Salamu kwako Rais, wakatae wanaokuroga kwa maneno na rangi ya kijani

Salamu kwako Rais, wakatae wanaokuroga kwa maneno na rangi ya kijani

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2016
Posts
2,668
Reaction score
3,751
Habari ya Jumamosi.

Ninayoheshima kubwa kukuandikia mama kukuambiatu kwa ufupi sana.

Mama wewe haya yanayofanyika unayaona na unajua mengi kuliko sisi raiya wako. Hilo lipo wazi

Ninachoweza kukuambia hao watendaji wako ambao wengine niwabadhirifu wengine ni wazembe wanakuloga sana. Uchawi wao nimaneno yakukupamba mitandaoni na majukwaani.

Kila kitu wanakusifia hata uliposema hutaki machawa wanakazana kwasababu wanajua bado hujawakataa.

Mfano wiki iliyopita kuna mteule wako mmoja amesema eti umejenga reli kuwazidi hadi wajerumani. Sasa unaweza ukajiuliza ni kweli?

Mimi ninasema kama nikweli hata tusiwaombe misaada.
Uchawi mwingine wanaoutumia nirangi ya kijani na njano.

Wakishapiga hizo nguo zao wanajifanya niwazalendo sana na INAWEZEKANA nawewe unaamini kama LABDA niwazalendo. Ila elewa kwamba wengi waliokutia fedheha kupitia ripoti ya CAG nihaohao kijani na njano. Sio makamanda wala rangi ya zambarau

Kilamtu ana mema na mabaya, ana ubora na mapungufu.. Ila ninachoweza kumzungumzia nikwamba linapokuja suala lamtu anaeweza kufanya kazi apewe asieweza au mwizi aondolewe. Maneno na rangi za mavazi yao isiwe kinga na ngao ya kukufanya usichukue maamuzi.

Hivi mama unapoenda hata kwa majirani na marafiki kuomba msaada au mkopo kwa ripoti ya CAG huoni kama wanakushangaa? Mama chukua hatua usizubaishwe na maneno na rangi wanazotumia huo ndio uchawi wao

Nimalizie kwakusema ripoti ya CAG imeivua nguo serikali. Chutameni huo ndio uungwana na kuchutama nikuwakataa wabadhirifu
 
Mama wnachokitaka ni kuendelea kukalia kiti. Adui mkubwa wa mama ni yule anayetishia uwepo wake kwenye kiti cha ikulu. Wengine wote mama hawamsumbui.
 
Mama wnachokitaka ni kuendelea kukalia kiti. Adui mkubwa wa mama ni yule anayetishia uwepo wake kwenye kiti cha ikulu. Wengine wote mama hawamsumbui.
Sasa haoni kama hao wezi ndio wanaweka miba na vinyesi kwenye njia anayotaka kupitia?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Majambazi yote yatafanya juu chini, kuhakikisha sa100 anapita, ili waendelee kufakamia Asali.. Kwa sababu Majambazi wanauwezo wa kumziba mdomo saa100.
 
Sasa haoni kama hao wezi ndio wanaweka miba na vinyesi kwenye njia anayotaka kupitia?
Hapa kwetu hakuna chaguzi. Mama hata akipata kura ya mumewe Hafidh peke yake atajitangazia ushindi kupitia tume mtu (siyo tume huru). Ndiyo maana hana hofu.

Na akijitangaza wananchi hawatajali, bado wataenedelea kujadili Simba na Yanga pamoja na connection ya Nyalandu.
 
Ooohoooo umehama channel
 
Wamama wako kihisia zaidi, kukataa asisifiwe ni kutomtendea HAKI
Kumsifia sana mtu mwenye akili timamu mbele za watu nikejeli. Kumsifia sifia Raia namba moja kila mara nikumdhihaki
 
Hapa kwetu hakuna chaguzi. Mama hata akipata kura ya mumewe Hafidh peke yake atajitangazia ushindi kupitia tume mtu (siyo tume huru). Ndiyo maana hana hofu.

Na akijitangaza wananchi hawatajali, bado wataenedelea kujadili Simba na Yanga pamoja na connection ya Nyalandu.
🤣🤣🤣Magoli ya maza
 
Back
Top Bottom