Salamo Arouch, bondia aliyeponyeka kwenye kambi za Nazi kwa kushinda mapambano 200

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Salamo Arouch alizaliwa Januari 1, 1923 ni Muisraeli mwenye damu ya kigiriki pia. Alikuwa ni bingwa wa Uzito wa kati wa Ugiriki mwaka 1938

Kipindi Adolph Hitler anawakamata wayahudi na kuwaua naye alikuwa ni mmoja wao na alikaa katika Kambi za Auschwitz. Walifika kambi hiyo May 15, 1943. Alikamatwa yeye, baba yake na mpenzi wake

Katika kambi hizo atakayeshindwa huwa anapelekwa kwenye Chemba za Gesi au kupigwa risasi. Mara nyingi mapambano hayo yalikuwa ni hadi mmoja ashindwe au maafisa wa ki-Nazi wachoke kuangalia mpambano

Malipo ya mapambano hayo ilikuwa ni chakula na kufanya kazi rahisi kwenye kambi hizo ili aendelee kupambana. Salamo alitoka kwenye kambi hizo Januari 17, 1945 baada ya kambi kuvamiwa wakati wa vita ya pili. Familia yake hawakuweza kutoka

Alipotoka aliishi Israel hadi alipofariki April 26, 2009 akiwa na miaka 86

Maisha yake yameigizwa vizuri katika filamu ya Triumph of the Spirit.

 
Duh ngumi za zamani hatari, naona gloves hazina hata pads, nuckles nje nje. Hapo ukichezea ngumi kumi tu za kichwa/uso umechakaa balaa.
 
Kwa Lugha rahisi alisababisha vifo vya wenzake 200 au alishiriki mauaji ya wenzake 200 ili yeye mmoja apone badala ya kushirikiana kuwaua askari wote waliokua wanawalinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…