mwalimu Jr.
Member
- Aug 20, 2008
- 51
- 4
UKOMUNISTI AU UJAMAA ulipokuwa ukikata roho televisheni za dunia nzima zilikuwa zikishangilia lakini hii leo UBEPARI umo katika sakra-mauti na wanafiki wote wanaupamba kwa urongo wa kila aina huku wakiomba lifanyike kila jambo ili 'artificial respiration' katika chumba cha wagonjwa mahututi kiwezeshe ubepari kuendelea kuishi.
Haiyumkiniki, kweli Wamarekani wanaweza kukwiba watakakokwiba lakini ubepari sio mfumo unaoweze kudumu kwa kuwa unaendelea kuwepo tu mpaka pale viongozi wa kibepari wanapojua kuwa wanaweza kuiba fedha yote iliyopo hazina na wao wakaendelea kujichana kama kawaida huku wananchi wa kawaida wakitumbukia kwenye kikaango cha mafuta ya kupikia.
Haya sio niliyoyasema mimi bali ni Karl Marx ambaye alistahili kuwa mtetezi wa ubepari na sio mpiga vita ubepari.
Hakuna UGAIDI mbaya kama ule wa VIONGOZI mliowachagua kugeuka wezi na mafisadi wa kutupwa. Kilichofanyika Marekani sio kingine ila ubia kati ya mabepari wa Republican party na wakurugenzi wa mabenki na taasisi za mikopo mikubwa mikubwa kuchota fedha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Marekani 2008 na kisha kutaka kuwabebesha msalaba wakopaji wadogo wadogo.
Dada Leah Bourne wa Marekani alishaandika kitabu kizuri tu kilichoitwa : The Inherent Instability of a Debt-Driven Economy' na wengi walimpuuza lakini yale yale aliyoyaandika ndiyo yanayoendelea hivi leo kama vile ni Mchezo wa kUigiza ambao ni 'live'!
Tafakari mwenyewe hivi gaidi wa kweli ni Bepari anayetaka kulitoa hata jiwe damu au wachanganyikiwa wachache wa madhambi ya ubepari wanaokurupuka hapa na pale na kuua na kuwajeruhi hata damu yao wenyewe?
Yanayotokea New York, London na kwingineko kwenye ubepari uchi uchi uliokomaa sio jingine ila ni jumuihso la kuanzishwa vita vya UGAIDI lililokuwa na lengo la kuruhusu VIONGOZI katika nchi za kibepari na vyama tawala kuwaibia WANANCHI wake kushoto na kulia kwa kisingizio cha kupiga vita ugaidi na kuanzisha uvamizi wa nchi kama Iraq na Afghanistan ili waibe bila kujulikana-toka kwenye mabenki yao na toka kwenye nchi wanazovamia.
Septembe 11 haikuua watu waliofikia hata 10,000 lakini toka hapa Marekani na washirika wake wamewaua Waislamu wasiokuwa na hatia milioni 4 na bado wanaendelea kuua.
Kiongozi mmoja wa Marekani aliwahi kuwaambia Wamarekani wenzake kwamba kama kuna kitu cha hatari na kuogopa sana ulimwenguni sio kitu kingine ila hofu. Akawataka waiogope hofu kuliko ukoma!
Chini ya uongozi wa Bwana George Bush, hata hivyo, Marekani sio tu imeweza kuwatia hofu Wamarekani bsli pia viongozi mbalimbali Afrika wakiwemo wale wa Afrika Mashariki.
Sote tunajua kuwa hofu au kisingizio chochote cha hofu kwa Afrika ni biashara nzuri kwa polisi wa Kiafrika kufanya biashara ya rushwa na kumalizia hasira zao za kulipwa mishahara kidunchu kwa watu masikini ha kama ilivyo Kenya kwa Waislamu ambao mfumo mzima wa nchi hiyo pamoja na kuchaguliwa kwa Raila Odinga kuwa Waziri Mkuu [ambaye Waislamu wengi walikuwa na imani naye ya kuibadili hali hiyo] umejengwa kuwadhalilisha na kuwahujumu Waislamu wa nchi hiyo.
Hatuamini kuwa Wana Usalama wa Tanzania wanaweza kuwa na wivu, ubabe, uonevu na chuki dhidi ya Waislamu kama jamaa zao wa Kenya. Na kwa sababu Watanzania sio watu wenye akili fupin na kununulika kwa bei sawa na bure hatuamini kwamba watawapa polisi wanyanyasaji wa Kenya ushirikiano wowote wa kutafuta wachawi wa Ugaidi wakati mchawi mwenyewe ndio huyo huyo anayetoa kitu kidogo kwa viongozi wao ili wawakurupushe jamaa kila inapokaribia Agosti 8 ili waonekane wanafanyia kazi rushwa waliyopewa na Waibaji wakuu wa madini Kongo na wavurugaji wa amani nchini humo.
Inafaa bila kujali tofauti zetu za rangi au dini au nyinginezo kujadili 'tatizo la matajiri kuhehushwa na hofu ya ugaidi kama kweli ni tatizo letu Afrika!'
Binafsi yangu ninadhani tuna matatizo makubwa kama vile kuuawa maalbino, ubakaji tena na midubwana yenye ukimwi; watoto wetu kunyanyaswa, kuumizwa hata kuuawa wakati mwingine na mijitu isiyo na huruma wakati kuna polisi tunaowalipa mishahara; barabara mbovu na zisizopitika kwa urahisi; serikali za Kiafrika kutufanza masikini zaidi jana tulikuwa tuna magari leo tunapanda na kunyanyaswa kwenye taksi, matatu na daladala; umeme ghali tena kwa asilimia ndogo tu ya wananchi mijini; hatuoni biahsara yoyote ya maana kati ya nchi zetu; mashirika ya hifadhi, bima, mifuko mbalimbali na benki kuu kutuibia fedha zetu; watoto wa viongozi na matajiri kupewa nafasi zote nzuri za masomo na kazi wakati watoto wa walalahoi wananyanyaswa kwa mikopo ya fedha za wazazi wao wenyewe na kuwa na wakuu wa vyuo vikuu wanasesere waliowekwa na viongozi wa nchi kwa sababu wanazojua wao wenyewe; elimu na afya zimepanda bei kichaa; kwingine hatuna maji wengine hawana umeme; usafiri, vyakula na vitu kupanda bei mara kwa mara na kadhalika na kadhalika.
Ninaamini Waafrika wa Afrika Mashariki tunastahili kuwa na hofu lakini sio ya kubomolewa kwa majengo ya balozi za Kimarekani kutokana na uzembe wao wenyewe. Watamtukanaje mamba wakati wako mgongoni mwake?
Hofu yetu iwe juu ya matatizo yetu ya msingi-chakula, maji, usalama, afya, elimu, mawasiliano na mahitaji mengine ya msingi kwa watu wetu.