Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Ndugu Mohamed Dewji
Mwenyekiti wa Bodi
Bodi ya Wakurugenzi
Simba Sports Club
DAR ES SALAAM
YAH: MECHI YETU DHIDI YA YANGA AFRICANS A.K.A UTOPOLO SIKU YA TAREHE 08 MACHI 2025
Ndugu Mwenyekiti, pokea salamu hizi za dhati kabisa kutoka kwangu mwanachama wa Simba Sports Club.
Ndugu Mwenyekiti, kwanza nakupongeza sana wewe binafsi na Bodi nzima ya Klabu ya Simba kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuijenga Simba yetu.Hakika msimu huu pamoja na kuwa hatujabeba kombe lolote, lakini angalau tumepata amani ya moyo kwa timu yetu kubakia kuwa timu pekee iliyoingia hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho.
Ndugu Mwenyekiti, Jumamosi tarehe 08 Machi 2025 kuna mchezo mgumu sana dhidi ya wapinzani wetu Yanga.Timu hii huko nyuma tulikuwa tunaibeza kuwa sio lolote sio chochote kutokana na kusajili wachezaji wabovu, tukawa tunawatambia sana mitaani, maofisini na kila mahali, kwa kweli walikuwa hawana raha.
Ndugu Mwenyekiti, mambo yamebadilika baada ya Yanga kuchukuliwa na kudhaminiwa na GSM.Hawa jamaa kwa kweli mbinu, mikakati na mipango yao imewafanya wana Yanga wawe na amani na furaha na hivi sasa hata wakiambiwa wacheze na sisi asubuhi wako tayari.
Ndugu Mwenyekiti, Yanga wametufunga mara tano mfululizo, haijawahi kutokea tangu dunia iumbwe.Narudia tena, Yanga wametufunga mara tano mfululizo na katika mechi hizo tano walizotufunga kuna mechi moja walitudhalilisha kwa mabao 5 0 ya mchongo, siku ile sitoisahau maishani mwangu hadi naingia kaburini.
Ndugu Mwenyekiti, ndani ya klabu yetu kuna wanafiki wengi, miongoni mwao ndio hao hao walioshiriki kutuangamiza kwa kumpa michongo yote Injinia hadi wakatulamba mabao 5.Sisi tunaamini ile mechi ilikuwa mipango ya watu walipewa fedha wakauza ramani basi imekuwa wimbo kwao kila maeneo wameweka mabango.
Ndugu Mwenyekiti, dalili naziona wazi kabisa jamaa wanakwenda kutuadhibu tena.Nasema hivi kwa sababu sio kawaida mechi za Simba vs Yanga kuwaona wachezaji wanazurula mitaani lakini leo nimemuona Aziz Ki akiwa anafuturisha nyumbani kwake na mkewe Hamisa Mobetto huku chawa Mwijaku akisherehesha tukio hilo.
Ndugu Mwenyekiti, hadi unaona akina Aziz Ki wanazurula mitaani ujue jamaa wameshamaliza mchezo na jumamosi wanakwenda kukamilisha ratiba.Hii ni dharau kubwa sana kwetu Mwenyekiti.
Ndugu Mwenyekiti, najua wewe unaipenda Simba lakini wewe hutuzidi sisi, sisi Simba ikifungwa hata watoto tunawakasirikia wakiongea na sisi, mke hanogi kabisa Yanga akinifunga.Yaani maisha yanakuwa yameharibika kabisa kufungwa na Yanga.Hili jambo nyie mnalichukua rahisi sana lakini kaeni mkijua kuwa roho zetu zinakuwa rehani tukifungwa na Yanga.
Ndugu Mwenyekiti, Yanga anatufunga mara ya sita mfululizo wewe unajisikiaje.Yaani Jumamosi sisi tufungwe mara ya sita nyie viongozi wetu mnaona sawa kweli? Yaani tunakwenda uwanjani sisi tukiwa underdog kwa Yanga.Leo Aziz Ki yuko mtaani anakula futari wakati mechi ni Jumamosi.
Ndugu Mwenyekiti, nakuomba sana, sitaki kukuchosha, naandika haya kwa niaba ya wanasimba wenzangu ambao hawapendi ujinga na kuona tunafungwa mara ya sita mfululizo na timu ambayo tunaimudu.MwanaSIMBA yeyote anayeipenda Simba hayuko tayari mwezi huu wa Ramadhan aingiwe majonzi na simanzi.
Ndugu Mwwenyekiti, namaliza, hadi sasa tuko nusu kwa nusu kusaka ubingwa, Ubaya Ubwela umefanya kazi yake, kama Yanga atatufunga mtakuwa mmetukatisha sana tamaa sisi wanachama, mashabiki na wapenzi.
Nauomba uongozi, ule uwanja wa Bunju nna mashaka nao sana, uwanja ule tangu tuanze kuutumia umekuwa shubiri kila tunapocheza na Yanga.Uwanja wa Bunju umekuwa wa kufungwa na kutoka sare na Yanga, sikumbuki lini tulimfunga Yanga tukitokea Bunju.Ule uwanja uko jirani na makazi ya watu, sisi tunafanya mazoezi halafu usiku watu wa utopolo wanaruka na kuingia ndani ya uwanja wanachukua nyasi na mazagazaga mengine, matokeo yake nyota zetu zote wanachukua wao.
Ndugu Mwenyekiti, sisi wanasimba tunakuamini sana ila tuna mashaka na wenzako unaowafanya nao kazi, kwa kweli nakuombeni sana tumechoka tumechoka tumechoka tumechoka kufungwa na Yanga.Kama kazi hamuiwezi leteni timu kwa mashabiki huku tufanye kazi wenyewe.Asante.