Salary slip yangu haioneshi deni langu kukatwa, Je nikope benki nyingine

Salary slip yangu haioneshi deni langu kukatwa, Je nikope benki nyingine

sometimesyes

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2017
Posts
360
Reaction score
288
Wasomi habari zenu,

Naomba nirukie moja kwa moja kwenye mada

Mimi ni mtumishi wa umma ambae nna mkopo benki fulani, na deni hata mwaka halijmaliza mwaka, sasa nimeshangaa kweney salary slip yangu ya mwezi Oktoba lile deni halipo na mshahara haujakatwa, napata majaribu kukopa taasisI nyingine ya kifedha.

Swali, endapo nitafanya hivyo na wakashtuka, kisheria itakua vipi hapo, wanaweza kuendelea kukata mshahara uliobaki au naweza kula mvua wazee wenzangu?

Nawasilisha
 
Kausha acha wenge, wasikilizie kama mwaka 1
 
Maamuzi yoyote unayofanya katika maisha yako hakikisha kwanza umeridhia kuwajibika na kubeba msalaba wako kwa lolote.

Ukishajihakikishia suala la kuwajibika sasa ndipo uanze utekelezaji wa maamuzi.

Kama kuna sehemu unaweza pata pesa na kulipa muda wowote basi sikilizia hilo deni ila kama hakuna fanya maamuzi ya busara kulipa deni.

Madeni huwa ni ya kawaida wakati wa kupokea pesa na kutumia tu, ila wakati wa kulipa na kuwajibika hapo huwa mambo yanabadilika mkuu.

Umekopa pesa then rudisha, hii mambo ya kusikilizia ni sawa na mtu anayerundika mizigo matokeo yake ikimzidi uwezo anaanza kulia Laiti angelijua
 
Utaratibu uko hivi Kuna baadhi ya Taasisi kama mtumishi wa umma ,unapokopa unapitisha mpk miez miwili ndio makato yanaanza rasmi hazina , usije kwenda kukopa kwingine itafanya uwe unakatwa ndani ya benk kwa standing oder familia itayumba jaribu kurudhika
 
Wasomi habari zenu,

Naomba nirukie moja kwa moja kwenye mada

Mimi ni mtumishi wa umma ambae nna mkopo benki fulani, na deni hata mwaka halijmaliza mwaka, sasa nimeshangaa kweney salary slip yangu ya mwezi Oktoba lile deni halipo na mshahara haujakatwa, napata majaribu kukopa taasisI nyingine ya kifedha.

Swali, endapo nitafanya hivyo na wakashtuka, kisheria itakua vipi hapo, wanaweza kuendelea kukata mshahara uliobaki au naweza kula mvua wazee wenzangu?

Nawasilisha
weka hapa tuone
 
Mimi ilishawahi kunitokea hii, ilikuwa mwaka 2009, nilikopa bank fulani hivi, baada ya miezi kadhaa deni likawa halipo kwenye salary slip na mshahara haukatwi, nikasubiri mpaka mwaka 2012 ndipo nikakopa kwenye bank nyingine baada ya kuona hakuna tena makato.

Sasa mwaka jana mwanzoni nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa hiyo bank, (maana namba ya simu niliyonayo niliijaza kwenye fomu ya mkopo) akaniambia kwamba nadaiwa mkopo na yeye amepewa kazi ya kufuatilia madeni sugu, alianza kama kwa kutaka kunitisha ili niogope, jibu langu lilikuwa rahisi tu, nilimwambia Mimi nilikopa huo mkopo kwa kutumia mshahara, nilidhaminiwa na Mwajiri wangu na nilikuwa nakatwa moja kwa moja kutokea hazina, hivyo Mimi sihusiki na uzembe wowote uliotokea.

Siku za baadae akawa mpole huku akinishawishi nipunguze deni kidogo, kidogo, kilichonisaidia ni kwa kuwa sasa hivi sipo kwenye Utumishi wa Umma, maana kama bado upo Utumishini ni rahisi kuingiziwa makato upya kwenye mshahara.
 
Tulia kwanza. Halafu hata huku unapiga kelele. Ni hela hizo ungekaa kimya peke yako na moyo wako.

Sasa fanya hivi kama una uvumilivu. Hiyo pesa iliyotakiwa ikatwe ifungulie akaunt isiyo ruhusu kutoa. Kila mwezi toa humo kiwango ulichotakiwa ukatwe kitunze huko. Ishi maisha kama unakatwa
 
Naomba kuuliza ,Kuna baadhi ya masharti ya kazi ukiomba wanakwambia uwe hujawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote,Sasa swali je Kama nimewahi kufungwa na kosa Hilo nikalikatia rufaa halafu nikashinda rufaa,je kipengere Cha kutiwa hatiani kitakuwa bado kinanibana?
 
Mifumo imezingua ila watakutafuta tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naomba kuuliza ,Kuna baadhi ya masharti ya kazi ukiomba wanakwambia uwe hujawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote,Sasa swali je Kama nimewahi kufungwa na kosa Hilo nikalikatia rufaa halafu nikashinda rufaa,je kipengere Cha kutiwa hatiani kitakuwa bado kinanibana?
Imekula kwako,ni sawa na Sabaya tuu hatakanyaga tena kwenye ofisi za Umma.
 
Naomba kuuliza ,Kuna baadhi ya masharti ya kazi ukiomba wanakwambia uwe hujawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote,Sasa swali je Kama nimewahi kufungwa na kosa Hilo nikalikatia rufaa halafu nikashinda rufaa,je kipengere Cha kutiwa hatiani kitakuwa bado kinanibana?
Linakuwa limefutwa na hata wakikuuliza wape judgement
 
Back
Top Bottom