Nahisi hii imetokea kwa wote ambao wanacheki namba. Yaani salary slip ya mwezi July inaonesha hela imeenda HESLB lakini kwenye akaunti ya HESLB-OLAMS deni haliko updated.
Binafsi naona tuwasubiri bodi mpaka tarehe tano Agost na kuendelea, labda bado hawaja-update kwenye mfumo wao, au bado hazina hawajapeleka hela kwenye akaunti zetu za bodi.
KUWAPONDA BODI;
Kwa nini bodi wanakuwa wababaishaji kuhusu madeni ya wadaiwa. Mwanzoni mwa mwaka huu, walisema wataunganisha mfumo wa bodi na hazina ambapo kila mdaiwa atakuwa anaona deni lake kila anapolipa.
Sasa leo mwezi wa saba bado hawajaunganisha huo mfumo maana yake nini?
Je, hawaoni kwamba wasipounganisha mfumo wa bodi, na hazina mtu anaweza kuwa amemaliza deni lakini anaendelea kukatwa na hazina? Ikumbukwe, baada kuondoa VRF, wadaiwa wengi deni halisi limepungua kwenye akaunti ya OLAMS-HESLB, lakini kwenye salary slip deni ni kubwa! Deni halisi lipo bodi.
Kama bodi walikuwa chapu kupeleka makato kwa waajiri, je, ni kitu gani kinawafanya washindwe kupeleka deni halisi hazina baada ya kuondoa VRF? Yaani wapo shapu kukata ila wamekuwa wazito kuhuisha taarifa hazina!
Je, wataalamu wa TEHAMA hapo bodi hawana uwezo wa kushughulikia hili suala la madeni bila kufika ofisini? Kwa mfano, tangu juni niliomba bank statement ila mpaka leo sijapata! Halafu website yao nzito kweli. Sections ambapo zipo kwenye website ni kama mapambo tu, uki-click hazifunguki. Ukiomba statement unaambiwa subiri. Sasa si wawatafute hata watengeneza blogu wawasaidie kuweka sawa hiyo tovuti!