Salima Mukansanga Refa wa kwanza mwanamke katika mashindano ya Afcon

Salima Mukansanga Refa wa kwanza mwanamke katika mashindano ya Afcon

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
1642399427325.png

Picha: Salima Mukansanga

Salima Mukansanga ameweka historia kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu nchini Cameroon, kwa kuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke kwenye mashindano ya wanaume.

Mnyarwanda huyo mwenye umri wa miaka 33 alisimamia mchuano wa Afcon siku ya Jumatatu. Huko nyuma ameongoza mechi za Kombe la Dunia la Fifa kwa Wanawake, Olimpiki ya Tokyo 2020, Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) - pamoja na kusimamia michuano ya timu za juu za wanaume nchini mwake.

Vyombo vya habari vya Rwanda vinaripoti kuwa akiwa kijana Bi Mukansanga alikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa mpira wa vikapu kitaaluma, lakini akachagua kuwa mwamuzi wa soka miaka 15 iliyopita.
 
Back
Top Bottom