Salamu za mwaka mpya toka TRA

Salamu za mwaka mpya toka TRA

TRA Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
128
Reaction score
370
WhatsApp Image 2023-12-31 at 20.07.11.jpeg
 
Nyie ni watata sana.
Mmeyumbisha sana uchumi wetu binafsi kwa kubambikizia kodi lukuki.

Salaam zenu za Mwaka mpya mngesema angalau mtashughulikia kero zotokanazo na changamoto za kodi hususan makadirio yasiyozingatia uhakisia na tozo zisizosaidia ukuaji wa mitaji.

Halafu muache kutumika kisiasa kwa sababu watu wengi wenye kukosoa serikali wanabambikwa kesi za kodi....

Mnazingua sana
 
Wambieni Tanesco kuwa umeme kutokuwa wa HAKIKA kutapunguza makusanyo Kodi mwaka kesho.
 
Wezi sana, kaka yangu mtoto wa baba mkubwa upande wa bibi mdogo alijenga nyumba nne dar es salaam baada ya kufanya kazi miaka mitatu ya mwanzo hapo TRA.

Tena mkampa demotion kali ya kumpeleka wilayani huko kwenye mikoa maskini. Akatembeza rushwa na akarudishwa tena dar. Sasa hivi ni bilionea.
 
Tunashukuru na tunawapongeza sana kwa kuendelea kufanya kazi nzuri na muendelee kutatua changamoto za wafanya biashara hasa wenye matatizo ya EFD!

Ninyi ni tegemeo la nchi kwenye kukusanya mapato na tungependa hata siku moja tujue kwa mchanganuo mchango wa Sanaa na Wasanii kwenye kodi na kulipa kodi tungependa kupata kwa details sekta ya Sanaa na Wasanii wamechangia nini na wanaliingizia kiasi gani Taifa kupitia sanaa!

Na pia tungependa kujua mnakusanya vipi kodi kwa wasanii wanapolipwa kwenye show zao? Hili jambo liko serious kiasi gani kuhakikisha kila mtu analipa kodi kutokana na anacho ingiza?
 
Wezi sana, kaka yangu mtoto wa baba mkubwa upande wa bibi mdogo alijenga nyumba nne dar es salaam baada ya kufanya kazi miaka mitatu ya mwanzo hapo TRA.

Tena mkampa demotion kali ya kumpeleka wilayani huko kwenye mikoa maskini. Akatembeza rushwa na akarudishwa tena dar. Sasa hivi ni bilionea.
Sasa hapo unashitaki TRA? Kwanini usipeleke jambo hili TAKukuru? Kujenga nyumba ni dhambi? Kama una ushahidi peleka Takukuru kinyume na hapo ni chuki na wivu kwa ndugu yako! Hivi angekupa nyumba moja ungemuandika hapa bila ushahidi?
 
Kidatta, mtu muungwana sana anayemtegemea Mungu, na Mungu alimlinda wakati anataka kumezwa na firauni. Huyu ni living testimony ya jinsi Mungu analinda wqtu wqke

Very humble person, sema hapambani vizuri na wahuni ndani ya mamlaka. Jamaa ana strong mental health.
Mpole na mnyenyekevu bila kujali anatokea kanda maalum.

Binafsi, namtakia heri ya mwaka mpya na Mungu wa mbinguni aendelee kumtunza na kumuongoza kuhakikisha anakusanya kodi halali na kuwa bana wakwepaji wote.
 
Ila TRA mnatugombanisha na watu kwenye suala la kukata 5% WHT.
 
Kidatta, mtu muungwana sana anayemtegemea Mungu, na Mungu alimlinda wakati anataka kumezwa na firauni. Huyu ni living testimony ya jinsi Mungu analinda wqtu wqke
Umefika kwenye mahekalu yake mbweni

Ukiona mahekalu yake utabadili msimamo wako wa kumsifia
 
Back
Top Bottom