Salamu kwa mpenzi

Afrika Furaha

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2010
Posts
329
Reaction score
10
Habari za JF wanandugu. Kwa kawaida ni kitu cha busara kumsalimia SHIKAMOO mtu aliyekuzidi umri. Lakin Je, kama una mpenzi wako amekuzidi umri ni lazima kusema SHIKAMOO? Hasa kwa mabinti ambao wao ndio huwa na wapenzi wakubwa kiumri zaidi yao. Mfano, Binti miaka 22 mwanaume 29, je huoni ni lazima umsalimie shikamoo?
 
kizazi ya ck hiz imevaa bukta....dawa kula nyama ya bata kwanza kila siku usiku....shikamooo zitamininika hadi usingizini....!!!
 
Mabinti wengine ataanza anakusalimia shikamoo, mkishaanza mahusiano shikamoo inakufa.
 
mabinti wengi hasa wa bara hawapendi kutoa shikamoo kwa wapenzi wake hata kama kunatofauti ya miaka 10.nadhan hisia iliyopo ni kua salamu ya shikamoo inaashiria kuto kuwepo kwa ukaribu wa kutosha baina ya wapenana.pia inafanya uhusiano uwe wa kikanuni zaidi kuliko kimazoea hivyo kufanya walengwa wasiweze kujiachia ipasavyo
 
Hivi nini maana ya shikamoo.....tuanzie hapa kwanza!
 

Kwani shikamoo ni lazima...???
 
Shikamoo zingefutwa tu, hazina maana. Kwanini tusitumie maneno ya kawaida tu kama "habari za leo", n.k
 
maneno hayooo,,,, ngoja ntulie niyasikize...... chini ya miguu yakooo,,,,kaazi kweli kweli,,,
 
Salamu ni heshima iwe shikamoo iwe habari ya saa hizi salamu ni salamu tu, hamjawahi kuona mfano si wote tafadhali msichana anapita kuna vijana wamekaa pale hasalimii akishapita utasikia msichana hana adabu kabisa huyo hata hasalimii kwani walikuwa wanataka shikamoo hao?/ si walikuwa wanataka mambo, habari zenu, saa saa hizi. So salamu ni ishara ya heshima na kuthamini mtu si lazima shikamoo??? Hapa swala ni salamu na si shikamoo wakuu. Hata huyo binti akikusalimu habari ya saa hizi mume/BF wangu utasikia kakupa heshima yako si lazima kivile shikamoo itumike aaa mie wangu tunapeana mambo mume wangu mpenzi umeamkaje kwisha habari tunaendeleza siku ha ha ha ha ha
 
Mmmh! Hata kwa wazazi au wakwe unaweza kusema hivi??
 
Bora kusalimiana kwa kimombo.
Shikamoo haina maana kabisa. Kwanza kuna watu wakitoa Shikamoo, wakiitikiwa tu ile marahaba ndio basi tena, hawaendelei kujuliana hali, n.k. Bora watu wa pwani, ambao hujuliana hali kwanza na mwishowe ndio wanapigana shikamoo. Lakini, I wish ingefutwa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…