Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Ndugu Fahdu Davis, Kocha wa Simba
Awali ya yote nakupongeza sana kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya ndani ya klabu ya Simba Sports Club.
Ama hakika hadi sasa kupitia wewe na benchi lako la ufundi sisi wanachama na mashabiki wa Simba tumeridhika na performance ya timu yetu hadi sasa.
Timu yetu sasa sio ya kubezwa, inacheza mpira mzuri unaoeleweka, umewafanya wachezaji wawe na upendo na kuheshimiana, kidogo siku moja mchezaji Jean Charles Ahoua alitaka kuleta za kuleta pale ulipomfanyia sub akanuna akipinga uamuzi wako.
Ndugu Kocha Fahdu, najua hujui Kiswahili lakini wakalimani wako watakutafsiria hiki nilichoakiandika kuhusu timu yetu ya Simba kuelekea mechi ya Derby.
Kocha Fahdu, jumamosi Simba unayoifundisha inashuka dimbani kucheza na hasimu wake aitwae Yanga ambaye anaongoza ligi.
Kocha Fahdu, wewe ni mwalimu tu, huna mapenzi na timu, leo unaweza kuvunja mkataba ukaenda Yanga na asikuulize mtu, lakini mimi hadi nakwenda kaburini siwezi kwenda kushabikia wala kuhamia Yanga.
Kocha Fahdu, mechi hiyo ni ngumu sana kwetu, ni fainali hiyo mechi, tukimkaza Yanga hiyo jumamosi safari ya ubingwa ni ileee.
Kocha Fahdu, Yanga wamekuwa wanatusumbua sana kipindi hiki cha hivi karibuni ingawa huko nyuma miaka ya 1990 wakati wakiongozwa na kigagu mzee Ngozoma walikuwa wanatuburuza sana, walikuwa na mshambuliaji akiitwa Mohamed Hussein.Alimuonea sana kipa wetu Mohamed Mwameja.
Miaka ya 2000 tukawa tunawakaza sana Yanga lakini mambo yameendelea hadi walipopata udhamini wa GSM, kibao kimebadilika.Wanatufunga wanavyotaka.
Wewe mwenyewe shahidi, majuzi tu raundi ya kwanza wametoka kutufunga na wewe ukiwa kocha, na sasa hivi raundi ya pili wenyewe wanasema lala buriani ndio tarehe 8.
Kocha Fahdu, elewa hiyo mechi sio ya ufundi, hiyo mechi sio kama unacheza na Azam au Singida, hiyo ni mechi nyingine kabisa.
Hiyo mechi weka pembeni utaalamu wako, waachie wenzako kwenye benchi la ufundi wakushauri, hiyo mechi ina mambo mengi nje, ukiambiwa mtoe Camara fasta unatakiwa umtoe bila kuuliza, vinginevyo utatugharimu.
Usiwe mbishi kwenye mechi hiyo, mechi ya raundi ya kwanza aliyofungwa Camara ilikuwa zumbulu tu, Chama kapiga faulo kipa akalogwa akaurudisha ndani Kijiri akajifunga, wanaojua kubet walishaiona hiyo gemu na walikuwa hela siku ile.
Nakukumbusha kuna kocha mmoja alikuwa akiwasumbua sana Yanga, akiitwa Mansour Magram (Sasa marehemu).Huyu kocha alipokuwa akifundisha Sigara hakuwahi kufungwa na Yanga, kama alifungwa ni kwa nadra sana, akaenda Simba pia akawa hivyo hivyo, huyu kocha alikuwa akiwapanga akina Bakari Idd, Idd Seleman kukabiliana na wachezaji wakorofi wa Yanga enzi zile.Sasa mechi yet una Yanga usije kudhania kuwa utawafunga kwa utaalamu wako hapana, hivi navokwambia wachawi wao wako Pangani, wako Zanzibar, wako Lindi na maeneo kadha wa kadha wakitafuta ushindi, hebu jiulize kwanini wao na wachezaji wao wazuri namna ile lakini bado wanatumia nguvu za kiza.
Kocha Fahdu, siku hiyo tarehe 08 Yanga hawatapita geti la kawaida, wameshaandaliwa sehemu ya kupitia, ndio uone kuwa mechi hiyo haina ufundi.
Msikilize sana Matola na waswahili wenzake pale benchi la ufundi, vinginevyo utaharibu mechi na unaweza kufukuzwa kwa mechi hiyo.
Nakushauri anza na kikosi hiki, Camara, Kapombe, Nouma, Hamza, Malone, Kagoma, Kibu, Mavambo, Ateba, Mpanzu, Chasambi, utakuja kunishukuru.Ahoua mwache kwanza mechi haiwezi hiyo, ukimpanga atakuwa mchezaji wa kumi na mbili wa Yanga huyo.
Sikiliza sana wataalamu wan je wanakwambia nn vinginevyo utakuwa umetukosesha sana amani siku hiyo kocha wetu.
Hiyo mechi ndio inaweza kukuweka Simba au kukufurumusha kwani hatuwezi kufungwa na Yanga mara ya sita mfululizo.
Nakutakia kila la heri kwenye mechi hiyo, Simba Nguvu Moja