Sala hii ni ya kuwaombea wanawake

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
505
Reaction score
872
1. Atakuwa na simu yake mpo nyumbani dakika hiyo anakwambia umbip hajui kaiweka wapi.
Tuhurumie Baba

2. Ana Nguo zimejaa makabati mawili lakini hajui avae nini ukimwambia mtoke!
Baba, ni magumu kwetu mambo haya.

3. Anakasirika ukikosa kumtumia text ya good night lakini yeye akikosa wewe inabidi uwe muelewa!
Tuwaeleweje, Baba?

4. Ana viatu zaidi ya pea 50 lakini hana viatu vya kuvaa vya kwenda ibadani.
Mungu uwasamehe

5. Akianza kuvaa saa moja atamaliza saa tano muda wote inabidi umsubiri tu.
Si kupenda kwao Baba ila nasi yanatushinda Bwana

6. Akienda saloon anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni na huna budi kumsubiri na usilalamike.
Mungu wetu, tupe moyo wa kuyahimili haya

7. Ana mafuta tofauti ya kujipaka mikono, shingo, kisogo, miguu, mpaka kisigino! Hata Mdomoni
Ee Mungu ni Wewe uyajuaye mateso tuyapitiayo Baba

8. Mnaachana asubuhi akiwa na furaha, na ukirudi jioni amenuna hataki hata kukusalamia na ukiuliza tu balaa.
Tupe uvumilivu ee Bwana!

9. Anajaribu ku match nguo na hereni na akiona hazifanani abadili nguo sababu tu ya hereni.
Teremka uwashike mikono yao baba..

10. Mkitembea barabarani inabidi ukae upande wa barabara eti wewe ni mwanaume ukigongwa na gari haina noma.
Eeh baba tuepushe na Hiki kikombe ulisema hawa ni wasaidizi wetu lakini tumekuja kuwa wafanyakazi wao.
 
Hahahaaa. Ila ukishakuwa mwanamke kuna vitu haviepukiki hata iweje.

Hiyo namba moja, mbili zinanihusu sana na namba tano japo sio sanaa ila inanihusu pia hasa kukiwa na ile mitoko muhimu. Ila mtuzowee tu jamani kwa sababu sidhani kama sala itasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…