Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
Hatimaye Meneja wa Wasfi Classic Baby (WCB), Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha Harmonize kaandika barua ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB.

Amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na karibuni watakuwa na kikao cha kukubaliana 'terms' ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na 'terms' zote za kuvunja mkataba.

Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa unaonyeshwa na msanii huyo siku za karibuni lakini amewaomba mashabiki wa Wasafi waendelee kutoa ushirikiano kwa Harmonize kwani ajaondoka kwa ubaya.

Sallam amesema katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafsi, kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa amejitenga.

Sallam amesema kwa sasa Harmonize moyo wake haupo Wasafi lakini ukweli ni kuwa bado ana mkataba na kundi hilo.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema, “Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.”

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam.


Mtazamo wangu;

Harmonize anaenda kuwa historia kwenye muziki wa bongofleva uenda tukashangaa sana pale ambapo hatutasikia tena muziki wa kueleweka kutoka kwake na ukawa mwisho wake kisanaa.

Waliomshauri Hamo anapaswa kuwachukia maisha yake yote kama waliomshauri Mavoko.
 
Namtakia kila la kheri Harmonize!
Kama ameona WCB hawawezi mfikisha anapo pahitaji basi si vibaya kwenda kuangalia njia nyingine!
Pia nampongeza kwa kutaka kuondoka kwa amani kwa kutumia mlango alio ingilia!

Lakini matarajio yetu ni kuona ana songa mbele zaidi ili ku tuprove wrong na kuonesha kwambwa amefika ambapo WCB wameshindwa kumfikisha!

Namtakia kila la kheri
 
Dua la kuku........... kwani mtu akikua c anaondoka kwa wazazi wake mbona mmemuwekea kinyongo au lebo ndo inamtegemea yeye akiondoka kuna mkwaja utakata???
Time will tell atarudi kuwalaumu Wasafi ndio wanamkwamisha.. Hamo hana talent ya kusimama nje ya Wasafi evidence project yake na Q chilla imeangukia pua pamoja na mkwanja mrefu alioweka
 
Back
Top Bottom