Salim Himidi kumbukumbu mwaka mmoja

Salim Himidi kumbukumbu mwaka mmoja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SALIM HIMIDI KUMBUKUMBU MWAKA MMOJA

Leo imetimu mwaka mmoja toka rafiki yangu na kwa hakika rafiki ya wengi waliojaaliwa kumjua kufariki Paris alipokuwa anaishi uhamishoni toka Comoro ilipovamiwa na askari mamluki wakiongozwa na Bob Denard.

Picha ya nne niko na Salim Himidi Msikiti Mkuu wa Paris Sala ya Ijumaa.

Habari za ziada:

Mmoja wa marafiki zake marehemu Salim Himid baada ya kusoma hiyo kumbukumbumbu yangu fupi kaniandikia hasa kwa kusahihisha kuwa Salim Himidi hakwenda Ufaransa kama mkimbizi.

Hebu msome kuhusu hilo na mengine aliyotuongezea:

":... alihamia hasa kwa ukaazi Paris baada ya kifo cha Rais Mohamed Taki ambapo wakati ule yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Wakati wa Ali Soilihi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Utawala wa Said Johari Salim alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Kila aliyeingia madarakani alihitaji utumishi wake.

Alipofunguliwa jela baada ya serikali kuangushwa na askari mamluki aliitwa Ikulu na Ahmed Abdullah.

Waliotumwa kupeleka ujumbe wakamwambia Ahmed Abdullah unataka kumteuwa yule Comrade Mswahili wale ndo walokupindua 1975.

Ahmed Abdulla alijibu, "Mimi namhitaji Salim kwa ujuzi, maarifa na uchapa kazi wake. Ucomrade na uwanja wa mapinduzi ni wake mwenyewe.""

Alipokutana naye akamsimulia yaliosemwa na akamwambia amemteuwa Katibu Mkuu wake.

Salim alimjibu atafikiria.

Lakini jibu la Abdullah lilikuwa tutaonana kesho ofisini."

Picha ya kwanza kushoto ni Salim Himidi na pembeni yake ni Leopold Senghor.

IMG-20210309-WA0254.jpg
IMG-20210309-WA0188.jpg
Screenshot_20210309-184322.jpg
 
Back
Top Bottom