Salamu za pongezi zaanza kumiminika kwa Museveni

Salamu za pongezi zaanza kumiminika kwa Museveni

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa mujibu wa matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya DW mchana wa leo, tayari salamu za pongezi kwa ushindi wa kishindo wa Museveni zimeanza kumiminika Uganda.

Wakati salamu hizo zikienda huko, ugeni mzito wa balozi wa Marekani kwa Bobi Wine anayeendelea kuwekwa kizuizini nyumbani kwake umezuiliwa kumfikia.

Museveni amemshutumu balozi huyu Beberu kwa kuingilia mambo ya ndani ya Uganda wakati sisi (Waafrika) hatuyaingilii ya kwao.

Hata hivyo, hadi sasa salamu za pongezi toka kwa rais wetu mpendwa Dk. Magufuli ndizo pekee zimeshapokelewa na nyingi nyingine zikitegemewa hivi karibuni hasa tokea Rwanda, Zimbabwe, China na nchi marafiki.

Hongera rais wangu Magufuli kwa kulifungua pazia hili la pongezi tokea juzi na kwa ujasiri mkubwa.

Umeonyesha njia, sasa yetu macho kuona nani shupavu mwingine atakayefuata nyayo zako.
 
Naam, salamu za pongezi nyingine zipo njiani kutokea
North Korea
China
Venezuela
Cuba
Russia
Rwanda
Iran
 
Bila shaka Mh. Rais atahudhuria uapisho wa rafiki yake kipenzi.

Ingependeza aende na ujumbe mzito kabisa kujibu ziara yake kule Dodoma.

Atakuwa naye alikuwa akiangalia TBC ya huko. Atakuwa naye alishangilia ushindi wa Hai ya huko.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwa mujibu wa matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya DW mchana wa leo, tayari salamu za pongezi kwa ushindi wa kishindo wa Museveni zimeanza kumiminika Uganda.
Barabara yako Kioboko yenu katangaza kuwa tenda kesho itangazwe ili kuikarabati kutoka Rusumo hadi Nyakahura. Jembe hilo JPM
 
Barabara yako Kioboko yenu katangaza kuwa tenda kesho itangazwe ili kuikarabati kutoka Rusumo hadi Nyakahura. Jembe hilo JPM

Tuna ratibu salamu za pongezi kwa jembe letu jingine kwanza.

Hivi kwani Nyakahura nayo ishaunganishwa jimboni Chattle?
 
===
Uganda is not a failed state. Therefore, foreign interest agents aiming the demise of Uganda should think twice.
 
Tuna ratibu salamu za pongezi kwa jembe letu jingine kwanza.

Hivi kwani Nyakahura nayo ishaunganishwa jimboni Chattle?
Lusahunga hadi rusumo bandugu! Kuanzia leo Acha kumkashifu JPM maana kilio chako amekisikia. Hivi unajua kuwa kwa siku Rwanda inanunua tani 600 kutoka Wazo kwenda Kigali?
 
Lusahunga hadi rusumo bandugu! Kuanzia leo Acha kumkashifu JPM maana kilio chako amekisikia. Hivi unajua kuwa kwa siku Rwanda inanunua tani 600 kutoka Wazo kwenda Kigali?

Kuweka rekodi sahihi, hadi sasa bado ni jembe letu peke yake ndilo lilokwisha tuna salamu za pongezi. Si Iran, North Korea wala China walosha sema lolote.

Vipi pia Hai huko, CCM ya huko imeweza kuikomboa kama ya huku?

Au wewe ulikuwa huangalii TBC ya huko?
 
Ushindi wa M7 ni ushindi wa watanzania wote, maana angalishindwa hata lile bomba lingeenda Kenya. Ujue Kenyatta ali support Mpuuzi Tundu Lissu na sasa mvinyo ulikuwa halali yake, yote ni husda kwa maendeleo ya Tizeti chini ya JPM. Atelele
 
Watanzania wote ndiyo kina nani?

Na miye umenijumuisha humo?
 
Back
Top Bottom