Salim Himidi: Comrade wa Ngazija

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SALIM HIMIDI KUMBUKUMBU: COMRADE WA NGAZIJA

Hukaa nikawaza wakati mwingine vijana wa Kizanzibari Makomredi jinsi walivyowanyima usingizi Wamarekani.

Najiuliza ingekuwaje makoredi wa Zanzibar na Comoro wangekamata dola katika visiwa hivi Zanzibar na Ngazija?

Leo imetimu miaka miwili toka rafiki yangu na kwa hakika rafiki ya wengi waliojaaliwa kumjua Salim Himidi alipofariki Paris, Ufaransa.

Mmoja wa marafiki zake marehemu Salim Himid baada ya kusoma kumbukumbu yangu fupi ya mwaka mmoja toka kufariki Salim Himidi ambayo nilisema kuwa alkuwa mkimbizi Ufaransa aliniandikia kunisahihisha kuwa Salim Himidi hakwenda Ufaransa kama mkimbizi.

Hebu msome kuhusu hilo na mengine aliyotuongezea ili wale ambao hawakuwa wanamjua wamjue Salim Himidi alikuwa mtu wa ana gani:

":... alihamia hasa kwa ukaazi Paris baada ya kifo cha Rais Mohamed Taki ambapo wakati ule yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Wakati wa Ali Soilihi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Utawala wa Said Johari Salim alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Kila aliyeingia madarakani alihitaji utumishi wake.

Alipofunguliwa jela baada ya serikali kuangushwa na askari mamluki aliitwa Ikulu na Ahmed Abdullah.

Waliotumwa kupeleka ujumbe wakamwambia Ahmed Abdullah unataka kumteuwa yule Comrade Mswahili wale ndo walokupindua 1975.

Ahmed Abdulla alijibu, "Mimi namhitaji Salim kwa ujuzi, maarifa na uchapa kazi wake.

Ucomrade na uwanja wa mapinduzi ni wake mwenyewe."

Alipokutana naye akamsimulia yaliosemwa na akamwambia amemteuwa Katibu Mkuu wake.

Salim alimjibu atafikiria.
Lakini jibu la Abdullah lilikuwa tutaonana kesho ofisini."

Picha: Salim Himidi na Nelson Mandela, Salim Himidi akihutuba UN na Salim akiwa pembeni ya Leopold Senghor.

 
Mzee Mohamed, Hivi hunaga simulizi za Mkiristo hata mmoja Katika maisha yako? Hujawahi kuishi ama kufahamiana na waliompokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao?!
 
Mzee Mohamed, Hivi hunaga simulizi za Mkiristo hata mmoja Katika maisha yako? Hujawahi kuishi ama kufahamiana na waliompokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wao?!
Uzalendo...
Ninazo simulizi.
Unaweza kusoma simulizi hizo katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…