Author
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 1,715
- 8,058
Kumbuka;
Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk. Akaachana nayo.
Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli. Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika?
Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.
Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?
Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 9 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako.
Bora ukazinywee Pepsi au juisi baridi au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.
Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara ni faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.
Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?
Hivi huna habari Bakhressa kuna biashara alishafanya na akaachana nazo. Una habari Dangote kuna wakati alipoteza dola bilioni 10 in one year? ($10 billion lost in a year!)
Trump mwenyewe aliwahi kufilisika kabisa. NIL. Zero.
Rock bottom.
Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa wa $1 million. Kama haupo tayari kupoteza pesa basi kazinunulie nguo mpya za sikukuu zikifika uvae upendeze.
Sisemi LAZIMA pesa ipotee. No. Ila nasema kama hauko tayari kupoteza you are not ready for the business world.
Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU na utayari wa kupoteza katika jamii huwa ni wachache tu.
Narudia sisemi uwe careless, No do your research. But uwe tayari kupoteza hela licha ya research zako. Kwani wewe unaweza kufanya research zaidi kuliko Dangote?
If you're afraid to lose money NEVER INVEST.
Baki na hela zako Bank.
Hizi ni Salam za Mwaka Mpya 2019 kwenu
Sent using Jamii Forums mobile app