Salama Jabir na Mkasi

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
Kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Bi. Salama Jabir katika EATV ni kizuri na nampongeza. Ila kwa maoni yangu, kitakuwa kizuri na bora zaidi kama atajali sana 'maswali fuatilizi' (follow up questions).

Mara nyingi, na hasa wale vijana wake, huwa na tabia ya kumkatiza mgeni mwalikwa wakati akijieleza kuelekea katika jambo muhimu zaidi na matokeo yake watazamaji wanakosa uhondo wa undani wa hoja au suala husika. Mfano mmoja ni wakati wakimhoji Bi. Faraja Kota-Nyalandu, ambapo alikuwa akielezea kitabu chake kuhusu mbinu 10 za kufaulu. Nilitegemea angetakiwa angalau aeleze mbinu kadhaa (kama sio zote), ili watazamaji, wakiwemo wanafunzi, wazisikie mbinu hizo. Badala yake, walimkatiza kwa swali jingine tofauti kabisa na kukata kiu ya mtazamaji kuzifahamu mbinu hizo za kufaulu (kwa mujibu wa binti huyo).

Kama hatajali, ningemshauri Salama na timu yake wajipange vyema ili kujiongezea ubora wa elimu ya kuhoji kwa nia ya kuboresha zaidi kipindi hicho.
 
Naomba niongeze...Salama ni mbunifu na ni mtangazaji mzuri,mimi na mnanisha na ellen wakule marekani,ila hawa ma bwana wawili,kwa kweli ni mizigo,wana point saa nyengine na saa nyengine wanautumbo mwingi..bila mfano,kwa sababu najua watamazaji wana lijua,sina bifu na mtu wala wivu,ila jamaa wamekaa kima igigo sanaaa.
 
wale madogo wako vizuri na nimefurahi walivyo match na speed ya the intelligent mega super star salama
 

Yes,Anashabihiana na Ellen DeGeneres.....I Wish Afanye Tv Talk Show Ya Kishkaji Na Kidaku(out of saloon)....
 
wale madogo wanaharibu kipindi banaa,wanapoteza sana swali lengwa na mada kwa ujumla...Salama aliangalie sana hilo maana yeye ndo mwenye maswali ya msingi sio hao madogo wachomekeaji tu!!
 
Wale madogo kiboko yao aje mgeni anaongea ongea kizungu huwa hawaulizi maswali kabisa sana sana huwa wanajikita tu kwenye kazi zao za kutengeneza nywele au kucha
 
Tatizo hawajui kiundani kuhusu wasanii husika wanaowahoji, salama anajua sana akimhoji lulu lazima suala la kuhongwa lihusishwe coz ni vitu vinavoshabiana na lulu, akimhoji ally rehmtullah lazima agusie ushoga, ni mtu ambaye ana upeo mkubwa wa kufikiri kwa umakini , wale jamaa wanaweza kuropoka tu na kubahatisha
 
Watu mnashindwa kuelewa ,kuwa mtangazaj pale ni salama,wale jamaa wapo katika kukamilisha aidia ya kipind kuwa ni mkasi "mazungumzo ya washikaj salooni" na hata kazi zao pia ni za saloon mfano Muba "yule mwembamba" ananyoa kwenye saloon moja ipo didis pub oysterbay.
 
K-Boko,
Ukifuatilia kwa makini utagundua tatizo sio hilo unalosema wewe; inawezekana kile kipindi ni kizuri sana kiasi cha airtime kuonekana haitoshi. Ukiangalia vizuri, utagundua si kwamba wahusika wanakatizwa bali watu wa editing wana-edit sana ili kipindi kiweze ku-fit within half an hour wakati mtazamaji hajaisha hamu ya kufuatilia. Nakubaliana na hoja ya "maswali fuatilizi" kwani ni mara nyingi sana Salama huwa utamsikia akiwaambia washikaji "NGOJA!" pale wanapataka kwenda nje kabisa ya swali lililotangulia! TRust me, kwa uchizi alio nao Salama kumpa nusu saa haimtoshi kabisa!!!
 
Last edited by a moderator:
Nilicheka sana siku Salama anamuhoji Lulu, na baada ya kum-tight kwa maswali ya ujeuri, Lulu akaanza ku-panic; hapo hapo Salama akampa za chembe "hoyaa, we vipi; unataka kunivalia kanga!"
 
Halafu nashindwa kuelewa sijui kwa nini salama uwa hamualik lady jaydee, au pengine lady jaydee hukataa kuhojiwa na kipindi hicho, naona salama kamaliza mastaa wrote mpaka muda mwingine anakosa kabisa watu wa kueleweka kwenye mkasi hadi wanatuletea wakina muhogo mchungu
 
Hata mi hua tunanikera badala tuendeleze kazi zao za salon mle hata hua siwaelewii kabisaa
 

Kwa hiyo Muhongo mchungu hafaii????
 
Kuna kipindi fulani kinaitwa the shop kule mtv,salama na timu yake wameiga almost kila kitu sasa sijui kwanini watu wanadhani yeye ndio kabuni..labda kikubwa kule wanatumia ung'eg'e na huku kiswazi...
Sorce:go to youtube/the shop mtv
 
Kuna kipindi fulani kinaitwa the shop kule mtv,salama na timu yake wameiga almost kila kitu sasa sijui kwanini watu wanadhani yeye ndio kabuni..labda kikubwa kule wanatumia ung'eg'e na huku kiswazi...
Sorce:go to youtube/the shop mtv
Hivi ni kitu gani pale ambacho ni very unique cha kuona Salama ameiga kila ki2 kutoka MTV? Ile show kufanyia Salon au maswali? By the way, hivi kuna mtu aliye interested na kile kipindi kutokana na mandhari ya wapi kinafanyika badala ya maswali? Na kama maswali, mbona maswali staili ile Salama hajaanza kwenye kipindi cha Mkasi? Ilikuwa vipi kwenye Planet Bongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…