maukijunior
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 233
- 366
iko u tubeSource ya uzi wako...?
Hata mavoko alionyesha uthubutu mkampongeza, kiko wapi?Harmonize ni lini aliuza mitumba Tandale? Hii ni fact ndogo ambayo inaondoa maana ya yote uliyoyaandika.
Nawashangaa sana mnaosema Harmonize kakosea kubadili management... Hivi nyie mnaijua WCB kuliko Harmonize?
Harmonize ni mtu wa ndani wa WCB, anajua mengi kuliko mtu yeyote nje ya WCB. Acheni kuleta siasa ktk masuala career za watu.
Huu uchambuzi wenu hauna maana yoyote maana tasnia ya muziki inahusisha mambo ya ndani ambayo hatuyajui tofauti na mpira unaochezwa hadharani ndio maana mtu unaweza kufanya uchambuzi ila sio muziki wetu uliobeba fitna za kila namna.
Mimi naona tumtakie heri kijana wetu, ameonesha uthubutu muacheni asonge mbele acheni hizi ramli zenu chonganishi.
Ngedere weweHizo style zinazochezwa kwenye hizo videos ulizotaja mbona video kibao za Nigeria wanazitumia kabla hata ya mwaka jana. Diamond kazichukua tu kazi-compile... Huyo unayesema kazivumbua mwambie akuambiye tena.
Yale maisha ya Instagram achana nayo , nenda kwenye account yake ya Instagram mwambie ule mchango Wa harusi alioahidi kutoka million 3 alitoa ?? Na rayvan alimchangia shilling ngapi ??Rayvan huyu huyu ambae baby mama wake alituambia wanatumia mil. 9 kwa photoshoot?
[emoji38][emoji38][emoji38]Vipi sikuhizi umehama Team Kiba?Wewe ni kati ya wasioujua muziki lakini una ujuaji mwingi ilhali huna ulijualo.
Unasema Lavalava sio msanii na nyimbo zake hazieleweki? Mimi sio shabiki wa hiyo WCB yenu ila Lavalava ndio msanii wangu bora pale WCB na hizo nyimbo zake unazosema huzielewi ndio nimejua hujui muziki.
Unathubutuje kusema mtu mwenye vibao vitamu kama Bora Tuachane, Utatulia, Go Gaga na wimbo wangu bora wa muda wote kwa Lavalava, Kilio sio msanii?
Wewe jamaa umejua kuniharibia asubuhi yangu!
Mkuu acha kabisa kuna siku huyo rayvan kakosa hela ya mafuta kutoka kwake tabata mpaka Mbezi .. Wengi Wa mashabiki wanadanganywa na zile picha za Instagram tu ...
Watu hawawezi amini kuwa rich mavoko licha ya kutoa zile hitsong alikuwa hana hata mia mfukoni na akipata show hao utatu mtakatifu wanachukua cha kwao na Wcb kwa ujumla na kinachobaki ndio anapewa...
Kuna Dogo mmoja diamond alimchukua kutoka Sweden ndio kachukua nafasi ya Moses iyoyo kama dancer instructor Wa wcb, nimekutana nae face to face na anajuta kuingia wcb ... Huyo Dogo ndio kabuni dance styles kwenye nyimbo zote za wcb kuanzia mwaka Jana . nyegezi, tetema, inama n.k ...
Well saidMi namtakia mmakonde kila la kheri kwenye maisha yake mapya nje ya WCB, ila ajue kwamba safari aliyoianza sio rahisi, apambane sana tusije tukamcheka huko mbeleni
Noorah kipindi yupo na hit ya ice cream alikuwa chini ya jembe ni jembeLabel ziko nyingi mimi nlijua labda amesign label ya nje ambayo ingembeba zaidi ya wcb.tuwe wakweli jembe hawezi kumjenga kumziki mana hajawahi kumsimamia msanii yeyote kimuziki,yetu macho na masikio tutaona yajayo
Jembe hatokula hela ya mmakonde anatembea nae tuKatika kitu Harmonize amefanya kikubwa katika maisha yake ni kuingia WCB na kizuri kikubwa zaidi nI kutoka WCB naamin ameshapata platform ya mashabiki wa kutosha ni vema sasa aishi maisha yake sio kusindikiza tena kuna mtu hapo amesema kwamba kama4 Diamond anakatwa 30% ya show inaingia kwa hao mameneja yeye ni nani asikatwe hiyo % lakin mimi naona huo ni ujinga mkubwa sana yaani manager watatu wachukue 30% bado manager wake nae achukue bado nyingine ibaki kwa kampuni cmon! Labda kama show inalipa 100m but hamna show ya namna hiyo na kijana hapo ndio akaanze kufanya maisha sasa ya uhalisia wala asikatishwe tamaa na hawa washabiki wa WCB maana kama Jux anaishi hayupo wcb, Aslay anaishi maisha mazuri tu yeye kwa nini ang'ang'ane na maisha ya kishowoff platform aliyonayo inamtosha kutoboa kimaisha ukipata chochote sasa ni cha kwake hakuna kugawana sijui na manager watatu wala wcb namuonea huruma tu Rayvan bado hajapata akili ya maisha ila kama akifumbuliwa macho ndio ataelewa ila abaki kwanza atengeneze jina na akili ipanuke
Label ziko nyingi mimi nlijua labda amesign label ya nje ambayo ingembeba zaidi ya wcb.tuwe wakweli jembe hawezi kumjenga kumziki mana hajawahi kumsimamia msanii yeyote kimuziki,yetu macho na masikio tutaona yajayo