Salamu za Rambirambi za Freeman Mbowe kutoka Gerezani zasomwa Kwenye msiba wa Mkwe wake, waombolezaji wabubujikwa na machozi

Salamu za Rambirambi za Freeman Mbowe kutoka Gerezani zasomwa Kwenye msiba wa Mkwe wake, waombolezaji wabubujikwa na machozi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Freeman Mbowe aliyeko gerezani kwa tuhuma za uongo amepoteza Mama Mkwe ambaye ni mke wa Mzee Edwin Mtei, hata hivyo hakukata tamaa, amefanikiwa kutuma salamu zake za rambirambi kupitia kwa mwakilishi wake ambapo ameonyesha masikitiko yake makubwa sana kwa kuondokewa na MZAA CHEMA katika kipindi hiki ambacho yuko jela kutokana na matakwa ya watawala.

Tutaweka video ya mwakilishi ikiwezekana ili kila mmoja ajionee mwenyewe.
 
Sema “...aliyeko gerezani kwa tuhuma za ugaidi...” (sio kwa “...kwa tuhuma za uongo...”)! Amemuongopea nani, labda?
 
Sote tunayo masikitiko makubwa kwa huyo, mh: aliyepachikwa tuhuma za uongu mtupu! M/Mungu amlinde na njama za watawala hawa wa awamu ya tano na sita wenye husuda. Tupo pamoja katika dua za kuwatakia kheri wote wana CDM ambao wamepewa tuhuma mbali mbali kwa ajiri ya kutaka kuendelea kwao kuwepo madarakani. #MBOWE SI GAIDI.
 
Sema “...aliyeko gerezani kwa tuhuma za ugaidi...” (sio kwa “...kwa tuhuma za uongo...”)! Amemuongopea nani, labda?
Ni tuhuma za uongo. OVA

Wewe jiulize hao Polisi wanaodai kuwa upelelezi wameshaukamilisha, ni kitu gani kinachowafanya wapate "mchecheto" kila kesi inapokuja mahakamani, watoe visingizio vya kitoto ili tu wacheleweshe kusikiliza kesi hiyo??
 
Apumzike kwa amani mama wa mke wa Kamanda. Pole sana kwa wana familia.
 
Karma itaifuata serikali ya CCM .

Ina nikumbusha yaliyomtokea yule mwandishi wa habari akashindwa kuhudhuria msiba na watu wengi walilia sana. Hakika watawala mioyo yao si ya nyama bali ni ya jiwe.

January 2, 2020

Ndugu, jamaa walia machozi kesi ya Kabendera kushindwa kuhudhuria mazishi.
 
Ka inchi kichafu haka...
Nchi zote zilizokuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa Afrika, zimebadilika na kuendelea mbele, Zambia, Mozambique, Kenya , Ethiopia, Nigeria, Ghana......

Lakini hiki ki inchi ni elimu ya kipuuzi inayofundishwa kutoa mizwazwa isiojielewa, ni ujasiri wa kujaribu, hata Zanzibar wanajaribu kutuonyesha ujasiri, lakini Tanzania imejaa mifisi tu................
 
Ni tuhuma za uongo. OVA

Wewe jiulize hao Polisi wanaodai kuwa upelelezi wameshaukamilisha, ni kitu gani kinachowafanya wapate "mchecheto" kila kesi inapokuja mahakamani, watoe visingizio vya kitoto ili tu wacheleweshe kusikiliza kesi hiyo??

Tuhuma za uongo ni pale mtu anapotuhumiwa kusema uongo. Sidhani kama anatuhumiwa kwa kosa hilo!
 
Ka inchi kichafu haka...
Nchi zote zilizokuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa africa, zimebadilika na kuendelea mbele, Zambia, Mozambique, Kenya , Ethiopia, Nigeria, Ghana......
Lakini hiki ki inchi ni elimu ya kipuuzi inayofundishwa kutoa mizwazwa isiojielewa
, ni ujasiri wa kujaribu, hata Zanzibar wanajaribu kutuonyesha ujasiri , lakini TZ imejaa mifisi tu................
Kenya umeipendea kitu gani mkuu, labda mahakama yake?

Kwa hilo nitaungana nawe, siyo kwa uchaguzi na matokeo ya haki. Au hujui huwa inakuwaje nyakati za chaguzi huko kwao?
Na zaidi, Kenya hajawahi kuwa "mstari wa mbele kwenye ukombozi wa Africa". Naona historia hiyo imekupita pembeni kabisa, kama hupotoshi kwa sababu unazozijuwa mwenyewe.
 
Back
Top Bottom