Kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Bi. Salama Jabir katika EATV ni kizuri na nampongeza. Ila kwa maoni yangu, kitakuwa kizuri na bora zaidi kama atajali sana 'maswali fuatilizi' (follow up questions).
Mara nyingi, na hasa wale vijana wake, huwa na tabia ya kumkatiza mgeni mwalikwa wakati akijieleza kuelekea katika jambo muhimu zaidi na matokeo yake watazamaji wanakosa uhondo wa undani wa hoja au suala husika. Mfano mmoja ni wakati wakimhoji Bi. Faraja Kota-Nyalandu, ambapo alikuwa akielezea kitabu chake kuhusu mbinu 10 za kufaulu. Nilitegemea angetakiwa angalau aeleze mbinu kadhaa (kama sio zote), ili watazamaji, wakiwemo wanafunzi, wazisikie mbinu hizo. Badala yake, walimkatiza kwa swali jingine tofauti kabisa na kukata kiu ya mtazamaji kuzifahamu mbinu hizo za kufaulu (kwa mujibu wa binti huyo).
Kama hatajali, ningemshauri Salama na timu yake wajipange vyema ili kujiongezea ubora wa elimu ya kuhoji kwa nia ya kuboresha zaidi kipindi hicho.