyadhifa mbalimbali tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000s, amekuwa katibu mkuu wa klabu ya Yanga kwa miaka kadhaa, amekuwa kiongozi mkoani Dar es salaaam, amekuwa kiongozi wilayani missenyi na sasa ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera.

Hoja ya pili ya kumuengua kwamba alipingana na waraka wa TFF nayo ni hoja ya kipumbavu kwakuwa yeye kama raia wa nchi hii anayo haki na uhuru wa kutoa maoni yake juu ya mambo fulani yanayofanywa na mtu yeyote ama taasisi yoyote. Hata hivyo iko bayana kwamba alipinga maamuzi ya kubadilisha katiba ya TFF kwa kutumia waraka ambao ni kinyume na katiba ya TFF, na hivyo kimsingi alikuwa anaitetea katiba ya TFF isivunjwe.

Jambo la mwisho na la muhimu, TFF kama vyama vingine vya michezo imeanzishwa na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na utaratibu wa kuifanyia marekebisho katiba yake lazima uzingatie sheria na kanuni za uendeshaji michezo na vyama vya michezo hapa nchini, na ndio sababu katiba yao imesajiliwa na serikali na haiwezi kuwa na uhalali wa kutumika ikiwa haijasajiliwa na msajili. Kama imethibitika kwamba utaratibu marekebisho ya katiba yao haukuzingatia katiba yao wenyewe na haukuzingatia kanuni za usajili wa katiba uliowekwa na serikali basi serikali inao wajibu wa kusimamia kuhakikisha kwamba taratibu na kanuni zinazingatiwa katika mabadiliko hayo, na serikali haijaiingilia TFF bali imeikumbusha umuhimu wa kufuata kanuni na sheria za nchi katika kuiendesha TFF kwakuwa hicho ni chombo kilichokasimiwa kusimamia na kuendesha mpira kwa niaba ya watanzania na kwa niaba ya watanzania wote.

Viongozi/watu wachache hawawezi kuigeuza TFF kuwa kijiwe chao cha kujiendeshea maisha bila kuzingatia sheria za nchi eti serikali ikae kimya kwa kuihofia FIFA. Lazima serikali iiambie TFF kufuata katiba yake ili kuepusha migogoro inayokinyemelea, na nina uhakika hata FIFA wakisikia kwamba mgogoro uliokuwepo unatokana na viongozi wake kukiuka katiba yao hawataweza kukubaliana nao bali watawashauri wazingatie katiba na si vinginevyo.

Kwakumalizia nikukumbushe kuwa kila mwananchi wa nchi hii anayo haki ya kufungua shauri mahakamani pale anapoona haki yake ama haki/maslahi ya umma yanahatarishwa, na kwahiyo mahakama haiwezi kukataa kupokea kusajili kesi yeyote kwakuwa katiba ya TFF hairuhusu, kitakachotokea ni baada ya mahakama kupokea shauri hilo na kulisikiliza ndipo itaamua kulifuta ama kuendelea kutokana na ushahidi na utetezi utakaotolewa mahakamani, kwahiyo ni vizuri ukafahamu na kutambua nguvu na mamlaka ya mahakama badala ya kuandika mambo ya jumla jumla bila kuzingatia muktadha husika.
 
Last edited by a moderator:
Mimi huyu Wambura niko na wasi wasi nae maana ni mda mrefu kinganganizi ni kweli ana maono ya kuinua soka au maonmo ya kujiinua yeye na familia yake!
 
Haya yote tunaongea, tunajua kuwa tuna mechi muhimu sana ya Kombe la Dunia mwezi huu dhidi ya Morocco? Vipaumbele vyetu sisi Watanzania ni nini hasa?
 
mkuu vipaombele vyetu sisi kama watanzania ni kila mtu awe mwanasiasa na kila mtu akumbukwe katika historia ya nchi hii.
 
Haya yote tunaongea, tunajua kuwa tuna mechi muhimu sana ya Kombe la Dunia mwezi huu dhidi ya Morocco? Vipaumbele vyetu sisi Watanzania ni nini hasa?
vipaumbele vyetu mkuu ni mapato ya viingilio mlangoni ndio tunayatolea macho sana..:A S 39:
 
Rutashubanyuma, kwanza nikubaliane nawe kwamba kuna baadhi ya maeneo Michael Wambura anajikongoja hana hoja za msingi.
Lakini pili nisikubaliane na wewe kabisa juu ya uendeshaji wa TFF, kwakuwa unatoa hoja potofu nadhani kwa kutojua hata kanuni za FIFA zinasemaje kuhusu uingiliaji wa serikali katika kuendesha/kuongoza chama cha mpira katika nchi husika.

Kadri ninavyofahamu FIFA wanaheshimu katiba za nchi na wanahimiza vyama vya soka vya nchi husika kuheshimu na kufuata sheria na katiba za nchi zao. Pale ambapo serikali inaingilia utendaji/uendeshaji wa chama cha mpira cha nchi ndipo FIFA wanaingilia.

Kwa hili la TFF kwanza utambue kwamba TFF wameivunja katiba yao wenyewe kwa kufanya marekebisho/mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012 kinyume na matakwa ya katiba yao wenyewe. Katiba inatamka kwamba wenye mamlaka ya kufanya marekebisho ya katiba ni "general assembly", kwa lugha nyepesi kabisa assembly inakuwepo pale ambapo watu wanakutana na si kwa njia ya kuandikiana waraka, kama ulimsikia mwanasheria mmoja akihojiwa redio one utakuwa ulipata ufafanuzi wa kina sana juu ya tafsiri sahihi ya general assembly na jinsi TFF chini ya Tenga walivyoibananga katiba yao. Tenga mwenyewe alibanwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akakimbilia kujitetea kuwa kulikuwa na makosa ya uchapaji wa katiba kwamba badala ya kutumia maneno at the general assembly ilitakiwa kuwa by the general assembly. Akasahau kuwa hata kama ilikuwa ni makosa ya uchapaji kwakuwa katiba hiyo imeshasajiliwa basi maana inabakia kuwa at the general assembly hadi hapo yatakapofanyika marekebisho mengine kwa mujibu wa maelekezo ya katiba.

Jambo lingine nataka nikufahamishe ni kwamba mgogoro uliopo si kuhusiana na sifa za wagombea wa uongozi Wambura na Malinzi bali ni namna kamati ya rufaa ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake Iddi Mtiginjola ilivyokiuka kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi katika kuwaengua baadhi ya wagombea, mathalani kamati hiyo kumuengua malinzi kwa kisingizio kwamba hana uzoefu wa kuongoza mpira kwa miaka mitano kwa sisi wafuatiliaji wa masuala ya michezo hapa nchini kilichofanyika ni uamuzi wa kiuwendawazimu kabisa, Jamal Malinzi amekuwa kiongozi wa mpira katika nyadhifa mbalimbali tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000s, amekuwa katibu mkuu wa klabu ya Yanga kwa miaka kadhaa, amekuwa kiongozi mkoani Dar es salaaam, amekuwa kiongozi wilayani missenyi na sasa ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera.

Hoja ya pili ya kumuengua kwamba alipingana na waraka wa TFF nayo ni hoja ya kipumbavu kwakuwa yeye kama raia wa nchi hii anayo haki na uhuru wa kutoa maoni yake juu ya mambo fulani yanayofanywa na mtu yeyote ama taasisi yoyote. Hata hivyo iko bayana kwamba alipinga maamuzi ya kubadilisha katiba ya TFF kwa kutumia waraka ambao ni kinyume na katiba ya TFF, na hivyo kimsingi alikuwa anaitetea katiba ya TFF isivunjwe.

Jambo la mwisho na la muhimu, TFF kama vyama vingine vya michezo imeanzishwa na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na utaratibu wa kuifanyia marekebisho katiba yake lazima uzingatie sheria na kanuni za uendeshaji michezo na vyama vya michezo hapa nchini, na ndio sababu katiba yao imesajiliwa na serikali na haiwezi kuwa na uhalali wa kutumika ikiwa haijasajiliwa na msajili. Kama imethibitika kwamba utaratibu marekebisho ya katiba yao haukuzingatia katiba yao wenyewe na haukuzingatia kanuni za usajili wa katiba uliowekwa na serikali basi serikali inao wajibu wa kusimamia kuhakikisha kwamba taratibu na kanuni zinazingatiwa katika mabadiliko hayo, na serikali haijaiingilia TFF bali imeikumbusha umuhimu wa kufuata kanuni na sheria za nchi katika kuiendesha TFF kwakuwa hicho ni chombo kilichokasimiwa kusimamia na kuendesha mpira kwa niaba ya watanzania na kwa niaba ya watanzania wote.

Viongozi/watu wachache hawawezi kuigeuza TFF kuwa kijiwe chao cha kujiendeshea maisha bila kuzingatia sheria za nchi eti serikali ikae kimya kwa kuihofia FIFA. Lazima serikali iiambie TFF kufuata katiba yake ili kuepusha migogoro inayokinyemelea, na nina uhakika hata FIFA wakisikia kwamba mgogoro uliokuwepo unatokana na viongozi wake kukiuka katiba yao hawataweza kukubaliana nao bali watawashauri wazingatie katiba na si vinginevyo.

Kwakumalizia nikukumbushe kuwa kila mwananchi wa nchi hii anayo haki ya kufungua shauri mahakamani pale anapoona haki yake ama haki/maslahi ya umma yanahatarishwa, na kwahiyo mahakama haiwezi kukataa kupokea kusajili kesi yeyote kwakuwa katiba ya TFF hairuhusu, kitakachotokea ni baada ya mahakama kupokea shauri hilo na kulisikiliza ndipo itaamua kulifuta ama kuendelea kutokana na ushahidi na utetezi utakaotolewa mahakamani, kwahiyo ni vizuri ukafahamu na kutambua nguvu na mamlaka ya mahakama badala ya kuandika mambo ya jumla jumla bila kuzingatia muktadha husika.

Mwita Maranya kubwa hapo ni tafsiri ya katiba ya TFF. Iko tafsiri yako na ya wa kwao.............
 
Back
Top Bottom