joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Bado ninapata ukakasi na kushindwa kuelewa waafrica hasa viongozi wanaosisitiza sala na maombi katika kupambana na Corona, tena wakisisitiza zaidi kuoamba Mungu aliyeletwa na mabeberu ambao kutwa tunasema hawatutakii mema sisi waafrika na wapo kutukandamiza.
Hivi inawezekanaje watu ambao ndio chimbuka la huyo Mungu lakini wenyewe wameona kwamba katika hili janga hana msaada kwao na kuamua kutumia njia za kitaalamu kwa kufunga nyumba za ibada, lakini sisi ambao tuliletewa na kulazimishwa kumuabudu huyo Mungu wao tunaendelea kuamini atatusaidia?
Vipi tunatilia wasiwasi vifaa vya kupimia Corona vilivyotengenezwa kwa kufuata Misingi ya tafiti ya kisayansi na kusema vimetoka kwa mabeberu, lakini huyo Mungu wa mabeberu tunamkumbatia na kutohoji lolote kuhusu ukweli juu ya uwepo wake?