Tatizo hamja komaa kisiasa,kameni za CHADEMA wanajaa sana vijana ambao wengiwao ni washangiliaji lakini hawapigi kura,CCM imewashika wazee na wanawake ndiomana inauhakika wa kura.
ATENGEZEKE, karibu JF, siasa za Bi'mulo ni moja ya maeneo yenye siasa kali kama za Busanda, Wasioijua Biharamulo waacheni pembeni waisikie hivyo hivyo.
Kwa aliyefika Biharamulo ya enzi zile na akifika leo, anaweza kulia au machozi yakamtoka, amini usiamini nilikuwa nina kakazi fulani hapo Biharamulo, lakini nililazimika kulala Chato, wengine wengi walikuwa wanalala Geita, wakati huo unapita kwenda Biharamulo, Geita ilikuwa mapori tuu na hiyo Chato ndio kabisa hata mi... haijatungwa!.
Leo Chato ndio kidume, lami mpaka sebuleni, Bi'mulo ni vumbi mpaka ndani ya glasi, chanzo cha yote hayo ni serikali ya CCM halafu bila aibu eti bado mnaikumbatia!, Watu wa Biharamulo na Busanda ni watu wa ajabu sana!, uchaguzi ukishamalizika ndipo nitasema, lakini kwa sasa nawashauri tuu, hebu fungueni macho na October 31 mseme "Basi imetosha!".