Prof Janabi wa JF
Senior Member
- Jul 7, 2023
- 165
- 450
Umeshaomba vitu vya kwenda nje ya nchi mara kadhaa ili haujawahi hata kuitwa kwenye interview japo unajiona kabisa vigezo vingi ulikuwa navyo? Haya acha kuamini uchawi ukaanza kutafuta waganga, leo nimekuja kushare experience kidogo kufanya uongeze uwezekano wa kupata application yako ijayo.
Mambo ya kujua
Hata kama fursa inatolewa na taasisi zilizoko Tanzania mathalani ubalozi wowote, jua kuwa hizo huwa haziangaliwi na watanzania kwenye kuamua nani aende
Mambo mengi mnayoomba yanapitia mchakato zaidi ya mmoja, kwanza mnachujwa na system(IT System), kisha wataalamu wa kujitolea, then wataalamu wa taasisi husika.
Kwenda international inahitajika sana kuonesha traits za kiuongozi.
Volunteerism inathamaniwa sana duniani anza sasa, hata ukienda kufanya kasaidia kufanya usafi kwa watoto yatima, rekodi jambo hilo. (Sasa wewe lete unanii wako kuwa hutaki kujulikana)
ZINGATIA
Usitumie vifupi kwenye application yako: Nishakuambia pale juu wanaopitia application yako hawatokei kwenu, sasa acronyms za kwenu hazieleweki kimataifa. Na hakuna mtu wa kuanza kutafuta ulimaanisha nini kwa context yako wakati kuna applications zaidi zinasubiri kuangaliwa. Mfano: Ukiuandika TCRA na mtu anayereview application yako ni mmarekani atadhani unaamanisha Texas Court Reporters Association(TCRA) kumbwe wewe umemaanisha Tanzania Communications Regulatory Authority(TCRA). Hizo acronyms haziwezi kueleweka, kwa hiyo acha uvivu andika kwa kirefu maneno yote hadi elimu yako, unless system imeweka vifupi yenyewe kama BsC, BA nk. Vinginevyo weka kirefu, andika kwa kirefu jamaa, hata kwenye elimu hizo vitu ziko tofauti sana.
Acha kutunga vifupi kwa uvivu wako: Kuna watu wanazingua, anachukua herufi za mwanzo anaunda kifupi akidhani watu wa taasisi husika wataelewa. Mfano, kuna Mandela Washington Fellowship ambao kwa kifupi ni YALI yaani Young African Leaders Initiative, sasa wewe kwa uvivu unaandika MWF ukitaka kumaanisha Mandela Washington Fellowship, kumbuka hiyo acronym ni yako kwa uvivu tu wa kuandika. Reviewer hadi akili ije ku-click kwamba umemaanisha nini ukizingatia sio mtu wa unapotokea, unakuwa ushalimwa X kitambo.
Achana na AI wewe jamaa: Oya acha mambo ya kwenda kwenye AI ikufanyie kazi, ifanye AI kucomplement sio kama substitute yako. Yaani andika kwa uziri weka kwenye AI inyooshe kiingereza kama bado kinakutoa jasho. Sasa wewe jidai ni express, tumia AI kama kichwa chako, baadae ooh nimerogwa! Umejiroga mwenyewe ndugu yangu, sizidishi maneno. Usitumie AI hata kama application haijasema usitumie. Hebu onesha unajua unachokifanya sio kuifanya AI ikusemee wewe jamaa.
Onesha sifa za kiuongozi: Hata kama application haijakuambia kuhusu uongozi jua kuwa wanaotoa hela hawatarajii uende nje urudi bichwa jeupe. Wao wanatamani kurekebisha fikra za viongozi wa baadae. Onesha sifa zako za kiungozi acha kutaka uonewe huruma bali onesha how good you are. Kuna mtu anaanza kusema ooh, mimi nimezaliwa uswahili/kijijini najua tatizo la umasikini kwa uzuri, halafu ukiangalia application yake hana sifa hata moja inayoonesha kuwa anajua tatizo la umasikini kwa experience yake ya kuzaliwa au kuishi uswahilini/umasikini. Kama ulishwahi kwenda kwa mtendaji wa kijiji au kata ukamwambia jambo hayo ndio mambo ya kuandika, sio kusema vitu ambavyo haviongezi sifa. Hauwazi kwanini wanaotembea nje ya nchi wengi ni watu wa maeneo mazuri? ni kwa kuwa wanapoandika wanaonesha wanayajua matatizo na sio kusema wameishi matatizo.
Kwenye application jifagilie: Kuna watu mnasema wakiniita ndio nitawaonesha mimi ni nani, nikuambie una safari ndefu. Muoneshe mtu kwenye application yako wewe ni nani ili mtu avutiwe kukuita. Acha kusifia application, jisifie wewe. Yaani kuna watu wanaleta uchawa kwenye application. Mfano unaomba Reham al-Farra Memorial Fellowship, badala ya kujifagilia wewe unaanza kumfagilia Reham al-Farra kwamba unamjua sana? Hiyo tabia ya uchawa iishie huko ukiomba kazi kwenye taasisi za huko, ukiomba international wanataka kujua umefanikiwa nini.
Taja tatizo, sema umefanya nini: Mwanangu una GPA kubwa ila unalaumu, kwa kuwa huna unachokifanya. Kazi yako ni kutaja matatizo tu, na hauna kitu umejaribu kukifanya. Kama shida ni haki za wanawake, sema umefanya nini kusaidia haki za wanawake, hata ukisema huwa unaandika JF ili kukuza uelewa wa haki za wanawake inaonesha tayari wewe unajaribu kutatua. Mimi najua shida ya wabongo kwenda nje ni exposure, hivyo naandika hapa ili watu wafunguke mdogomdogo, kwenye CV yangu naweka kwamba nimechukua initiative hii baada ya kukuta wabongo ni wachache huko nje ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kifupi acha kuwa mlalamishi na kuilaumu serikali, nje wanajua uongozi/serikali ni tatizo wanataka kuona juhudi zako binafsi ni zipi.
Nimechoka kuandika, kifupi na wewe usiapply shavu lolote la nje. Nenda kwa waganga wakufanyie maajabu ya kuja nje.
See you next time.
Mshamba anayewakilisha Taifa Marekani.