Tetesi: Sakata la Zanzibar lawagawa CCM, watendaji serikalini

Vunja Muungano....ndoa yenye kiapo cha Mungu inavunjika itakuwa muungano wa akili za binadamu...koti limebana livue
 
 
Hawa wenzetu maslahi yao mbele ya nchi nyuma wanasahau hesabu ya pumzi uliyoibakiza kwenye ulimwengu anayo mwenyezi mungu

Haya sasa Huyo six kwa kuhofia mamlaka ya uraisi na labda alidhani atakuja kuwa rais akaleta makando kando yake wee Leo yuko wapi? ni ushauri wangu kwa wazanzibar wachukue talaka yao fasta

Migogoro iliyopo Zanzibar toka Uhuru inasababishwa na bara toka kuifuta historia ya kweli kupanda historia ya uwongo kuwekewa serikali zisizo za matakwa ya wananchi yote tunafanya as ifike mahali na wao wafurahie Uhuru wao kama nchi guru sio kubanwa kwenye makwapa ya wachache.
 
Sasa naelewa kwanini Magufuli alisema Zanzibar wazimiwe umeme kama bado hawajalipa Deni Tanesco, kumbe anajua muda wowote Seif anapewa nchi...

Hata Prof Lipumba nae kamtimua nafasi na kumpa Sakaya ktk harakati za kuhakikisha kua kama CUF itapewa nchi basi kuwe na mvurugano ufanyike uchaguzi mwengine halafu CCM ishinde tena.

Duh... Hii nchi hii!!

Hivi mtu ukisoma sana uzeeni unakua chizi eennh?
 
Stori mfu hizi, juzi juz mlileta taarifa shein kuutubia Wabunge, bandiko fake
 
Si tuliambiwa linchi hili litajiri sana na muda mfupi tutaanza kuwakopesha nchi majirani na hao waliokuwa wahisani wetu!
What went wrong?
There is no hurry in Africa! When there is enough food (ugali), why think more ? Somebody on behalf will do it!
 
Sijaona chochote kipya kwa post hii zaid ya mdau kuunga unga Maneno na story za vijiwe vya ghahawa vya kibanda maiti na Buguruni malapa k na kutaka kuja kutuaminisha kama tetesi nyeti wakati ni msanii tu, Hakika hata kimoja jipya hapo.
Tz inasonga mbele kama kawa, wenye chuki wajinyonge.....wanakodoa kodoo
 

Ndugu yangu acha ujinga. Uchaguzi Zanzibar ni 2020 full stop!
 
Hiyo na
1) Serikali ya ZnZ inauza umeme kwa bei ndogo kuliko inayonunulia ,ikiwa mbinu ya kuwabembeleza wazenj
2) Makusanyo ya Zeco yanasaidia kuendesha serikali,kwani mapato ya ndani ,mikopo na misaada haitoshi kugharamia

Hiyi namba 1 si kweli, umeme zenji ni ghali sana.... Unit moja ni karibu 250tsh
 
Ndugu yangu acha ujinga. Uchaguzi Zanzibar ni 2020 full stop!
Kaka i think that is the bitter truth... ukweli mchungu kabisa ndo huo... lakn hata hivo 2020 si mbali... tuwe na subra njema...
 
Jahazi linazama ,akili za ajabu kusuburi 2020 kujinusuru.

Nyuma ya pazia hili la tetesi kuna mengi. Wasemaji wa CCM wapo kimya nyinyi mnajitekenya.

Tetesi naziacha mbali. Ninachokijuwa Tanzania imepewa masharti na wahisani. Tulikosa fedha za MCC na baadhi ya misaada mengine. Ninavyojuwa Balozi wa umoja wa Ulaya Tanzania kama miezi mitatu nyuma aliarifu kuendelea na Mazungumzo na rais Magufuli kuhusu suala la Zanzibar kupatiwa ufumbuzi na pendekezo lao la kurejeshwa GNU, na kuarifu matarajio yao kuwa muda mchache wanatarajia ufumbuzi utapatikana. Sijapata habari za kukanushwa taarifa hii na SMT wala SMZ.

Leo zilizopo ni fununu za mgawanyiko kwa wana CCM wanaotaka kutiiwa masharti na wale wasiotaka.

Lete taarifa za kweli kama hizi fununu sio wenyewe itakuwa umetusaidia.
 
sasa kama mtoa hoja huna taarifa kamili , unataka tujadili nini? TULISHASEMA HATUJARIBIWI, SIO NA VIKARAGOSI VYA NDANI NI HADI WENYE PUA NDEFU. HII SERIKALI NI HADI 2020 PANDE ZOTE BARA NA VISIWANI.
 
sasa kama mtoa hoja huna taarifa kamili , unataka tujadili nini? TULISHASEMA HATUJARIBIWI, SIO NA VIKARAGOSI VYA NDANI NI HADI WENYE PUA NDEFU. HII SERIKALI NI HADI 2020 PANDE ZOTE BARA NA VISIWANI.

Tofautisha kati ya "mtoa hoja" na "mleta taarifa" mimi nimeleta taarifa za tetesi tu.

Lete ukweli yakinifu.
 
Kaka Yangu kishada.. jambo ambalo mie linanitatiza saana ni kuwa kipi hasa kinochelewesha kufikia kukubali hayo maamuzi? wakati kweli yote inajulikana na maalim kasema haki yake atapata bro? what causes the delay? kwamfano chuoni mkishamaliza mitihani si majibu yanatoka na wala hayacheleweshwi? what causes these delays za watu kukubali kutiiwa kwa mwasharti ya wahisani? what causes the delay Maalim kuipata haki hio anotuambia haiko mbali kupatikana? give me one valid reason
 
Aliyeshinda kiti cha uraisi ni maalim Seif. Mpaka lini nyinyi CCM mtamuabudu Marehemu Nyerere kwamba bila ya ccm hakuna muungano, mpemba asipewe uongozi. Aibu gani hii. Huyu mkulu anasubiri cuf iongoze awakatie umeme ambao deni limetiwa na ccm kwa kugawana mapato wenyewe.
Nawaambieni nyinyi ccm tumewakataa tokea miaka 50 iliyopita kwa sababu dira yenu ni chuki na dhulma, hamkubali ukweli. Kazi yenu kupinga lolote lisemwalo na watu wasiokuwa nyinyi.
 
Wanadelay kwa kupoteza muda wakidhani labda wananchi watarudi nyuma. Sikiliza basi kijana ikiwa Seif atashindwa na jambo hili kwa ubaya wa watawala , jua tu walionyuma ya Seif wananjia ya mkato zaidi kuliko hiyo ya diplomasia, njia ambayo italeta heshima na haki zaidi. Ila kwa kuheshimu umoja na udugu na utulivu wa Afrika mashariki ndio maana tunavumilia. Ila ikiwa CCM inafanya ujanja wa kutokuheshimu maamuzi yetu sisi wananchi jua tu sisi hatuwaogopi na tutawanyakua ghafla ni ndio itakuwa mfarakano wetu.
 
Wao wanalishwa na kuvalishwa bure. Hawana cha kupoteza. Tatizo ni mimi na wewe pamoja na wana ukoo wetu
hata under wanunuliwa.ni kweli hawajui adha wanayopata wengine.ogopa mtu asiyejua bei ya chumvi....!!!
 

Kinachoendelea ndani huko binafsi sikujui. Lakini katika akili ya kawaida . Hapa kuna tatizo na njia za utatuzi ziko nyingi. Nafikiri wahusika wameplan njia ya diplomasia na kuweka mbadala wake. Tutazame pande tatu za wahusika. CUf kupitia kauli za Maalim Seif zimenukuliwa mpaka karibuni kule kisiwani Pemba. Kuwaahidi watu haki yao itapatikana muda si mrefu kupitia ziara ndefu aliyofanya. Upande wa CCM kuna ukimya kidogo na kauli za kujihami kuwa hakuna mabadiliko. Upande wa tatu ni wa jumuiya za Kimataifa. Kwa mara ya mwisho ni hiyo kauli ya Balozi wa EU Tanzania (nimeeleza hapo juu kwenye Comments) ambapo mrejesho hatujaupata wala makanusho.

Kuna usiri umetawala tu na sasa mwandishi alizipata hizi tetesi na kuziweka hapa ili mwenye taarifa za kuthibitika atujuze.

Bila shaka kuna kitu kinatokota.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…