Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Salim alikuwa hapendi tule kwenye migahawa yenye vyakula vya Kizungu na siku zote akinipeleka migahawa ya Kihindi na kuna mgahawa mmoja akiupenda sana.
Mwenye mgahawa huu alikuwa Mzanzibari ambae baba yake alikimbilia Ufaransa baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1964 na baada ya baba yake kufariki mwanae akawa anauendesha.
Hapo tutaagiza chai, chapati, sambusa na kababu pamoja na chatney yake. Ukitukuta hapo tunakunywa chai na ukatupia jicho sahani zetu wala huwezi kujua kama tuko katikati ya jiji la Paris, utadhani labda tuko ‘’Passing Show,’’ Malindi, au mgahawa wowote Stone Town, Zanzibar.
Tutakunywa chai huku tukisikiliza muziki wa Kihindi wa Lata Mangeshkar, Asha Bhosle, Mohamed Rafi na Mukesh uliokuwa ukipigwa kwa sauti ya chini sana.
Nilijua Salim akiwa hapa alikuwa anarejea udogoni Zanzibar akiiwaza Zanzibar ambayo haitaweza kurudi tena.
Salim akinihadithia utoto wake nyumbani Zanzibar na vipi filamu za Kihindi na nyimbo zake zilivyokuwa zikisikilizwa kila nyumba na vipi wacheza senama wa Kihindi kama Raj Kapoor, Dev Anand, Dilip Kumar, Nargis, Madhubala walivyokuwa maarufu visiwani.
PICHA: Picha hii nimempiga Bwanatosha akiwa kwenye mgahawa wake aupendao wa Kihindi Paris.