Sakata la Wabunge 19 viti maalum ni Drama

Sakata la Wabunge 19 viti maalum ni Drama

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
DRAMA linaanza hivi;

Ndugu wana bodi JF, ikumbukwe kuwa mara baada ya uchaguzi 2020, CHADEMA hawakuridhishwa na mwenendo wa mchakato mzima wa uchaguzi na walitoa msimamo wao wa kutokuyatambua matokeo ya uchaguzi ule, hii ilipelekea kutoa tamko hadharani na kuwaagiza wale waliokuwa wameshinda katika ngazi ya udiwani na ubunge kupitia chama hicho kutoenda kuapishwa Kama sehem ya kuuenzi msimamo wao.

Lakin katika hili kuna ukwel upi utakaozidi kile wahenga walichonena "Bahati ya mwenzio, usiilalie Mlango wazi"? Hapa pakatokea Vuta nikuvute, washindi hao wakaonekana kana kwamba wanakaidi msimamo wa chama, lakini chama husika hakikutilia maanani Sana suala hili.

Huku wakiusahau msemo ule usemao "samaki mmoja akioza, basi uozo wa tenga u amekaribia" kwa hyo muondoe samaki mmoja alieoza ili asieneze uozo katika wengine wazima THE BIG MISTAKE'.

DRAMA inaendelea:

CHADEMA waliendelea na msimamo wao huku wakijimwambafai katika vyombo vya habari na kutilia maanani katika msimamo wao ya kuwa hawatoweza kupeleka majina ya wabunge 19 viti maalum ili kuuenzi msimamo wao na kutofungamana na kile wao walichokiita udhalimu.

Wakati huo huo, wakati ambapo jogoo hajawika mara tatu kama ilivyokuwa kwa Petro, ndipo tukahabarishwa ya kuwa wabunge 19 viti maalum wako tayari kuapishwa akiwemo aliyekuwa mfungwa wa siasa ambaye alitolewa gerezan usiku huku yeye mwenyewe akistaajabu mbona hajaimba Kama ilivyokua kwa Paulo na Silas, lakini milango ya gereza imejifungua yenyewe? Zaidi milango ile ilikua na marashi ya noti yaan kutoka ufungwani mpaka Bungeni!

( Hapa ndipo utakumbuka lile lililofanywa na Yuda, mbele ya vipande vya Fedha, ni Bora Yesu aende Msalabani akisindikizwa na bakora za kutosha).

Part 2 drama itaendelea soon.

Ila umejifunza nini?
 
Back
Top Bottom