SALA,U KWA TUNDU LISU

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
POLE TUNDU LISU.
1)Maisha ya mwanadamu,yamejawa na mikasa
Mirahisi na migumu,mapito mengi na visa
Inapomwagika damu,nchi inajitikisa
Pole sana ndugu Lisu.

2)Ulihamka salama,kazini kuelekea
Ungeiona alama,labda ungelikimbia
Kilicho mbele na nyuma,ni mungu ana kijua
Pole sana ndugu Lisu

3)Maumivu ulopata,hakika kweli makali
Risasi ilikupata,chini ukaenda chali
Mlengaji hakusita,alikulenga kwa mbali
Pole sana ndugu Lisu.

4)Anaejua ni nani,muhusika hatujui
Kujua sababu nini,kwanini hatutambui
Ukweli bado sirini,ukweli haukimbii
Pole sana ndugu Lisu.

5)Basi kama ni siasa,muhusika awe nani
Alofanya hivi visa,kwanini haujulikani
Macho yanaponasa,hadithi huwa moyoni
Pole sana ndugu Lisu.

6)Baya hulipwa kwa baya,jema hulipwa kwa wem
Wachamungu wana haya,wabaya hawana jema
Wanaotenda vibaya,hawaoni nia njema
Pole sana ndugu Lisu

7)Twaomba pona mapema,tukutane mjengoni
Nchi ijengwe kwa wema,faida I mitaani
Sote tuje kusimama,tukiwa na furahani
Pole sana ndugu Lisu

SHAIRI-POLE NDUGU LISU
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Ni lini mara ya mwisho uliwahi kumuombea Babako? Au Tundu Lisu amekuuma sana klk Familia yake na mke wake anayelala naye kitanda kimoja na kumjua nje ndani?
 
Ni lini mara ya mwisho uliwahi kumuombea Babako? Au Tundu Lisu amekuuma sana klk Familia yake na mke wake anayelala naye kitanda kimoja na kumjua nje ndani?
Wacha kutoa povu Ndugu aliyekua harusini hahitaji mwaliko Kwa hiyo imekuumiza Kwa vina vya shairi Mungu Mpangaji
 
Mungu ni mwema na amani tele. Mungu huponya mja wake kwa matatizo aliyonayo. Ee Mwenyezi Mungu naomba uzidi kuimarisha afya ya Lissu na uponyaji kabisa. Amen
 
Wacha kutoa povu Ndugu aliyekua harusini hahitaji mwaliko Kwa hiyo imekuumiza Kwa vina vya shairi Mungu Mpangaji

Mungu mwenyewe umeanza kumjua jana, unafikiri kabla ya hapo hakuwepo?
 
Ni lini mara ya mwisho uliwahi kumuombea Babako? Au Tundu Lisu amekuuma sana klk Familia yake na mke wake anayelala naye kitanda kimoja na kumjua nje ndani?
Punguza jazba, jibu kishairi wewe.
 
Shairi lako ni zuri. Muda mwingi napitia hapa walau nipate shairi la kujisomea naambulia sifuri. Kongole ndugu Idd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…