Salamu na ujumbe wangu wa Krismasi kwa wanachama wote wa JamiiForums

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Tumsifu yesu kristo/Bwana Yesu asifiwe wapendwa katika Kristo.
============<>====<>==
Wapendwa kesho ni siku ya furaha kwa sisi Waamini wa Yesu Kristu, Ambapo itakua ni sikukuu ya kumbukumbu ya Kuzaliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Wapendwa ningependa nichangie kidogo nanyi kuhusu jinsi ya kusherekea sikukuu siku ya kesho.

>>Kesho kwa atakae fanikiwa Afike kanisani yeye na familia yake pia waweze kupata Sakramenti ya Kitubio na Ekaristi takatifu.

>>Kaeni na familia zenu kula pamoja na kusherehekea pamoja.

>>Usiwaache watoto wako wakala hadi wakapitiliza ikawa mbaya kwa afya zao.

>>Kwa watakao ruhusu watoto wao kwenda kusherehekea na wenzao sikukuu baasi wawasindikize wawapeleke, wawavushe barabara au wawapandishe gari, msiwaache wazurure bila kuwepo mkubwa wao.

>>Siku ya kesho msinywe sana mwishoni mkapelekea kuanza kufanya yasio mpendeza Mungu, pia ni vyema mkaambatana pamoja kama familia nzima.

>>Itapendeza zaidi kama siku ya kesho mkaitumia kusherehekea na watu wenye ukosefu wa mahitaji mbali mbali mfano Wagonjwa, wazee, yatima, wafungwa walemavu etc.

>>Endesheni kwa uangalifu magari yenu isije kua siku ya historia mbaya kwenye maisha yako.

>>Mkumbuke kumtolea Mungu shukrani kwa kuweza kuwafikisha Krismasi hii ya mwaka huu.

Ni hayo tu ndugu zangu..
Nawakaribisheni nyumbani Fuoni Zanzibar pia watakao weza tukutane Kanisa la minara Miwili.

"Msaada wangu u katika bwana aliye zifanya Mbingu na Nchi"
Aksanteni wapendwa.

-Mondray-
24 Dec 2017
 
Naona watu wamekususa x- mas njema mkuu jf watu wachoyo sana wa comment ngoja nikomment mpaka zifike 100 naona vyuma vimekaza hawataki hata kusikia baraka za sikukuuu
 
Wamekusikia sana.. Nawe pia uwe na Krismasi njema..

Ila leo usiku maguest, malodge na mahoteli yatajaa, kondomu zitauzika sana!!
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Ni kweli dada Coz watu wanapenda story za migegedo tu hahaa
Naona watu wamekususa x- mas njema mkuu jf watu wachoyo sana wa comment ngoja nikomment mpaka zifike 100 naona vyuma vimekaza hawataki hata kusikia baraka za sikukuuu
 
asante Mimi kesho mgeni wako kumbe yupo jirani ....nipo tunguu hapa kesho mgeni wako rasmi
 
Ahsante ila Kaa mbali na Shetani msogelee Mungu zaidi..πŸ™‚
Wamekusikia sana.. Nawe pia uwe na Krismasi njema..

Ila leo usiku maguest, malodge na mahoteli yatajaa, kondomu zitauzika sana!!
 
Thanx and u too..

Chambu ni neno la Kiha likiwa na maana mzazi wa mtu (me/ke) aliyeoa au kuolewa na mwanao..

Eg. Baba yako na baba wa mke wako/Mama yako na mama wa mke wako ndo wanaitana Chambu.
Chambu ni nini? eleza haraka kabla sijachukia

Merry Christmass to u
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…