Sakata la Wamachinga: Suluhisho pekee ni Serikali kuhimiza wananchi kufanya biashara rasmi kwa mujibu wa sheria na kusimamia maslahi ya pande zote

Tatizo la uwepo wa wamachinga sio kukosa maeneo rasmi ya kuuzia bidhaa zao, tatizo ni asili ya biashara ya umachinga.

Biashara ya umachinga inataka kuzurula, kusongamana, holela na kufanyika maeneo ya njia kuu zenye kupitiwa na watu wengi.

Kuna sehemu nyingi kuna masoko mazuri lakini utashangaa wafanyabiashara wengi (wamachinga!) wamejazana nje ya soko na ndani hakuna wauzaji.

Mmachinga ni sawa sawa na kuku wa kienyeji, anaishi vizuri kwa kuachiwa azurure.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wanaambiwa wawapanhe wamachinga..hv kwa hii Dar wamachinga wapo Zaidi ya milioni mbili watawapanga wapi?
 
Uongozi mzuri ni maamuzi magumu bila kusitasita.
Ni kweli kabisa mkuu; kiongozi mzuri ni yule anayefanya maamuzi magumu yenye tija kwa taifa la kesho. Kuendelea kuwabembeleza machinga kwa sababu za kisiasa ni mwanzo wa kuendelea kudidimkza uchumi. Ni vema yakafanyika maamuzi yatakayoleta tija ya kudumu. Umachinga ni kirusi.
 
Vitambulisho vya wamachinga vilishazikwa .
Kitambulisho siyo suluhu ya kudumu; ni suluhu ya muda mfupi.

Haikuwa mbaya lakini bado inaonekana haina tija ya kudumu


Suluhu ya kudumu ni kufanya b8ashara rasmi kwa kuzingatia sheria za kufanya biashara
 
Huu umeme na mabarabara wamevikuta mjini hata hawajui madhara ya kuwa barabarani na chini ya transformer hivyo waliopewa mamlaka ya kusimamia matunzo ya hivyo vitu ndo wawajibishwe.
Hatari sana.
 
Kitendo cha wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza kuwavunjia miundo mbinu ya biashara ndogo ndogo na kusababisha baadhi bidhaa zao kuporwa. Serikali imevunja sheria ndogo za wafanyabiashara wadogo ya mwaka 2018 sura 288 na waliohusika kuna siku watawajibika kusababisha hasara hizo.

Mtindo wa kuthamini kupendezesha vitu na kutweza utu na haki za wafanyabiashara wadogo haukubaliki kisheria, kikanuni, kiutaratibu, kiutamaduni, kijamii, kiusalama na kimantiki hivyo wasababishaji wa hasara, usumbufu na uonevu ni sharti wawajibishwe
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…